Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 378
- 766
Bunge la Tanzania limepitisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Kazi (NA.13) wa Mwaka 2024 ambao umeongeza likizo ya uzazi kwa wanaojifungua Watoto njiti ambapo itaanza kuhesabiwa wiki 40 baada ya Mama kujifungua huku Baba wa Mtoto njiti akipewa likizo ya siku saba badala ya likizo ya siku tatu.
Akiwasilisha maelezo ya muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Kazi wa Mwaka 2024 (The Labour Laws (Amendments) Bill, 2024)kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete Waziri wa Madini Anthony Mavunde amesema hayo jijini Dodoma Januari 31, 2025
Aidha, marekebisho ya muswada huu ni utekelezaji wa maombi yaliyotolewa na Chama cha Wafanyakazi katika Sherehe za Wafanyakazi (Mei Mosi) zilizofanyika May 01 Mei 2024 Mkoani Arusha baaya kutangaza kuongezeka kwa Siku za Likizo kwa Wanawake wanaojifungua Watoto Njiti (Kabla ya Wiki 36 za Ujauzito)