Baadhi ya watu wanajiuliza kwanini ''bwana yule'' hapati tena siri za Ikulu?

Baadhi ya watu wanajiuliza kwanini ''bwana yule'' hapati tena siri za Ikulu?

Turudie mara ngapi? Ni Dhaifu!!!!!!!, tumerudi enzi za Msioga za Mr. Dhaifu!
Afadhali sasa, hali ile ilitisha kila agizo lilikua ni sheria na ndiyo Katiba. Tulikua tunaelekea kubaya sana. Leo ukienda posta hakuna utaratibu vibanda vimetapakaa kila mahali, na kwa sabau ya uholela, ilidhaniwa ndiyo utaratibu sahihi wa kuendesha nchi, kiuhalisia tulikosa ustaarab, na nafikiri itatumika nguvu kubwa kuweza kuwashawishi wamachinga ili waelewe kuwa hawakua sahihi, kila watakachoambiwa wataona wanaonewa, kumbe ni utaratibu mbovu tu. So kila awam na mambo yake ambayo yanakera.
 
Mimi ni kijana nimesoma na kulingana na ugumu wa ajila nikaona fursa ipo kwenye ujasiriamali nikajiajili na kuajili vijana wenzangu pia ili kusogeza Maisha na kujipatia Ugali wa kila siku. Maamuzi yangu ya kuamua kusimama na Diamond PlatnumZ haikua kwaajili ya vita bali Utanzania.

Kijana amusha legea huko twitter.
Wamemfanyiaaa mbayaaaa
 
Hembu soma hiyoo hicho ndio namaanisha maana wewe umeisha kula na huna.usingizi. utanifanya nichoke maana huelewi ninacjo maanisha kuyumbishwa kwa serikali na kundi la wtu wa mitandaoni kwa baadhi ya mambo ambayo ni ya kipuuzi.
Upuuzi kama wa kumkamata mtekaji ole sabaya? 😅😅😅
 
Tatizo kuna mengine ni husuda na chuki lakini.hayana maana nimekupa swala mpambazi mpaka kaitwa tbs !!

Sijui unaelewaa nacho kimaanisha au hutak tu kuelewa ili tubishane
Sasa kwa akili yako unadhani huyo dogo kaitwa tbs kwa agizo la raisi?
 
Sasa mkuu aliyemkamata jamaa ni SSH au TBS wazee wa kukurupuka kama Dr. mwaka alivyokurupuka akaenda mfungia Dr. mwaka kisa mangekimambi ana bifu zake na diamond.
Kigogo ana movement zake flani nyingine hata mimi sizikubali, ila mleta mada siyo kweli kwamba SSH nafuata kigogo anachosema.
Angekuwa anafuata basi Biswalo asingekuwa judge, Manji asingekuwa kakamatwa na takukuru, Happy asingekuwa mbunhe, Dotto asingekuwa serikalini, tungekuwa na baraza jipya la mawaziri
Una kichwa kigumuna umeanza kuelewa TBS waliomkamata ni kwa sababu samia anawapa priority hio timu sana kiasi kwamba kumuita mpambazi haikuwa na maana yoyote .

Na alie sababisha hayo yote ni kigogo 2014 kwa sababu mpambazi alikua ana mtetea diamond platnumz kama hujui na uelewe kwamba unabisha lakini hujui kinacho endelea toka.juzi.
 
Dah....Dogo tuliza makalio...Kule bandari washapiga makinikia [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji2960]
 
Acheni mama achape kazi na akimaliza muda wake atatuletea katiba mpya ili tusije tukarejea kwenye utawala wa kishetani katika nchi hii.

Uhalifu,wizi, ubakaji wa wazi wa akina Sabaya , Utesaji ,unyanganyi ulijaa lakini ulifichwa na vyombo vya habari havikuruhusiwa kuanika wazi.
Miradi mapaka ya vyoo vya mashimo ilikua inarushwa hewani kwa gharama ya mamilioni ya walipa kodi.
Acheni Ukabiwa wenu mlipanga kuigawa nchi na mmeshindwa.

Mungu alisikia kilio cha mayatima waliobaki na wajane waliokua wamesababishiwa na watu katili kama nyie msiojali utu na uumbaji wa mwanadamu.
Watu walikua wanajifanya miungu watu na kupora Mali za watu.
Hivi unafikiri utajiri wa wafanyabiashara unapatikaba kirahisi kama huo wa kwenu wa miaka mitano mnakua mabilioneo kupitia ofisi za umma na madaraka ya kukwapua Mali za watu!!

Acheni mama afanye kazi yake. Au mnataka mturudishe enzi zile Kikwete amejenga mabarabara Vyuo , Nyumba za wanajeshi nchi nzima, akanunua mandege ya jeshi ya kisisa, vifaru n.k pamoja na hujuma za Kagame na timu yake inayojifanya imejirejesha kwa mgongo wa awamu ya tano lakini JK alivumilia kutukanwa mana anajua ni wajibu wake kuleta maendeleo sio hisani mana ni pesa za umma.

Mama amepewa hiyo nafasi na Mwanyezi Mungu mwenyewe ili awatendee haki watanzania.
Binadamu hatukuzaliwa na Madaraja wala mandege hayo ni mambo ya Mabeberu waliyaleta hivyo hatuhitaji MTU anayetumia mtutu wa bunduki kutuletea vitu vya wakoloni na mabeberu waliovianzisha. Treni ,mandege ni vitu vya huko ulaya kwa ngozi nyeupe tutafileta kwa hekima na upendo kwa watu wetu na sio kuuana kwa sababu ya madaraja.
Kodi zitalipwa kwa haki. Na watakaojaribu kutikisa kiberiti kwa kutuletea habari za mwendazake tutadili naye kweli kweli.

Kigogo ataendelea kuikosoa serikali mana ndivyo alivyoamua na hatutapoteza muda kumzuia wakati kuna mengi anayoyasema ni ya kweli na hakuanza kuyasema Leo na hayakuanza kufanywa leo.

Wa awamu ya tano amepita na sasa ni awamu nyingine bora zaidi.

Hatuwezi kubakia na simu za mezani wakati ni awamu ya smartphone. Kuendelea kusifia simu ya mezani ni ujuha.

Mama ameanza vizuri sana na anaipeleka nchi pazuri.
Huwezi kupuuza Covid 19 wakati kuna watu wana ndugu zao huko nje na wanabiashara huko Nje . Kuna watu wanaenda kuhiji na wameshaambiwa hawataruhusiwa kwenda. Ulitaka akomalie mambo yatakayowaathiri watu. Mitandao ni sauti ya watu wenye akili kubwa waliokosa fursa ya kukalia viti vilivyotolewa kindugu ,kikabila na kiitikadi. Ulitaka wasemee wapi zaidi ya kwenye mitandao.
Kwa ni mama apuuze mitandao wakati mitandao anaiona ina mijadala mipana na inafichua maovu kwa ushahidi wa wazi.

Mama ataendelea kuwapiga chini wale wasioendana na kauli mbiu yake bila kumwogopa MTU.
Nguvu yenu ikikua kwa MTU na sasa inaondolewa na MTU hivyo kuwani wapole tu. Waliolia sasa wanacheka na waliocheka kwa dhulma sasa wanalia kwa haki.

Hatutaruhusu watu wa aina ya Sabaya kukalia ofisi za umma.
Mama ameonyesha njia na Mungu atamlinda mana ameamua kusimama kwenye haki.

Uchaguzi wa marudio umefanyika kule Kigoma hatukusikia MTU akikatwa mapanga . Aliyeshinda akatangazwa kwa haki. Hakuna aliyenyanganywa Fomu wala kutekwa. Sasa kwa nini tudimpende Malkia wetu wa Afrika Mama Samia.

Mama Samia tunampenda sana. Na tunasubiri awamu yake ikikaribia kuisha tufanye maandamano makubwa ili katiba ibadilishwe atawale maisha kama Malkia wa Uingereza. Hatutaki Utawala wa kihuni tena wenye Magenge ya wahalifu na watesaji.
Chaguzi zilikua kama vita ,mtu anaenda kuchukua fomu Mkurugenzi anafunga ofisi anakimbia . Akibahatika kupata fomu wanakuja wahuni wanaotumia ofisi ,na mishahara ya umma wanawapora wagombea.
Hayo ndiyo maendeleo kweli au ni uhuni?

Huduma bora zipo na zitaendelea kuwepo na wale wanaozurotesha tunajua ni wale waliokua wamepewa kwa upendeleo na kikabila ambao wapo kila mahali nchi nzima na ndio wanaolalamika badala ya kuchapa kazi walidhani wamebinafsishiwa hii nchi kumbe kila kitu kiko mikononi mwa Mungu.

Mama Samia Hoyeeeeee!!!!
Kazi inaendelea kwa hekima na maarifa makubwa kabisa.

Waliobweteka kwa kumtegemea binadamu awakingie kifua kwa kuumiza wenzao sasa basi.
 
Yatima baba yako na mama yako ! Huenda wewe ni yatima au ulikosa mirathi mbona unahasira hivyo.
Hahahahhahahaha! Nan anataka mamirathi dogo? Faiti upate zako ...mpk leo mnalia lia tu wanaume wazima .shame on u!..
 
Una kichwa kigumuna umeanza kuelewa TBS waliomkamata ni kwa sababu samia anawapa priority hio timu sana kiasi kwamba kumuita mpambazi haikuwa na maana yoyote .

Na alie sababisha hayo yote ni kigogo 2014 kwa sababu mpambazi alikua ana mtetea diamond platnumz kama hujui na uelewe kwamba unabisha lakini hujui kinacho endelea toka.juzi.
Huyo muuza sabuni ni mpumbavu. Diamond hawezi kurisk biashara yake kwasababu ya mtu mwingine na ndio maana anajipendekeza kwa kila mwenye madaraka na pesa.

Haya sasa huyo muuza sabuni yeye kaumiza biashara yake kwa kujipendekeza kwa mtu ambaye hata hamjui.
 
Huyo muuza sabuni ni mpumbavu. Diamond hawezi kurisk biashara yake kwasababu ya mtu mwingine na ndio maana anajipendekeza kwa kila mwenye madaraka na pesa.

Haya sasa huyo muuza sabuni yeye kaumiza biashara yake kwa kujipendekeza kwa mtu ambaye hata hamjui.
Yule Champ Soap kunani tena
 
Nimeona sehemu nyingi baadhi ya watu wakijadili kuhusu ''bwana yule'' huku wengine wakimbeza lakini wengine wakiuliza kimetokea nini kwa sasa ''bwana yule'' hapati tena siri za Ikulu.

Kwa wasiojua vizuri wameenda mbali zaidi na kudai eti kwa sasa siri za Ikulu zimethibitiwa na uongozi mpya!

Napenda niwasaidie kwa kuwaambia kuwa hakuna siri za Ikulu zilizothibitiwa ila wale waliokuwa wanatoa siri za Ikulu na kuzipeleka kwa ''bwana yule'' kwa sasa ndio hawa ambao wako madarakani. Kwa maana nyingine, kwa sasa ndio walioshika Ikulu/utawala moja kwa moja. Yaani sio tena watoa ushauri bali kwa sasa ni wabunifu na wasimamia utekelezaji.

Biashara yao na ''bwana yule'' ya kumpa siri za Ikulu iliisha siku ambayo Rais Samia aliapishwa kuwa Rais wa Tanzania!

Haishangazi kuona kwa sasa ''bwana yule'' anawashambulia sana baadhi ya wale waliokuwa wanampa siri za Ikulu baada ya kugundua hawataki tena mahusiano naye. Yaani kwa sasa wamemalizana naye!

Nasikia kwa sasa wale wale waliokuwa wanampatia siri za Ikulu wana mpango wa ''kumnyamazisha'' ili huko mbeleni asije akatumia umaarufu waliomuwezesha wao wenyewe kuichafua serikali yao. Kibaya zaidi, wanamjua vizuri kwa maana kuwa, wanazijua nguvu zake na udhaifu wake(strengh and weakness) kwa sababu ndio walimuwezesha kupata umaarufu kwenye mitandao ya kijamii. Hata kupata kitambulisho cha ''blue tick'' ilikuwa ni jitihada za baadhi ya wale waliokuwa wanampatia siri za Ikulu.

Baada ya kukosa ushirikiano kwa sasa ''bwana yule'' anafanya jitihada za kuwa karibu na wenyeCHADEMA ili apate uungwaji mkono kwenye mitandao! Kwa wanaofahamu historia ya ''bwana yule'' watajua kuwa huko nyuma hakuwahi kuipenda/kuishabikia CHADEMA hasa hakumpenda Mwenyekiti Mbowe na aliwahi kumshambulia sana akidai mwizi wa pesa za chama.

Huko mwanzo, ''bwana yule'' alikuwa ni mwanaCCM lakini baadaye akawa ''mwanaACT-Wazalendo'' kabla ya ujio wa Maalim Seif na kundi lake! Wakongwe wa siasa nchini wanajua kuwa ACT-Wazalendo ni ''stepping stone'' kwa wanaCCM! Kwa maana nyingine, ACT-Wazalendo ni kama fimbo ya kuchapiana wanaCCM kwa wanaCCM!

Hasira za ''kutoswa'' zinamfanya aanze ''revenge'' kwa waliomtosa kwa kutumia ''platform'' za CHADEMA.

''bwana yule'' anajua bila kupata sapoti ya wanaCHADEMA hawezi kuendelea kuwa ''relevency'' kisiasa katika dunia ya mitandao kwa sababu CHADEMA ni kundi pekee la kisiasa nchini ambalo hajapoteza uungwaji mkono.

Hoja iliyopo kwa sasa ni kujua kama ''kinyago'' walichokichonga walioko madarakani kwa sasa kitawatisha au watakiangamiza kabla hakijaanza kuleta madhara!
Na watu wengi wanauliza mbona tangu dhalim afyekelewe mbali na Corona matukio ya watu kutekwa na kubambikiwa kesi yamepotea kabisa?
 
Back
Top Bottom