aisee hii inatesa ndio changamoto ninayo pitia mimi. niliwambia wazazi wanitafutie binti wa kuoa huko kijijini kwetu baada ya kuona jitihada zangu zakupata mke zimegonga mwamba hapa mujini, binti alipatikana tena mzuri nika unganishwa nae tukayajenga na kukubaliana kabisa. shida imekuja kwenye mahali walikubaliana m1.6, wazazi wakasema sawa lakini sisi tutatoa m1 then kiasi kilicho baki kitamaliziwa siku za usoni maana kijana bado anajitafuta tunaomba na ndoa kabisa, wakakubaliana na siku ya kwenda kutoa. chaajabu baada ya siku kadhaa mzee wangu alipokea ujumbe kutoka kwa baba mkwe mtalajiwa ya kwamba mke wake kagoma ETI mpaka pesa ienee, nilishangaa sana mwisho nikawambia Kama hawataki basi wanitumie hala yangu nifanye mambo mengine. nime ambiwa nivute subira wanaweka mambo sawa, lakini kiukweli kama mambo nihaya naona kama kuoa itakua changamoto kwangu