Awiaman ooza
JF-Expert Member
- Mar 25, 2023
- 512
- 866
😘🤗Mungu atunusuru.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
😘🤗Mungu atunusuru.
Nimecheka kaa fala 😂😂😂🤣🤣🤣🤣🤣 bongo raha sana eti afufuke mara 3Kwa maana nyingine, akifa leo akafufuka anapelekwa prison, akifia huko prison mara ya pili then afufuke anarudi tena ,mpaka afe mara tatu ndio hukumu imtoke😂
Ametenda makosa hayo kati ya mwaka 2018 na 2022Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida imemhukumu kifungo cha maisha mkazi wa Mtaa wa Majengo, Fabiano Dubabe kwa kosa la kuwabaka na kuwalawiti watoto wake watatu.
Dubabe, aliyekuwa akijishughulisha na kazi ya ulinzi anatuhumiwa kutenda makosa hayo kati ya mwaka 2018 na 2022 kwa nyakati tofauti.
Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Robert Oguda alisema Mahakama imeridhishwa bila kuacha shaka kuwa, mtuhumiwa alitenda makosa hayo kinyume na sheria ya adhabu.
Alisema ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka umethibitisha bila kuacha shaka kwamba, mshtakiwa ana hatia kama alivyoshitakiwa.
“Mshitakiwa, Mahakama hii inakutia hatiani kwa makosa mawili ya kubaka watoto wako wawili wa kike kwa nyakati tofauti na kila kosa utatumikia jela miaka 30.
“Lakini unatiwa hatiani kwa makosa matatu ya kumwingilia kinyume na maumbile mtoto wako wa kiume, kila kosa utatumikia jela maisha yako yote,” alisema Hakimu Oguda.
Mwanasheria wa Serikali na Mwendesha Mashitaka, Nuru Chiwalo alisema mbele ya Mahakama hiyo kuwa mshitakiwa alitenda makosa hayo kati ya mwaka 2018 na 2022.
Chiwalo alisema jumla ya mashahidi 18, akiwamo mke wa mshitakiwa kwa nyakati tofauti walitoa ushahidi dhidi ya Fabiano.
Wakati akijitetea, mshitakiwa aliomba kupunguziwa adhabu kutokana na hatia aliyokutwa nayo kwa kuwa ana familia inayomtegemea.
MWANANCHI
Ukishakutwa Na hatia mahakamani ukaombwa ujitetee huna namna nyingine ya kusema zaidi ya hiyo sababu tayari umeshakutwa na hatia hata usiposema hivo adhabu ipo pale paleNi kweli inatia shaka, lakini mbona nae kajitetea kwa kuomba kupunguziwa adhabu?
Huoni kama hapo inakuwa kama amekubali kosa?
Kujitetea kwake ingekuwa, sijatenda kosa ila.Ukishakutwa ba hatia mahakamani ukaombwa ujitetee huna namna nyingine ya kusema zaidi ya hiyo sababu tayar umeshakutwa na hatia hata usiposema hivo adhabu ipo pale pale
sasa ukishatoa utetezi wako mwisho ukatiwa hatiani unadhani kinachobaki nini kama sio kuomba upungizowe adhabu ?Ni kweli inatia shaka, lakini mbona nae kajitetea kwa kuomba kupunguziwa adhabu?
Huoni kama hapo inakuwa kama amekubali kosa?