KERO Baadhi ya Wafanyabiashara Soko la Soweto na Uyole (Mbeya) wanauza Samaki walioharibika kwa makusudi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kiufupi Mbeya yote imekaa kimagumashi magumashi kila kitu ni uhuni uhuni tu alafu wa kishamba..
 
Kwani ni lini Mtanzania akawa mwadilifu na mkweli?

Wanauza nyama zilizolala buchani

Wanauza mbegu fake

Wanauza Mchanga wanasema mbolea

Wanachanganya vumbi kweybidhaa ili.kuongeza uzito na upuuzi mwingine kama huo.

So na hao ni sehemu ndogo tuu ya uhuni so hakuna Cha kushangaa maana hata waliopewa jukumu la ulinzi kulinda Afya wanasubiria tamko.la Rais,twende hivyo hivyo.
 
Funza kama anatoka ndani ya Kambare poa tu,unamchanganya na Kambare unawala mbona ni protini za kutosha.Mbaya funza atoke kwenye kinyesi.
Labda samaki awe ananuka tu, ila kama hanuki nawala wote yeye na hao funza wake.
Sema ubaya tu ni kua huenda wale wapuuzi huenda wanapuliza madawa ili wasitoe harufu ambayo labda yana madhara, hiyo ndo shida.
 
Kiufupi Mbeya yote imekaa kimagumashi magumashi kila kitu ni uhuni uhuni tu alafu wa kishamba..
Hakuna sehemu isiyo na wafanyabiashara wahuni hii nchi.

Nenda Ilala, nenda karume, nenda kariakoo uone kila bidhaa inafanyiwa kanjanja labda hizi za viwandani.

Ila mbogamboga, hao samaki, matunda, nguo, viatu kote huko kuna kanjanja.
 
Kiufupi Mbeya yote imekaa kimagumashi magumashi kila kitu ni uhuni uhuni tu alafu wa kishamba..

Sehemu gani TZ hakuna magumashi? Nchi yote hii imeoza.
 
Hatari
 
Watu wameweka maslai mbele ndomana magonjwa kama saratani yamezidi kwenye jamii
 
Chukua hatua binafsi, mnyororo wa chakula hapa nchini hauna usimamizi madhubuti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…