🤣 kuna jamaa alipata wife material shapeless kabisa ila ana rangi ya wastani chocolate na anasura nzuri, ila ni pure shapeless 🤣. Walikaa kwenye mahusiano kama miaka 2 mpaka 3, Jamaa alimpenda sana na alikuwa anataka aanze mchakato wa kumuoa. Ghafla yule mwanamke shapeless kabisa akaanza kunenepa, ila kunenepa kwake ilikuwa juu kabakia mwembamba ila chini ndio unene wote unajaa, yule shapeless alifungasha msambwanda na mahipsi ambao sio wa kawaida ndani ya muda mfupi, ndani ya muda mfupi ilibidi jamaa yangu amfanyie shopping ya nguo maana nguo zote zilikuwa zinambana sana na zingine zilikuwa zina chanika kutokana na ukubwa wa mahipsi/msambwanda. Baada ya muda mfupi jamaa akaanza kuona mapicha picha 🤣. Mwanamke akaanza kumwambia wewe sio type yangu! Mara akaanza kumwambia wewe huwezi kunioa Mimi! Mara amwambie nahisi nilikosea kuwa na mahusiano na wewe! Huwezi kunioa mimi kisha unipeleke kunifuga mkoani (jamaa alipata kazi ya serikali mkoani)!
Mwisho wa siku ilibidi wa achane tu, mipango ya ndoa iliisha.
Jamaa alipata binti mwingine wa kumuoa
Yule binti kutokana na kuwa na msambwanda mkubwa, akaanza kupata masponsa wenye hela, akawa na vitu vya gharama simu za milioni tatu za iphone ndio zikawa zake, nguo za gharama , nywele za gharama, maisha ya gharama. Akaanza kusafirishwa kwenye mahoteli ya gharama zanzibar, South Africa, Kenya, Dubai. Baadae inasemekana alitiwa Mimba na sponsa na sponsa aliikataa, pia mke wa sponsa alimwambia atamtafuta na kumuua. Sasa hivi huyo dada ni single mother, kachoka, kazeeka, kachakaa karudi kijijini anafanya vibarua.