Kwa kweli mpaka hapa tilipofika hakuna professionalism katila kuendesha nchi kwa sababu zifuatazo :-
Hivi Mazeliii wa nchi amekua mtu wa kusikiliza lawama za mtandaoni na kuamua mstakabali wa nchi ?!
Hivi Mazeliii amekua mpaka aone watu wanalilia jambo fulani ndio aamue lifanyike tena mtandaoni? Yeye kama yeye hashituki ?kutoa mwelekeo kbla mambo hayawa mabovu?
Huyu Mazeliiii ni wa kupangiwa nani afungwe nani asifungwe kweli ? Anajitoa akili kama hakuwepo serikali iliyopita sijui anafanya kufurahisha nini ?
Kweli kuna mapungufu yalikuwepo lakini Raisi wa nchi kawa mwepesi kiasi cha uwezo wake kujadiliwa na mtu mtandaoni na anafata ?
Raisi anashindwa kufanya vetting kwa usahihi hiii ni dhahili apelekeshwe na wala asijione anatusikiliza ! Kama jambo dogo kama hilo hataki kuumiza kichwa kufikia mwafaka no self decisions.
Note : Wananchi wengi wao wanauza matunda, fundi simu, fundi nyumba , wanashona viatu ,machinga, wakulima, wafanyabiashara wa chini na kati(wajasiriamali wadogo wadogo hawa ndio wananchi)
Kundi hapo juu lilitakiwa lipewe haki ya kusikilizwa pia kama hao wa mtandaoni wanavyopewa hio haki kwa sababu hao ndio wanaumia......kwa sababu feud kubwa ya viongozi wa ccm na vyama vya upinzani wasivishwe wananchi !! Kiasi kero zao zisisikilzwe.
Vyama vya upinzani na ccm ni tabaka la juu ambao wanatazama masilahi yao! Na sio wanachi wa kawaida? hao ndio wamekua wasemaji wao lakini ni wanajisemea wao kwa kiasi kikubwa na kujirekebishia njia zao haswa kwa haya yanayo endelea kwa sasa.
Wito wangu kwa Viongozi wakuu wa nchi huu upepo mnaochezeshwa kuanzia Raisi , TRA ,TPA, TBS mkisikia mtu mtandaoni mmekua wepesi sana kushtuka bila kuchunguza vizuri kwa sababu ya kuogopa tunawaomba muwe wajasiri na wachambuzi bila kuogopa mkuu atawaambia nini ? Msiende kwa upepo !.
Nimesikitishwa sana na kitendo cha kigogo 2014 kumpakazia kijana huko twitter anaitwa MPAMBAZI kwamba anasabuni za kemikali na kweli serikali imeshituka sijui huu uoga mmetoa wapi ?
Kijana alikua anamtetea diamond platnumz kwa sababu kawa tofauti na maamuzi ya kigogo 2014 wametuma taarifa mpaka kijana kaitwa " sifa hamu kama watamdhuru "
Ila naona jinsi serikali ilivyochezeshwa ikacheza na team mtandao kuzidi kipimo cha kawaida na sasa wamekua na kichwa kikubwa.
HATUZINDUI MIRADI IMESIMAMA.
WIZI NA UVAMIZI UNAZIDI.
AGENDA YA 2020/2021 to 2024/2025 YA TANZANIA HAONGELEWI.
KILA SIKU COVID 19 INAJADILIWA KUZIDI CHANGAMOTO ZINGINE WAKATI BALANCE INATAKIWA KUWEPO KWA SEKTA ZOTE 24.
AJALI BARABARANI ZIMEANZA KUREJEA TARATIBU HILI JAMBO HALINA TAMKO.
ASKARI WANAUWANA NA KUKAMATANA.
HUDUMA ZINATOKA TARATIBU NA KUSUASUA.
WATU HAWAELEWI MPANGO WA DODOMA UNAENDELEAJE ,? MAANA NI KAMA UMESIMAMA ?
ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI MBONA IMESIMAMA HATUONI UTEKELEZAJI WAKE , HATUONI MABADILIKO YALIYO ORODHESHWA HATUJUI TUPO WAPI TUNAELEKEA WAPI ?
WITO: Mama tunakuomba endelea kufatilia miradi kuna pesa zipo kule watu hawalipwi, miradi imesimama, na pesa inaliwa hapo dar es salaam JPM alitaka kuzindua miradi, hembu ikamilishe uzindue tazama progress,.
Punguza kutazama watu wa mtandaoni focus na ilani ya chama bado mambo hayajatimia na imebaki miaka minne.
Ajira millioni 8 zipo mkonono mwako.
SGR bado ....
Umeme wa nyerere bado...
Mishahara ipande hilo lipo mkononi mwako.
Mama nchi imepoa tukimbilie lengo letu.
Kazi iendeleee lakini sio kizembe.
Nawasilisha.