Interlacustrine R
JF-Expert Member
- Jan 22, 2022
- 7,186
- 14,274
Tatizo uwa mnapenda maslay queen
Kilichokutokea hata nami pia kilinitokea isipokuwa huyu alinikubalia kuwa Mpenzi wangu akatoka nami tukakaa mahali tukala tukanywa, bili ilitoka kama 48,000, nikawa namsikilizia anasemaje, cha ajabu akasema amefurahi kutoka nami out ila hajisikii kuliwa nami siku hiyo. Nilimkubalia tukaagiza uber tukasepa, nilipofika karibu na kwao tu alianza kaniambia ye ni jobless woman anahitaji support toka kwangu nimsaidie pesa ya matumizi nikashangaa...nilimwambia siku zote huwa anaishije bila mimi? Alijitetea oooh...huwa anasaidiwq na Ndugu zake mara ye ni single mother ana Watoto watatu anawalea mwenyewe ametelekezewa na Me, nikamwambia "pambana ndiyo ukubwa huo", alizidi kulalamika wewe...nikamwambia "kama anafanya biashara anijuze mapema maana hata hatujafungua mapenzi kivitendo nitaanzaje kuhudumia ghafla ghafla na je nina uhakika hatanibadilikia mbeleni kunikataa?" eti oooh nisiwe na wasiwasi wowote maana kashanikubalia nilimlipia uber nikataka niondoke akanishika mkono nilimkata jicho aliniachia mwenyewe. Baada ya siku 3 alinipigia simu na kuanza kulalamika"kwanini hunitafuti Mpenzi wako, unajua nimeamkaje, nimekula nini, nimeshindaje nikaona isiwe tabu basi nilimkubalia tu kuwa majukumu yalinizidi ndiyomaana aliona kimya" tukaagana, siku 2 mbele alirudia tabia yake ya kunilalamikia kuwa namkosea sana kutomtafuta nakati ye ni Mpenzi wangu, nilikuuliza alitakaje? Alinijibu kuwa simjali sijui hata anaishi vipi, anakulaje anavaaje au analipaje kodi nikamjibu kuwa "yeye si bora sana kiasi awe anatafutwa yeye tu bali hata nami anapaswa kunitafuta ndiyo maana ya upendo" alijitetea weee lakini nilisimamia hapo hapo. Nilikata simu, nili-block na kufuta kabisa no yake mazima. Miezi 6 sasa hatujawasiliana tena. Ke wa Kizazi chetu cha 2000 ni chuma ulete waliochangamka na pasua kichwa tupu.
Picha tafadhali ya wife material alivyokaa kishamba.wengi wenye akili hawana shape zinazovutia, wamekaa ki wife material, wanaonekana washamba balaa..!! Ila haya maisha bhaana..!!😂😂
Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.