DOKEZO Baadhi ya Wahudumu wa Treni ya SGR (Dar) wanalangua tiketi kisha wanaziuza kwa bei ya juu

DOKEZO Baadhi ya Wahudumu wa Treni ya SGR (Dar) wanalangua tiketi kisha wanaziuza kwa bei ya juu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Socialisim isha prove failure Dunia nzima ni Tanzania tuna force ujamaa, Hilo shirika kuanzia Mkurugenzi hadi mfagiaji hakuna alie commited hapo wanacho angalia ni wananufaika vipi wao.

Serikali inakomaa sana na ujamaa sijui kwa nini na usha pitwa na wakati.
Shida nchi hii wakiitwa watu wenye weledi kuendesha shirika utasikia nchi imeuzwa wakati ni ukweli usiopingika kila cha serikali watu wanajipigia tu hawana uchungu sababu mwisho wa mwezi wanalipwa tu. Shirika likiendeshwa na private operator ufanisi utakuwa juu kwa sababu anataka pesa zaidi ili alipe gharama za serikali na yeye apate faida kwa hili usimamizi na huduma zitakuwa bora. Ni lazima tufanye mchakato wa kupata operator wa SGR.
 
Siku kadhaa zilizopita mtoa mada fulani aliandika " Treni zinaondoka kwenye vituo behewa zikiwa tupu huku wakiambiwa zimeshajaa" na mwingine akasema "bites (vyakula) wanauziwa..

TRC ni suala la muda itakua kama mwendokasi . Itakufaa

Fukuza wafanyakazi wote wanaonyesha hali za wizi
no thats not a solution. solution ni ku wapa private sector waendeshe.
 
Ebhana hii ndo bongo, ukizubaa kidogo unapigwa huku umesimama- Tatizo hata walio juu nao wanapiga hii mentality inendelea kukua, kila mtu anawaza namna ya kuingia kwenye system apige

Hakuna Maadili kazini, Kuna Madili kazini - hii ndo TZ
 
no thats not a solution. solution ni ku wapa private sector waendeshe.
Solution nyingine NI mkurigenzi mtendaji Kadogosa kazidiwa KAZI hapati muda WA Ku concentrate
Abaki Tu kusimamia ujenzi WA Reli za Mwendo KAZI ambazo bado ziko under construction

Atafutwe Mkurigenzi mwingine WA kusimamia kitendo cha biashara ya uendeshaji SGR.Kazi Yake iwe hiyo Tu

Kwenye ujenzi kule NI pasua kichwa na Kadogosa kajitahidi Sana apokewe Hilo eneo kuwe na Ma wakurugenzi wawili WA kitengo cha ujenzi ,uhandisi na miundombinu Yake abaki Kadogosa na kitengo cha Biashara atafutwe mwingine
 
Kwanini mtu ana smart phone na anaenda kukata manually?

Kata online, hakuna ulanguzi, hakuna mtu kati
 
Ni kweli huduma inapatikana katika simu, computer online n.k,

Ila kila mara treni imejaa, na ukibahatisha inaonekana seat moja au mbili ndio zimebakia, ajabu ukipanda treni unalala seat wima kabisa hakuna watu. Ukiingia online kila behewa no Seat ila ukiwa ndani ya behewa zinatembea tupu. Kuna namna mahali iangaliwe na tupewe ufafanuzi
Hii hata mimi nimeshuhudia.
Kwenye mtandao, unaona behewa limebaki na siti mbili tu, unakata moja ukifikiri behewa limejaa, muda wa safari unashangaa behewa liko nusu!
Inawezekana app yao haiko sawa.
 
Mtanzania ni mwizi na mshenzi by nature
Hii nchi na raia wake wana laana ya kudumu
Hii project soon itakuwa failure , Yaani ni sawa na kujenga ghorofa kwenye msingi wa tope .
Msingi wa maendeleo ni mifumo thabiti ya uongozi na katiba inayobana ushenzi kama huu + taasisi imara za kusimamia hili .
 
Hili linatu cost sana ajira za kuangaliana usoni na sio weredi ni shida tupu
Shida ya ajira za upendeleo ndio hayo .Wanaajiriwa wasio na maadili kabisa

Kwenye mfumo WA kukata Tiketi WA TRC waweke sehemu ya jina kamili na MTU aje na kitambulisho wakati WA kupandia

Mbona mabasi Hilo mfumo wao umeweza

Hata ndege mbona wameweza

Latra huo mfumo wanao waupeleke TRC

LATRA pelekeni mfumo wenu T
 
Usichoelewa hapa ni kuwa hakuna abiria atakayeruhusiwa kuwa na ticket isiyo na namba yake ya NIDA,kitambulisho cha taifa,Leseni au barua ya serikali ya mtaa,kwahiyo hao walanguzi hawataweza kumuuzia mtu asiehusika na hiyo ticket...
Huenda hata wewe Bado hujaelewa mkuu ieleweke kuwa anaekuuzia hiyo ticket ni muhisika Moja Kwa Moja yaani mfanyakazi na sio mmoja huenda ni Dili la watu zaidi ya10! Sasa watashundwa vipi kukuingiza?

Umesahau majuzi wamekamatwa watu wakifanyia mitihani watu wengine hasa waheshimiwa kabisa? Sasa Hilo linawezekana vipi na hili lisiwezekane? Safari Bado ndefu sana kiongozi kuifikisha hii nchi
 
Waajiri Wahindi ndiyo wasimamie kila kitu. Hao Waswahili ni watu wa hovyo kabisa hawawezi kuwa na maadili na mwisho wataiua kabisa hiyo huduma
Mama alipo binafsisha bandari hawakumuelewa ila ni nchi tu yenyewe imeamua kulea huu ujinga, mbona inawezekana kuwalazimisha watanzania kuogopa rushwa na wizi halafu badae unakuwa ndio utaratibu wa maisha?
 
Tatizo linaanza kwenye jinsi ambavyo hao watumishi wa hiyo treni wanavyopatikana. Wengi ni ndugu wa viongozi au hata makada wa ccm. Ndiyo maana hakuna weledi na hawajali wanaona sawa tu wanayoyafanya. Hili tatizo lipo pia kwa Air hostess wa Air Tanzania ambao hawana umahiri wowote. Huduma zao ni duni below standard.

Ndiyo maana nashauri uendeshaji wapewe watu wengine kama Wahindi au hata Wakenya tu watanyooka hao wstumishi. Mtanzania hawezi kujisimamia kwa chochote
 
Hao washikwe na wachukuliwe hatua kali kabisa, nje ya sheria. Wawachiwe Kariakoo wapigiwe kelele za wizi, majambazi. Wananchi wachukuwe hatuwa za mitaani.
 
lakini na nyie wabongo muwe mnakata tiketi mapema mnapopanga safari zenu, mtu unajua una safari ijuma badala ukate tiketi jumanne unasubiri hadi alhamisi jioni au ijumaa ndio unaenda kupanda treni huku huna tiketi, unategemea nini hapi zaidi ya kulanguliwa
 
Hao washikwe na wachukuliwe hatua kali kabisa, nje ya sheria. Wawachiwe Kariakoo wapigiwe kelele za wizi, majambazi. Wananchi wachukuwe hatuwa za mitaani.
Haki za binadamu hawatakubali. Dawa ni kuipa menegement ya kigeni isimamie. Sisi hatuwezi kujuana kwingi. Google inasimamiwa na wahindi sisi tusione aibu. Tuwape wageni waisimamie hii biashara. Hata Emirates Ailines inaendeshwa na wazungu
 
Tatizo linaanza kwenye jinsi ambavyo hao watumishi wa hiyo treni wanavyopatikana. Wengi ni ndugu wa viongozi au hata makada wa ccm. Ndiyo maana hakuna weledi na hawajali wanaona sawa tu wanayoyafanya. Hili tatizo lipo pia kwa Air hostess wa Air Tanzania ambao hawana umahiri wowote. Huduma zao ni duni below standard.

Ndiyo maana nashauri uendeshaji wapewe watu wengine kama Wahindi au hata Wakenya tu watanyooka hao wstumishi. Mtanzania hawezi kujisimamia kwa chochote
Bila kuwajibisha kwa ukali kabisa hata ukamchukue mtanzania wawapi atakuwa mwizi ,kinacho leta hofu na woga kwenye wizi wa mali za umma ni kuwajibishana tuu! Bila kujali ni nani na ana undugu na nani, tukiliwez hilo hujuma na wizi vitakwisha kabisa ,ila kwa style hii ya kuleana leana kisa ukada na riport ya CAG ina ibua wizi halafu bunge lina utetea! Kamwe usitarajie muujiza wa uzalendo nchi hii kwa mfumo huu.
 
Waajiri Wahindi ndiyo wasimamie kila kitu. Hao Waswahili ni watu wa hovyo kabisa hawawezi kuwa na maadili na mwisho wataiua kabisa hiyo huduma
Wahindi walishapewa Hilo shirika la reli wakashidwa kuliendesha
Kwao India kwenyewe shirika lao la Reli.choka mbaya
 
Bila kuwajibisha kwa ukali kabisa hata ukamchukue mtanzania wawapi atakuwa mwizi ,kinacho leta hofu na woga kwenye wizi wa mali za umma ni kuwajibishana tuu! Bila kujali ni nani na ana undugu na nani, tukiliwez hilo hujuma na wizi vitakwisha kabisa ,ila kwa style hii ya kuleana leana kisa ukada na riport ya CAG ina ibua wizi halafu bunge lina utetea! Kamwe usitarajie muujiza wa uzalendo nchi hii kwa mfumo huu.
Kwa sababu hatuwezi kuwajibisha tuweke wageni watusimamie. Hawatatuonea aibu. Na tusione unyinge kuweka wageni. Hata mashika makubwa tu ya Ulaya, Gulf na USA yanaendeshwa na wageni
 
Mimi nitaipanda baada ya watu kuichoka! Kwa siku za mwanzoni kila mtu anataka kupanda SGR kwa hiyo lazima kutakuwa na idadi kubwa ya watu wanaotaka kutumia usafiri huo!
 
Back
Top Bottom