Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida imemhukumu kifungo cha maisha mkazi wa Mtaa wa Majengo, Fabiano Dubabe kwa kosa la kuwabaka na kuwalawiti watoto wake watatu.
Dubabe, aliyekuwa akijishughulisha na kazi ya ulinzi anatuhumiwa kutenda makosa hayo kati ya mwaka 2018 na 2022 kwa nyakati tofauti.
Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Robert Oguda alisema Mahakama imeridhishwa bila kuacha shaka kuwa, mtuhumiwa alitenda makosa hayo kinyume na sheria ya adhabu.
Alisema ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka umethibitisha bila kuacha shaka kwamba, mshtakiwa ana hatia kama alivyoshitakiwa.
“Mshitakiwa, Mahakama hii inakutia hatiani kwa makosa mawili ya kubaka watoto wako wawili wa kike kwa nyakati tofauti na kila kosa utatumikia jela miaka 30.
“Lakini unatiwa hatiani kwa makosa matatu ya kumwingilia kinyume na maumbile mtoto wako wa kiume, kila kosa utatumikia jela maisha yako yote,” alisema Hakimu Oguda.
Mwanasheria wa Serikali na Mwendesha Mashitaka, Nuru Chiwalo alisema mbele ya Mahakama hiyo kuwa mshitakiwa alitenda makosa hayo kati ya mwaka 2018 na 2022.
Chiwalo alisema jumla ya mashahidi 18, akiwamo mke wa mshitakiwa kwa nyakati tofauti walitoa ushahidi dhidi ya Fabiano.
Wakati akijitetea, mshitakiwa aliomba kupunguziwa adhabu kutokana na hatia aliyokutwa nayo kwa kuwa ana familia inayomtegemea.
MWANANCHI
Mama alitaka ampoteze huyo mwehu.wakati anafanya hayo Mke wake alikua yuko wapi na anafanya nini ?
je Watoto wenyewe wamethibitisha hilo ?
hizi habari zinakua na maswali mengi pengine kunakua na visasi maana kwa akili za kawaida mimi siamini kama Baba anaweza wafanyia hivo Watoto wake wa kuwazaa ila yote tumuachie Mwenyezi Mungu ndiye mjuzi zaidi 🙏
hai make sense hapa kuna kitu behind mimi akili yangu haikubali kabisa.Mama alitaka ampoteze huyo mwehu.
Kuna binadamu wanasikitisha sana...Wakati akijitetea, mshitakiwa aliomba kupunguziwa adhabu kutokana na hatia aliyokutwa nayo kwa kuwa ana familia inayomtegemea.
MWANANCHI
Ni kweli inatia shaka, lakini mbona nae kajitetea kwa kuomba kupunguziwa adhabu?hai make sense hapa kuna kitu behind mimi akili yangu haikubali kabisa.
sasa baba Mwenye akili zako uliwazaa mwenyewe una akili zako timamu sasa uvif…re hivyo vitoto ili iweje ?
bado hainiingii akilini
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Halafu alivyokuwa taahira ati naomba nipunguzie adhabu kwa sababu nina familia inanitegemea.
Familia inakutegemea kwa hicho kibako na kifiro?!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Hapo kama huyo Baba alifundishwa na Wamarekani?au tuwalaumu Wamarekani??
Nimecheka kaa fala 😂😂😂😂😂😂 daaah wengine mpaka nguruwe mkuuuNguvu za kiume sio dili kubwa Sana Kama zinavyohangaikiwa kuliko kuhangaika na maisha. Mbona wazungu nguvu zao kiduchu wanatumia ma toy ama kuwapeleka wapenzi wao kwa waafrika ili wawakaze Ila wanaishi poa zaidi kuliko sie. Inabidi zipunguzwe nguvu zinafanya watu wanafaki even animals mpaka kuku jamani