Baadhi ya wanawake wana roho mbaya sana

Baadhi ya wanawake wana roho mbaya sana

Selwa

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2010
Posts
583
Reaction score
590
Juzi kati mke wangu alikuwa anapitia msongo wa mawazo sana, anasoma ukubwani kwahiyo kubalance biashara na kisomo kinamramba, kama wiki mbili anadeal na kesi ya wizi dukani kwake na mitihani. Wizi ilikuwa kiasi kidogo ila mkinga kapambana mwizi kapatikana kisha karudi darasani. me nilimuacha apambane na huyo mwizi mwenyewe ili nione kama ataiacha au ataihandle yani nimefurahi kuona kaweza kusimamia mpaka mwizi kapatikana kawekwa ndani kesi imeanza amelipwa hela yake afu kaingia kwenye mitihani.

Kama surprise nikampangie aende zanzibar baada ya mitihani, siku ikafika wakaenda yeye mdogo wake na watoto wakatoka apo nikaenda kuwakuta serengeti tukawa pamoja tukarudi wote. Yani alifurahi kupindukia nikamuliza mama vipi mbona kama huamini . Akaniambia alivokuwa anapambana na kesi marafiki zake wote walimwambia aniache, yani nina kesi nina mitihani na mme yupo tu akufanyii lolote lazima ana demu nje doh niliumia sana
. Yani wale marafiki zake walikuwa wanafurahi kumwona anateseka wakidhani namfanyia maksudi kumuumiza walikuwa hadi wanakuja sehemu napofanya kazi wananipiga picha kisa tu nimetaka mwanamke ajifunze kuwa mgumu katika biashara. Wakamjaza chungu ya maneno sasa kumpeleka hizo sehemu 2 tu wanaaanza ooh anajisafisha. Hivi kwanini wanawake hawapendani?
 
Ulimkosea sana. Mwanamke hapimwi kwenye mazingira ya namna hiyo. What if angeharibu kwenye masomo yake kwa sababu ya kutoona msaada ungekuja kumsaidia kurekebisha masomo yake wewe?

Wakati wa matatizo ndio wakati wa msaada wako kuonekana ukizingatia yeye ni mkeo. Sasa unasubiria uje um suprise na safari za zanzibar sijui serengeti inamsaidia nini kwenye mambo aliyoyapitia.
 
Napingana na wewe hapo kwenye kusema wanawake wana Roho mbaya, hakuna kitu kama hicho.

Kama ilivyokua Kwa wanaume kuwepo katili na wema, Hali kadhalika wanawake wema na wenye Roho mbaya wapo.

Suala la Roho mbaya Halina jinsia,inategemea mazingira.
 
Nyie nao mmeruhusu mahusiano yenu kujulikana kwa hao marafiki yani mnajianika km bango la matangazo lazima kila mtu asemw anachojisikia, mie kwenye circle yangu sijamuona wa kuniletea hizo shobo hadi amtumie picha Mr 😅😅 kwanza itajulikana walianzaje mpk kutumiana picha zangu nk
 
Hawa viumbe asilimia fulani ni hatari sana sanaaa
Tena maneno ndio wanayatumia haswaaa

Kubwa la vyote ni wivu, ungekuwa hauna mbele wala nyuma wasingemuambia hayo waliyosema.

Wanakutamani, sasa mwambie awatambue kuwa wanataka atoke kwenye ndoa wao wafurahie kakukosa.

Wao lazima hawana furaha unayompatia mkeo, hata kama wameolewa.

WIVU kitu kibaya sana, ni maombi mtu ugundue watesi wako mapema hata wakiwa kama malaika kitabia kwako mwanamke na mwanaume pia. Kuna wanaume wana wivu sana pia
 
Ulipaswa kumuonyesha mkeo umuhimu wako kwa kusimama na kutatua changamoto aliyo ipata.
Mwanamke kiasili ni kiumbe dhaifu sana, na kiumbe hiki maranyingi hudondoka wakati wa changamoto kama hizo na wanakuaga out off mind.
Mkuu, niamini nakwambia wanawake wengi huliwa hata na wanaume wasio wapenda hasa katika nyakati kama hizo.
Next time don't do that mazee...
 
Yah, ni kweli. Ila hivi vitoyo vinawapa stress sana wakinamama ukimpotezea kidogo tu anahisi ushatekwa navyo.

Nashukuru Mungu Sina upepo navyo hata kidogo. Kwanza vinavyoandika text vifupisho na maongezi nao najikuta kabisa hapa sio fungu langu.

Hivyo vitu vidogovidogo vinakata mzuka wote. Ujue Hadi kufikia mambo makubwa lazima baadhi ya vitu viwaweke pamoja. Bora wazee wenzetu hata masihara Yao yame graduate.

Au ni uzee unanisumbua?
 
Hahah, uzee unakunyemelea kaka. Hahah
 
Hahah, uzee unakunyemelea kaka. Hahah

Tayari nipo nao kiongozi, nnaishi nao japo kuna mtu anabisha sana kwamba mie sio Babu.

Kuhusu hili la vi Gen Z haihusiani na suala la uzee, tokea zamani nilikua nna uhakika kesi za miaka 30 haziwezi kunipata, vinginevyo nisingiziwe tu. Sina kabisa upepo na vibinti...
 
Hata sisi wanaume hatupendani,na wanawake pia hawapendani, adui wa mwanaume ni mwanaume na mwanamke ila adui wa mwanamke ni mwanamke .
Uadui na kutopendana inafungwa katika udhaifu wa mwanadamu wa ubinafsi, kama kusingekuwa na ubinafsi vyote hivyo vingekuwa na nafasi ndogo sana kwenye maisha ya mwanadamu.
 
mwanamke ni kiumbe kingine hii ninavyoamini siku zote, hujiona wao wana akili nyingi sana, hujiona wao ndio wanastahili kila zuri, na kwa kuwa wao ni version ya pili ya mwanadamu, kuna errors nyingi sana zimejitokeza kwao, ni kama walipewa akili kubwa kuliko uwezo wao wa kuhimili hiyo software, kwanza adui wa mwanamke ni mwanamke mwenziwe, rejea kesi nyingi mtaani zinahuhisha wanawake, iwe mahusiano ama madaraka utakuta chain inaanzia kwa wanawake, kuna imani fulani ziliamua hawa kuwaacha nyuma kwanza kwenye kila mipango ili baadae watakapo kuja kustuka waweze kubalance mambo lakini wapi, suala la mwanamke kuwa ni kiumbe advanced linapokuja uala la kuharibu hilo ni la miaka na miaka. siwasemi kwa ubaya, lakini natambua Mwanamke ni wa kuishi nae kwa hesabu sana, awe na elimu ama asiwe na elimu, wote ni wale wale tu, wanaweza kuishi kwa hisia kwenye mazingira halisi na usijue, wanaweza kusoma mawazo yako yaani wana uwezo wa kuingia ndani ya kichwa chako wakachakua chakua wakachanganya mafile kadri watakavyo, na akakaa pale anasubiri anguko lako huku yeye akiwa ndio mshauri wako Mkuu. siku zote naamini hawa wamekuja hapa kutu challenge, wapo kwa mission maalum, so unapochagua Mwanamke ni kama unachagua changamoto ambayo unaamini unaweza kukabiliana nayo, hatuwawezi kwa mambo yaliyo sirini, labda mambo ambayo ni dhahiri shahiri hapo kidogo tunaweza kumzungumzia huyu kiumbe, maana kila walalapo wenzetu wana upgrade soft huku sisi tukiwa ndio watendaji wakubwa. rejea tunavyopambana kwa ajili yao. kuna mengi sana lakini kubwa na la muhimu kujua ni kwamba mwanamke ni zaidi ya Uke. kuna mission kubwa sana ya uwepo wa hawa viumbe. sio wa kuwachukulia poa. na ili ujijue umepevuka kiasi gani, una ujasiri kiasi gani, uvumilivu na akili, basi tafta mwanamke upite nae njia moja
 
Back
Top Bottom