KERO Baadhi ya Wafanyabiashara Soko la Soweto na Uyole (Mbeya) wanauza Samaki walioharibika kwa makusudi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mwanongwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2023
Posts
611
Reaction score
567
Habari Wana jukwaa la JamiiForums, leo nimekuja na jambo hili linalowahusu hawa Wafanyabiashara wa Samaki katika masoko ya Soweto na Uyole jijini Mbeya.

Baadhi ya hao watu hawajali kabisa afya za watu, maana wamekuwa na utaratibu wa kuuza Samaki ambao tayari wameharibika na hawafai kwa matumizi.

Mimi ni mhanga wa hao Wafanyabiashara hasa wa Soko la Uyole maana ndiyo lipo karibu na kwangu, hivyo huduma muhimu nazipata pale.
DSCPDC_0000_BURST20241201084549401.JPG
Kuna wale Samaki Wakavu, mwanzo nilikuwa najua wale ndiyo salama kuliko Samaki wa Bichi kumbe nilikuwa najidanganya.

Kuna siku Mwanongwa wa watu nikajichanganya nikanunua Samaki aina ya Kambale ambaye amekaushwa kwa kutumia Moshi, nilivyofika nyumbani na kumuweka kwenye maji ya Moto nikaona wadudu aina ya funza wakitoka kwenye Samaki.

Kesho yake nikaenda sokoni na yule Samaki na kumuonesha muuzaji, alichonijibu ni kuwa yupo tayari kunibadilishia Samaki na siyo kurudisha fedha, nikaachana naye na kuondoka.
DSCPDC_0002_BURST20241201084549401.JPG

WhatsApp Image 2025-01-06 at 10.50.34_127b92c7.jpg
Baada ya muda nikaamua kufanya uchunguzi kangu kuhusu Wafanyabiashara wenye tabia kama hizo, nikampata kijana mmoja ambaye ameajiriwa kwenye duka la Samaki (Fresh food).

Huyo kijana alinisimulia jinsi ambavyo Wafanyabiashara hao wa Samaki wanavyofanya, anadai wale Samaki wabichi wakianza kuharibika baada ya kukaa muda mrefu kwenye majokofu wanaamua kuwakaanga kwenye mafuta na kuwauza.

Hivyo, wanafanya huku wakijua kabisa kwamba Samaki hao hawafai kwa matumizi ya binadamu, ila kwa kuogopa hasara wanaamua kuwauzia watu Samaki waliyoharibika.

Ukiachana na hao Samaki wa bichi, kuna hawa Samaki wa kukaushwa kwa Moshi, hawa ni vigumu sana kutambua kama wameharibika mpaka ukifanikiwa kuwaweka kwenye maji ya Moto ndiyo utaona wadudu wanavyotoka.

Wafanyabiashara wa Samaki hawa wakavu mara nyingi huwa wanachukua blashi na mafuta ya kupikia, kisha wanaanza kuwapaka Samaki hao ili waonekane wanahali nzuri lakini kumbe ni balaa.

Hivi kama kitu kimekudodea mpaka kimeharibika kuna haja gani ya kuendelea kukiuza na kupelekea kuziweka hatarini afya za watu? Si bora ukatupe tu.

Na ninyi ma bwana afya mliopo sokoni, hivi kazi yenu mnaijua kweli au ndiyo kutwa kuchukua rushwa na kushindwa kusimamia misingi ya kazi zenu.

Wafanyabiashara wa Soko la Soweto na Soko la Uyole hiyo tabia mnayoifanya ni sawa sawa na uchawi, hivi unawezaje kumlisha binadamu mwenzio kitu kilichooza na mkiambiwa mnakuwa wakali.

Serikali ifuatilieni watu wenu mliowapa dhamana ya kusimamia na kukagua maduka ya vyakula, wanashindwa kuzifanya kazi zao kwa weledi matokeo yake kutwa wanarudi na vifungashio nyumbani vimejaa rushwa za Samaki, kuku na vitu vingine vingi ili wawe kimya.

Tunakoelekea tutatoana ngeu kwa kweli maana hii sasa imezidi hata kama ni kutafuta pesa ila siyo kwa staili hii.

Mwanongwa nawakumbusha tu kuwa hii tabia siyo nzuri ipo siku mtaua binadamu wenzenu kwa kuwauzia chakula kilichooza.
 
hadi mihogo, wanajua kabisa ni mibaya lakini utakuta wanawabambikizia watu, hasahasa watoto,.....
 
Aisee mwezi uliopita hata mimi nilinunua kambale wa kukausha, tena nilichagua mkubwa kabisa. Kufika nyumbani kucheki naona funza wanadondoka nilishangaa sana. Nahisi ule mtikisiko njiani walishtuka wakachanganyikiwa. Sokoni niliwaona wako poa tu.

Niliwatupa palepale. Kilichoniuma sana ni hela yangu tu
 
Habari Wana jukwaa la JamiiForums, leo nimekuja na jambo hili linalowahusu hawa wafanyabiashara wa Samaki katika masoko ya Soweto na Uyole jijini Mbeya.

Baadhi ya hao watu hawajali kabisa afya za watu, maana wamekuwa na utaratibu wa kuuza Samaki ambao tayari wameharibika na hawafai kwa matumizi.

Mimi ni mhanga wa hao wafanyabiashara hasa wa Soko la Uyole maana ndiyo lipo karibu na kwangu, hivyo huduma muhimu nazipata pale.
Kuna wale Samaki Wakavu, mwanzo nilikuwa najua wale ndiyo salama kuliko Samaki wa Bichi kumbe nilikuwa najidanganya.

Kuna siku Mwanongwa wa watu nikajichanganya nikanunua Samaki aina ya Kambale ambaye amekaushwa kwa kutumia Moshi, nilivyofika nyumbani na kumuweka kwenye maji ya Moto nikaona wadudu aina ya funza wakitoka kwenye Samaki.

Kesho yake nikaenda sokoni na yule Samaki na kumuonesha muuzaji, alichonijibu ni kuwa yupo tayari kunibadilishia Samaki na siyo kurudisha fedha, nikaachana naye na kuondoka.
Baada ya muda nikaamua kufanya uchunguzi kangu kuhusu wafanyabiashara wenye tabia kama hizo, nikampata kijana mmoja ambaye ameajiriwa kwenye duka la Samaki (Fresh food).

Huyo kijana alinisimulia jinsi ambavyo Wafanyabiashara hao wa Samaki wanavyofanya, anadai wale Samaki wabichi wakianza kuharibika baada ya kukaa muda mrefu kwenye majokofu wanaamua kuwakaanga kwenye mafuta na kuwauza.

Hivyo, wanafanya huku wakijua kabisa kwamba Samaki hao hawafai kwa matumizi ya binadamu, ila kwa kuogopa hasara wanaamua kuwauzia watu Samaki waliyoharibika.

Ukiachana na hao Samaki wa bichi, kuna hawa Samaki wa kukaushwa kwa Moshi, hawa ni vigumu sana kutambua kama wameharibika mpaka ukifanikiwa kuwaweka kwenye maji tena ya Moto ndiyo utaona wadudu wanavyotoka.

Wafanyabiashara wa Samaki hawa wakavu mara nyingi huwa wanachukua blashi na mafuta ya kupikia, kisha wanaanza kuwapaka Samaki hao ili waonekane wanahali nzuri lakini kumbe ni balaa.

Hivi kama kitu kimekudodea mpaka kimeharibika kuna haja gani ya kuendelea kukiuza na kupelekea kuziweka hatarini afya za watu? Si bora ukatupe tu.

Na ninyi ma bwana afya mliopo sokoni, hivi kazi yenu mnaijua kweli au ndiyo kutwa kuchukua rushwa na kushindwa kusimamia misingi ya kazi zenu.

Wafanyabiashara wa Soko la Soweto na Soko la Uyole hiyo tabia mnayoifanya ni sawa sawa na uchawi, hivi unawezaje kumlisha binadamu mwenzio kitu kilichooza na mkiambiwa mnakuwa wakali.

Serikali ifuatilieni watu wenu mliowapa dhamana ya kusimamia na kukagua maduka ya vyakula, wanashindwa kuzifanya kazi zao kwa weledi matokeo yake kutwa wanarudi na vifungashio nyumbani vimejaa rushwa za Samaki, kuku na vitu vingine vingi ili wawe kimya.

Tunakoelekea tutatoana ngeu kwa kweli maana hii sasa imezidi hata kama ni kutafuta pesa ila siyo kwa staili hii.

Mwanongwa nawakumbusha tu kuwa hii tabia siyo nzuri ipo siku mtaua binadamu wenzenu kwa kuwauzia chakula kilichooza.
Tafadhari mkuu naomba unambie madhara ya samaki aliyeharibika/kuchina na badae kukaangwa ana madhara gani?

Mkuu bila shaka hujawahi ishi ziwani. 87% ya samaki waliobanikwa huwa wapo katika hali ya kuharibika na ili kuwaokoa hubanikwa hadi kuakauka ndio maana huwa na harufu kali sana hata akipikwa.

Kama ukihitaji samaki fresh mzuri nenda mwaloni kanunue huko hata hao wa kwenye mabucha ya samaki huoshewa chemical ya kutunzia maiti ili wasiharibike ndio maana unaweza mkuta samaki ni mbichi lakini mkavuu na hana dalili za kuharibika.Sio samaki tu hata nyama mabuchani. Popote kwenye nzi wengi hiyo nyma ni salama ukikuta hakuna nzi na ukavutiwa nayo kwisha habari yako...Bila shaka humu kuna watu wenye mabucha watatoa waliyo nayo kuhusu hili la dawa za maiti.

Mimi nilikuwa na rafiki yangu mkulya alikuwa na bucha nikienda kununua nyama alikuwa ananimbia kanunue kwa fln badae ndo akaniambia maana alikuwa ananiita msabato namna nilivyokuwa najari afya .

Nambie madhara ya yake sasa mkuu
 
Aisee mwezi uliopita hata mimi nilinunua kambale wa kukausha, tena nilichagua mkubwa kabisa. Kufika nyumbani kucheki naona funza wanadondoka nilishangaa sana. Nahisi ule mtikisiko njiani walishtuka wakachanganyikiwa. Sokoni niliwaona wako poa tu.

Niliwatupa palepale. Kilichoniuma sana ni hela yangu tu
Hatari sana
 
Tafadhari mkuu naomba unambie madhara ya samaki aliyeharibika/kuchina na badae kukaangwa ana madhara gani?

Mkuu bila shaka hujawahi ishi ziwani. 87% ya samaki waliobanikwa huwa wapo katika hali ya kuharibika na ili kuwaokoa hubanikwa hadi kuakauka ndio maana huwa na harufu kali sana hata akipikwa.

Kama ukihitaji samaki fresh mzuri nenda mwaloni kanunue huko hata hao wa kwenye mabucha ya samaki huoshewa chemical ya kutunzia maiti ili wasiharibike ndio maana unaweza mkuta samaki ni mbichi lakini mkavuu na hana dalili za kuharibika.Sio samaki tu hata nyama mabuchani. Popote kwenye nzi wengi hiyo nyma ni salama ukikuta hakuna nzi na ukavutiwa nayo kwisha habari yako...Bila shaka humu kuna watu wenye mabucha watatoa waliyo nayo kuhusu hili la dawa za maiti.

Mimi nilikuwa na rafiki yangu mkulya alikuwa na bucha nikienda kununua nyama alikuwa ananimbia kanunue kwa fln badae ndo akaniambia maana alikuwa ananiita msabato namna nilivyokuwa najari afya .

Nambie madhara ya yake sasa mkuu
Daaah
 
Saizi kila kitu feki, nimenunua dawa za kuku mbili kuwapa kuku wanazidi kuumwa baada ya kupona, baadae nikagundua ule muhuri wa expire date umefutika wote maanake niliuziwa dawa feki na kuku wamekufa wawili tayari
Pole sana
 
Umenikumbusha mbali sana...tuko na mazaa anapika mboga mara kuweka samaki kwenye sufuria la moto wadudu wakatoka wanaruka ruka...alibeba sufuria kama lilivyo akampelekea muuzaji...muuzaji alimrudishia hela maana alikua muwazi tu samaki zote ziko ivo ni za kitambo bado hajafwata mzigo mpya
 
Balaaaa
 
Back
Top Bottom