Baadhi ya wanajeshi jiondoeni kwenye siasa msije kupata fedheha!

Huyu ndiye kanali lubinga? Miaka mingi sana alikua CCM wazi wazi tokea akiwa active soldier. Acha waendekeze siasa jeshini siku wakipinduana wasije kulaumu mtu. Maana naona wanalionjesha jeshi ladha ya siasa, sasa siku wakitaka kila kitu itakuaje? Na hivi upinzani wanauua, wasishangae JWTZ ndio ikawa exit strategy ya CCM!!
 
JWTZ wa leo wangejua tu ilikuwaje tulianzisha JWTZ mwaka 1964 leo hii CCM wasingekuwa madarakani kwa Wizi na Ufisadi wanaoufanya dhidi ya Watanzania masikini.
 
JWTZ linapaswa kujitafakari pale majenerali wake wanapojiunga na CCM! Vyama vya upinzani siyo magaidi!
 
Siku Moja ndani ya JWTZ kutakuwa na wafuasi wa Chadema au wasiyoipenda ccm. Hapo timbwili litaanzia kambini. Timu ccm dhidi ya timu chadema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…