Mzee umenikumbusha mbali sana,nakumbuka kipindi nipo form 3 nilikuwa muhuni sana,mbabe shule nzima,naenda shule asubuhi nimevuta bangi macho mekundu kinoma.
Nakumbuka ilikuwa ijumaa kipindi cha mwisho kabisa ,mwalimu wa English alikuwa anafundisha darasani,alarm ililia mda umeisha nikachukua begi langu hapo bado mwalimu yupo darasani maana alikuwa na tabia yakuendelea kufundisha hata kama alarm imelia,nikasema leo atanisamehe nasepa kuwahi kuvuta bangi alafu ilikuwa ijumaa nishahaidiana na demu wangu,nikambandue gheto kwangu...
Nikachukua begi nikampita mwalimu,mwalimu akaniambia unaenda wapi mimi bado nafundisha nikamwambia acha kunizingua mda ushaisha,mwalimu akanifuata kunizuia nikasimama,mwalimu mwenyewe ndo alikuwa ametoka chuo nalingana nae kwa mrefu sema umri kanipita miaka kadhaa.
Teacher akasogea akanikaba sweta,akanitandika kofi moja darasa nzima wanafunzi looooo,nikasema hapa ngoja nimfundishe mimi nani,alafu kipindi hicho nilikuwa najifunza taekwondo wanafunzi wote waliniogopa maana nilikuwa napiga mateke kama damme,wengine nilikuwa nawafundishaga wananipa vibuku buku vyao.
Nilivumilia kofi nikamsogelea,kidogo nikamtandika teacher bonge la kichwa,akaanguka chini ile anahamka akakutana na stop kick kule akaanguka kwenye meza iliyokuwa mbele ya darasa.
Teacher midamu inamtoka puani na mdomoni,akanifuata kashika mbao ya kuchorea mistari ubaoni,akairusha nikakwepa nilimpiga flying jump ushiro Teacher akaanguka akazimia,nikatoka nduki huku wanafunzi wanasema ameua ameua....
Ile natoka darasani,kumbe gheti lakutokea nnje ya shule limefungwa,nikakamatwa na walinzi,wakaniweka chini akaja academic master,alikuwa ametoka jeshini...aliomba fimbo kama yakuulia nyoka aisee nilipigwa na yule mwalimu,wanafunzi wa shule nzima wanaangalia huku wakiwa kimya,maana huyo academic aliogopeka sana,alinipiga mpaka fimbo ikavunjika vunjika akanza kunipiga kama mwizi nilikula kichapo heavy mpaka wale walinzi waliingilia...
Nikachukuliwa nikapelekwa ofisini kwa head master,nikapewa suspension nije na mzazi..
Nikamuelekeza mdingi akasema tutaenda shule jumatatu,kweli jumatatu imefika asubuhi mapema tushafika ofisini kwa head master,mdingi akaongea na head master mda mrefu sana wakaelewana,nikaambiwa nikawaomba walimu msamaha mbele ya shule nzima,nikagoma mdingi alinifuata alinitandika ngumi kama anapigana na mtu,alinikwida mpaka assembly,akanisimamisha aya omba msamaha haraka huku damu zinanitoka kama maji,wanafunzi wengine msameheni jamani msameheni..
Nikaomba msamaha mbele ya shule nzima,yule mwalimu niliyempa kichapa akahama shule,kwanzia siku hiyo nikapewa mkiranja washule nzima,wanafunzi waliniogopa mpaka namaliza o level heshima debe...