DOKEZO Baadhi ya Wahudumu wa Treni ya SGR (Dar) wanalangua tiketi kisha wanaziuza kwa bei ya juu

DOKEZO Baadhi ya Wahudumu wa Treni ya SGR (Dar) wanalangua tiketi kisha wanaziuza kwa bei ya juu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Wahindi walishapewa Hilo shirika la reli wakashidwa kuliendesha
Kwao India kwenyewe shirika lao la Reli.choka mbaya
Hao hao Wahindi ndiyo wanaendesha Google, Microsoft, World Bank n.k. inategemea na wahindi. Lakinj kwenye management ni the best. Kama hakuna Wahindi wawape hata Wachina. Ila wamatumbi lazima waliue hilo shirika
 
Kwenye IT wako vizuri kwenye Reli hamna kitu

Kwao Reli Yaowahindi India mahututi Hizo management skills za Reli wameokota wapi wakati Reli Yao Tu marehemu
 
Ni kweli huduma inapatikana katika simu, computer online n.k,

Ila kila mara treni imejaa, na ukibahatisha inaonekana seat moja au mbili ndio zimebakia, ajabu ukipanda treni unalala seat wima kabisa hakuna watu. Ukiingia online kila behewa no Seat ila ukiwa ndani ya behewa zinatembea tupu. Kuna namna mahali iangaliwe na tupewe ufafanuzi
Dadek! Washafanya yao.
Na hapo utakuta mbinu nyingine kama buku hivi zipo kwenye mafaili. Ni bandika, bandua.
Hiyo ndio Tanganyika halisi
 
Waajiri Wahindi ndiyo wasimamie kila kitu. Hao Waswahili ni watu wa hovyo kabisa hawawezi kuwa na maadili na mwisho wataiua kabisa hiyo huduma
Wala pilipili waliwahi pewa reli ya kati, hali ndio ikawa mbaya zaidi.
Tanganyika ni special mzee!
Wakianzisha Olympic ya Ujanja Ujanja tungeweza kuambulia hata dhahabu.
 
Ndugu abiria,
Shirika la Reli Tanzania linapenda kukutaarifu ya kwamba kuanzia tarehe 10/08/2024 unapokata tiketi,hakikisha unakitambulisho kimoja wapo kati ya NIDA, kiambulisho cha Kura, bima ya Afya, leseni ya Udereva, hati ya Kusafiria,au kitambulisho cha kazi. Kama hauna basi uje na barua ya Serikali za mtaa yenye picha yako iliyogongwa muhuri. Kwa mtoto anayekatiwa nusu tiketi kuanzia miaka 4 hadi 12 tafadhali fika na nakala moja wapo kati ya cheti cha Kuzaliwa, bima ya Afya, hati ya Kusafiria au kitambulisho cha Shule.Na siku ya kusafiri hakikisha unakuja na kitambulisho chenye jina sahihi ambalo lipo katika tiketi yako.
Kwa mawasiliano zaidi piga simu ya Huduma kwa Wateja namba 0800110042

Labda hii ya kukagua jina Vs Vitambulisho itasaidia kudeal na changamoto hiyo .
Hii inafanyika Duniani kote, sijui Kwa Nini walichelewa.
 
Watanzania badilikeni. Nunua tiketi yako mtandaoni kabla ya kwenda station. Mambo ya kwenda station huna tiketi unabahatisha ndio mwisho wa siku mnalialia.
Weekend hizo treni zinajaa kweli. Sasa mnaleta mazoea ya hovyo huna tiketi unaenda kichwa kichwa station kubahatisha. Anatokea mtu na tiketi yake anataka akuuzie kwa bei yake unaanza kulialia. Tuache mazoea ya Magufuli bus terminal, kata tiketi mapema uone kama utakazimishwa kuuzowa tiketi mara tatu ya bei.
 
Umeelewa alichoandika lakini?

Hata ukifika pale na cheti Cha ubatizo utaambiwa tren imekaa hivyo jiongeze Kuna abiria kaghaili kusafiri ndo unapigwa Cha juu

Hivyo vitambulisho havitasaidia lolote
Kama ni hivyo inabidi uzuiwe kuondoka hadi umtaje aliyekuuzia tiketi ili huo mchezo ubainike na wahusika uwataje wachukuliwe hatua.

Tukiendelea kununua hizo tiketi za magendo ndivyo tutakavyoendelea kuimarisha huo mtindo mchafu.

Nashauri mtego uwekwe ili hao watumishi wakamatwe na kupewa kesi ya Uhujumu uchumi.
 
Nakubaliana nawewe lkn je nani atamfunga paka kengele Ili Hali waliambiwa hadharani wale kulingana na urefu wa kamba zao?
 
Ni siku chache zimepita tangu Huduma za Usafi wa Treni ya SGR uanze na juzi tulishuhudia Rais Samia Suluhu Hassan akiongoza zoezi la uzinduzi.

Usafiri huo umekuwa kimbilio kwa Watu wengi, sababu kuu ikiwa ni muda ni kutokana na kutumia muda mfupi kufika maeneo husika.

Lakini nimefika pale mara kadhaa hasa Wikiendi kuna jambo nimeligundua, kuna mchezo mchafu unafanywa na baadhi ya Watendaji hasa wanaokata tiketi.

Wahusika hao wanatumia Watu wao wa karibu kununua tiketi wanapohisi kuna abiria wengi zaidi hasa Wikiendi, baada ya kufanya, hivyo Wanunuzi wa hizo tiketi wanajifanya kughairi safari, kinachoenda kufanyika zile tiketi zinauzwa kwa bei ya juu zaidi, mfano tiketi ya Dar-Moro ya 13,000 inauzwa mpaka 30,000.

Baadhi ya wahudumu wa ndani wakishakata tiketi kupitia jamaa zao zile tiketi wanawapatia wahudumu wa nje ya madirisha ambao jukumu lao ni kutoa maelekezo na usaidizi kwa abiria namna ya kupata tiketi.

Wakishapewa hizo tiketi wanafuata abiria mmojammoja aliyekosa wanakwambia ujiongeze wakupe tiketi, wanakuandaa kuna Mtu kaghairi kusafiri, ukishindwa kufikia kiwango wanachokitaka wanakutosa wanaenda kwa mwingine.

Wale wahudumu ambao wanafanikisha mchezo huo wakiona uwezekano wa kushutukiwa wanakwambia kaa subiri mpaka Treni ikikaribia kuondoka, ikija wanakupa tiketi unawapa chao na kupanda.
Huu mchezo mchafu uenda baadhi hawajaubaini maana unafanyika kwa siri na Watu wanapiga hela hasa kipindi cha wikendi, ni mamlaka nifuatilie suala hilo haraka ili kuondoa mazingira ya upigaji.

Bila mamlaka kuchukua hatua mapema mradi huu utakuja kuwatajirisha baadhi ya Watu kupitia njia na taratibu ambazo hazina uhalali.

Kama kuna mabehewa ambayo tayari yameshawasili nchini ni muhimu ukafanyika mchakato wa haraka yakaongezwa hasa siku za weekend kwa lengo la kuondoa mazingira ya upigaji.

Lakini pia ikiwezekana mchakato wa kupata wawekezaji uharakishwe ili waweze kuingiza mabehewa zaidi kwa kuwa kwa mwenendo huu uenda kuna Watu wachache wananufaika na hali hii.

Pia soma:
~ Ukitaka kukata tiketi SGR unaambiwa treni imejaa, muda wa kuondoka treni inakuwa wazi
~ Online booking SGR haifanyi kazi, nifanyaje?
bongo kila kitu dili.
 
Kama ni hivyo inabidi uzuiwe kuondoka hadi umtaje aliyekuuzia tiketi ili huo mchezo ubainike na wahusika uwataje wachukuliwe hatua.

Tukiendelea kununua hizo tiketi za magendo ndivyo tutakavyoendelea kuimarisha huo mtindo mchafu.

Nashauri mtego uwekwe ili hao watumishi wakamatwe na kupewa kesi ya Uhujumu uchumi.
Au kama majina ya kwenye ticket yanatofautiana na majina ya kwenye kitambulisho chako hakuna kusafiri, na inatakiwa ihesabike kama vile umeiba ticket ya mtu mwingine!!
 
Hawana uwezo wa kununua tiketi zote 4,000 kwa siku 2 au. 3 mfululizo. Ticket unaaweza. Kuilipia kwa Tigo pesa hapo hapo ulipo, siku ukienda ni kupanda tu..
 
Au kama majina ya kwenye ticket yanatofautiana na majina ya kwenye kitambulisho chako hakuna kusafiri, na inatakiwa ihesabike kama vile umeiba ticket ya mtu mwingine!!
Nakubaliana na hili maana kujisajili kwenye mfimo wa e ticket huwa tunaweka namba ya NIDA ambapo lazima majima yako yaonekane, so kitambulisho inabidi kiwe lazima.

Kama tunafanya check in mapema, hili linawezekana kufanyika
 
Kwa sisi flight catcher shii kawaida sana dunia nzima. Akili mukichwa mzee.

Hata mabasi, ndege, uwanja wa taifa kuangalia match nk hukosi madalali wao hawana nia ya kusafiri lakini hufanya hayo mambo.

So just get used to it. Ile sio daladala panga safari yako mapema otherwise kama una emergency kubali upigwe tu. Dunia tambara bovu no chance for the innocents.
 
Kama waliweza kuharibu mfumo wa kulipia kwa kadi wa brt na hawakufanywa chochote kwanini wasiharibu mfumo wa sgr
 
Ndugu abiria,
Shirika la Reli Tanzania linapenda kukutaarifu ya kwamba kuanzia tarehe 10/08/2024 unapokata tiketi,hakikisha unakitambulisho kimoja wapo kati ya NIDA, kiambulisho cha Kura, bima ya Afya, leseni ya Udereva, hati ya Kusafiria,au kitambulisho cha kazi. Kama hauna basi uje na barua ya Serikali za mtaa yenye picha yako iliyogongwa muhuri. Kwa mtoto anayekatiwa nusu tiketi kuanzia miaka 4 hadi 12 tafadhali fika na nakala moja wapo kati ya cheti cha Kuzaliwa, bima ya Afya, hati ya Kusafiria au kitambulisho cha Shule.Na siku ya kusafiri hakikisha unakuja na kitambulisho chenye jina sahihi ambalo lipo katika tiketi yako.
Kwa mawasiliano zaidi piga simu ya Huduma kwa Wateja namba 0800110042

Labda hii ya kukagua jina Vs Vitambulisho itasaidia kudeal na changamoto hiyo .
Mtoto anasafiri Kwa dhamana ya mzazi ambae tayari ana kitambukisho, sasa mtoto mdogo wa miaka 4 mpaka 6 hata bila cheti anajulikana tu ni mtoto hivyo nusu tiketi inamhusu, angalau wale wa miaka 10 au 12 hapo forgery ya umri inaweza ikawepo maana hata wa miaka 14 anaweza kujifanya ana miaka 12
 
Back
Top Bottom