Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Kutokana na hali ya ukame inayoendelea nchini na hivyo kusababisha upungufu wa chakula. Kwenye baadhi ya maeneo baadhi ya wanaume wamekimbia nyumba zao na kuwaacha wanawake na watoto pekee katika familia.
Baadhi ya wanawake Wamekuwa wakijitaftia ridhiki kwa kwa kutembea umbali mrefu kuelekea maeneo ya mjini kwenda kuuza kuni, mkaa au kuomba chakula
Wanawake hao jamii ya kimaasai wamesema huondoka majumbani kwao alfajiri ya saa kumi na hutembea kwa miguu hadi saa tatu au nne za asubuhi hadi kufikia kata za mjini ambapo hupeleka kuuza mkaa na kuni na hufika nyumbani usiku wa saa tatu hadi saa nne.
Baadhi ya wanawake hao kutoka kata za mirongo na Mbuyuni mkoani Arusha wamesema kuwa wanapitia changamoto nyingi za kimaisha kutokana na Kuwa wababa wamekimbia familia zao na hivyo hupambana wenyewe kwa kila kitu.
Pia baadhi ya wanawake wa kimaasai kutoka vijiji vya olkomoro wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro wamesema kutokana na ukame na Kukosekana kwa Mavuno familia zimekuwa zikishindia uji na hivyo wababa wa familia kukimbia familia zao. Na hivyo watoto nao kukosa afya iliyo bora kutokana na kukosekana kwa mlo kamili