Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Anaweza kusababisha magonjwa ya tumboTafadhari mkuu naomba unambie madhara ya samaki aliyeharibika/kuchina na badae kukaangwa ana madhara gani?
Mkuu bila shaka hujawahi ishi ziwani. 87% ya samaki waliobanikwa huwa wapo katika hali ya kuharibika na ili kuwaokoa hubanikwa hadi kuakauka ndio maana huwa na harufu kali sana hata akipikwa.
Kama ukihitaji samaki fresh mzuri nenda mwaloni kanunue huko hata hao wa kwenye mabucha ya samaki huoshewa chemical ya kutunzia maiti ili wasiharibike ndio maana unaweza mkuta samaki ni mbichi lakini mkavuu na hana dalili za kuharibika.Sio samaki tu hata nyama mabuchani. Popote kwenye nzi wengi hiyo nyma ni salama ukikuta hakuna nzi na ukavutiwa nayo kwisha habari yako...Bila shaka humu kuna watu wenye mabucha watatoa waliyo nayo kuhusu hili la dawa za maiti.
Mimi nilikuwa na rafiki yangu mkulya alikuwa na bucha nikienda kununua nyama alikuwa ananimbia kanunue kwa fln badae ndo akaniambia maana alikuwa ananiita msabato namna nilivyokuwa najari afya .
Nambie madhara ya yake sasa mkuu
Hebu weka picha tuwaone hao "Samaki wa Bichi" walivyo kama wanafanana na samaki wa baharini au la.Habari Wana jukwaa la JamiiForums, leo nimekuja na jambo hili linalowahusu hawa Wafanyabiashara wa Samaki katika masoko ya Soweto na Uyole jijini Mbeya.
Baadhi ya hao watu hawajali kabisa afya za watu, maana wamekuwa na utaratibu wa kuuza Samaki ambao tayari wameharibika na hawafai kwa matumizi.
Mimi ni mhanga wa hao Wafanyabiashara hasa wa Soko la Uyole maana ndiyo lipo karibu na kwangu, hivyo huduma muhimu nazipata pale.
Kuna wale Samaki Wakavu, mwanzo nilikuwa najua wale ndiyo salama kuliko Samaki wa Bichi kumbe nilikuwa najidanganya.
Kuna siku Mwanongwa wa watu nikajichanganya nikanunua Samaki aina ya Kambale ambaye amekaushwa kwa kutumia Moshi, nilivyofika nyumbani na kumuweka kwenye maji ya Moto nikaona wadudu aina ya funza wakitoka kwenye Samaki.
Kesho yake nikaenda sokoni na yule Samaki na kumuonesha muuzaji, alichonijibu ni kuwa yupo tayari kunibadilishia Samaki na siyo kurudisha fedha, nikaachana naye na kuondoka.
Baada ya muda nikaamua kufanya uchunguzi kangu kuhusu Wafanyabiashara wenye tabia kama hizo, nikampata kijana mmoja ambaye ameajiriwa kwenye duka la Samaki (Fresh food).
Huyo kijana alinisimulia jinsi ambavyo Wafanyabiashara hao wa Samaki wanavyofanya, anadai wale Samaki wabichi wakianza kuharibika baada ya kukaa muda mrefu kwenye majokofu wanaamua kuwakaanga kwenye mafuta na kuwauza.
Hivyo, wanafanya huku wakijua kabisa kwamba Samaki hao hawafai kwa matumizi ya binadamu, ila kwa kuogopa hasara wanaamua kuwauzia watu Samaki waliyoharibika.
Ukiachana na hao Samaki wa bichi, kuna hawa Samaki wa kukaushwa kwa Moshi, hawa ni vigumu sana kutambua kama wameharibika mpaka ukifanikiwa kuwaweka kwenye maji ya Moto ndiyo utaona wadudu wanavyotoka.
Wafanyabiashara wa Samaki hawa wakavu mara nyingi huwa wanachukua blashi na mafuta ya kupikia, kisha wanaanza kuwapaka Samaki hao ili waonekane wanahali nzuri lakini kumbe ni balaa.
Hivi kama kitu kimekudodea mpaka kimeharibika kuna haja gani ya kuendelea kukiuza na kupelekea kuziweka hatarini afya za watu? Si bora ukatupe tu.
Na ninyi ma bwana afya mliopo sokoni, hivi kazi yenu mnaijua kweli au ndiyo kutwa kuchukua rushwa na kushindwa kusimamia misingi ya kazi zenu.
Wafanyabiashara wa Soko la Soweto na Soko la Uyole hiyo tabia mnayoifanya ni sawa sawa na uchawi, hivi unawezaje kumlisha binadamu mwenzio kitu kilichooza na mkiambiwa mnakuwa wakali.
Serikali ifuatilieni watu wenu mliowapa dhamana ya kusimamia na kukagua maduka ya vyakula, wanashindwa kuzifanya kazi zao kwa weledi matokeo yake kutwa wanarudi na vifungashio nyumbani vimejaa rushwa za Samaki, kuku na vitu vingine vingi ili wawe kimya.
Tunakoelekea tutatoana ngeu kwa kweli maana hii sasa imezidi hata kama ni kutafuta pesa ila siyo kwa staili hii.
Mwanongwa nawakumbusha tu kuwa hii tabia siyo nzuri ipo siku mtaua binadamu wenzenu kwa kuwauzia chakula kilichooza.