Baba Askofu Dr. Alex Gehaz Malasusa, Mkuu wa KKKT na mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Hospital ya KCMC ! KCMC ipo ICU!

Baba Askofu Dr. Alex Gehaz Malasusa, Mkuu wa KKKT na mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Hospital ya KCMC ! KCMC ipo ICU!

Attachments

  • downloadfile.jpg
    downloadfile.jpg
    1.1 MB · Views: 1
Msikilize huyu mtanzania!!

Mkurugenzi wa Hospital hiyo kubwa nchini,amejikita kwenye miradi ya ujenzi,akiachilia mbali maisha ya watu!

Idadi ya vifo ni kubwa mno, na Kuna uwezekano mkubwa mmiliki wa duka kubwa la majeneza nje ya hospital hiyo ni la wa Mkurugenzi wa KCMC

Manesi wamezidiwa kazi, wagonjwa ni wengi , madaktari wameanzisha vituo na hospital zao mjini kibao na Kila Kona na hazitumii Wala bima😭😭😭

Kuna tabia imezuka hospital ya KCMC, intern ni wengi kuliko manesi na madaktari.

Matokeo yake, huduma inatolewa below standard kupitia intern.

Kuna wazungu wapo intern,hawajui kitu chochote na sijui wanatokea nchi Gani ,ndio wanatunika kutibu watu ambao wengi wanafariki kukosa umakini na madaktari bingwa

Angalizo: Serikali ifanye ukaguzi WA mara Kwa mara kukagua mochwari ya hospital ya Rufaa ya Kanda ya KCMC, ilibkujua idadi ya watu waliofariki na sababu za vifo vyao,Hali ni mbaya mochari Kila siku imejaa!*
Tangu Malasusa arudi madarakani, hali hii imekuwa mbaya zaidi. Inawezekana huyu mzee wa Sumbawanga anawatoa watu kafara ili aendelee kukaa madarakani milele.
 
Habari nzuri sana hii kwa BAKWATA
Acha kulazimisha udini mahala pasipostshiki.
Mimi ni muislamu na nipo Moshi mjini.
Waislamu wa Moshi mjini na mikoa jirani pia wanaitegemea hospitali ya Kanda ya kcmc pale wanapokuwa na maradhi yaliyoshindikana katika hospitali ya mkoa ya Mawenzi.
Endapo huduma zikidorora katika hospitali ya kcmc watu wa Moshi watalazimika kufunga safari kwenda Muhimbili Dar esa salaam na hapo litakuwa ni tatizo la watu wa dini zote!
 
Kuongezeka kwa Maiti KCMC Wakati wa Weekend na Sikukuu za kitaifa

Katika hospitali ya KCMC, kuna mwelekeo wa kuongezeka kwa idadi ya maiti, hasa wakati wa weekend na siku za sikukuu za kitaifa. Wakati wa Ijumaa, Jumamosi, na Jumapili, hospitali inashuhudia wimbi kubwa la vifo. Hali hii inazidi kuongezeka wakati wa sikukuu ambapo shughuli nyingi zinaendelea, na watu wengi hawajishughulishi na kazi zao za kawaida.

Wakati huu, madaktari wengi huamua kuondoka hospitalini siku moja kabla ya weekend au siku ya sikukuu, wakielekea makwao au kwenye vituo vyao vya kutibu nje ya KCMC.

Hii inapelekea kupungua kwa huduma za matibabu katika hospitali, kwani madaktari muhimu wanakuwa hawapo. Uongozi wa hospitali pia unakumbwa na hali hii, ambapo mara nyingi wanakimbilia makao yao au vituo vya afya vya kibinafsi, wakiacha wanafunzi, manesi, na intern kufanya kazi bila usimamizi wa kutosha.

Hali hii inawatia wasiwasi wanafunzi na wanachuo wanaofanya kazi hospitalini, kwani wanakabiliwa na mzigo mkubwa wa kazi na changamoto za kushughulikia wagonjwa wengi bila msaada wa kutosha kutoka kwa madaktari wa kitaalamu.

Wakati wa weekend na sikukuu, idadi ya wagonjwa huwa kubwa, na hivyo inakuwa vigumu kutoa huduma bora.

Baada ya sikukuu au weekend kukamilika, ukipitia kwenye mochwari, utagundua kwamba imejaa maiti. Hii ni ishara ya wazi kwamba kuna tatizo kubwa katika usimamizi wa huduma za afya katika kipindi hiki.

Wakati wa matukio haya, ni rahisi kuona jinsi mfumo wa afya unavyoweza kushindwa kutoa huduma zinazohitajika, na hivyo kusababisha vifo vinavyoweza kuepukwa.

Ili kuboresha hali hii, ni muhimu kuanzisha mfumo wa TISS (Takwimu za Idadi ya Watu Wanaokufa) ndani ya utawala wa KCMC.

Mfumo huu utasaidia serikali na uongozi wa hospitali kupata takwimu sahihi za vifo vinavyotokea kila siku, kila wiki, kila mwezi, na kila mwaka. Kwa njia hii, wataweza kubaini mwelekeo wa vifo na kuchukua hatua zinazohitajika ili kuboresha huduma za afya.

Hali ya wagonjwa KCMC ni mbaya, na inahitaji umakini wa haraka. Kukosekana kwa madaktari wakati wa kipindi cha ongezeko la wagonjwa kunaweza kusababisha ongezeko la maafa na vifo.

Ni wajibu wa uongozi wa hospitali na serikali kuhakikisha kwamba kuna mtu anayeweza kusimamia huduma za afya hata wakati wa weekend na sikukuu, ili kuhakikisha wagonjwa wanapata huduma wanazohitaji.

Katika hali hii, ni muhimu pia kuwajengea uwezo manesi na wanafunzi wanaofanya kazi KCMC ili waweze kutoa huduma bora hata wanapokabiliwa na changamoto. Kuimarisha mafunzo na kutoa rasilimali za kutosha kwa wahudumu wa afya ni hatua muhimu katika kuboresha hali ya huduma za afya.

Kwa kuongezea, inahitajika kuwepo na mikakati ya kuhamasisha madaktari na wahudumu wengine wa afya kubaki hospitalini wakati wa kipindi hiki cha ongezeko la wagonjwa. Hii inaweza kufanywa kwa kuimarisha motisha na kutoa mazingira bora ya kazi.

Kwa kumalizia, KCMC inakabiliwa na changamoto kubwa katika kutoa huduma za afya, hasa wakati wa weekend na sikukuu.

Ni muhimu kwa uongozi wa hospitali na serikali kuchukua hatua za haraka ili kuboresha hali hii.

Kuanzisha mfumo wa TISS na kuimarisha usimamizi wa rasilimali za kiafya ni hatua muhimu katika kuhakikisha kwamba wagonjwa wanapata huduma bora na kupunguza idadi ya vifo vinavyoweza kuepukwa.
 
Ride Natty Ride
Ride Natty Ride lyrics
Dready got a job to do
And he’s got to fulfill that mission
To see his hurt is their
Greatest ambition
But we’ll survive
In this world of competition
‘Cause no matter what they do
Natty keep on comin thru
And no matter what they say
Natty de deh every day
 
CCM hii kauli inaonyesha mmekubaliana nayo.
Kidumu Cha Cha Mapinduzi
 

Attachments

  • VID-20250126-WA0016.mp4
    23.8 MB
Hali imepelekea wanaostahili kulazwa KCMC wanauguziwa vichochoroni. Ameumia staff mkubwa kwa ajali kavunjika mguu, hapa mjini lakini kakubali kwenda tibiwa BOMA, kalazwa chimba cha uwani na hataki kusikia neno KCMC.
Hii ni fedheha kwa hospitali yetu. Walio izunguka ni mapato ya kiasi gani yanapotea?
Na hali ikiendelea hivi, ipo siku patabaki majengo bila wagonjwa. Lau kama ndio lengo la mkurugenzi wa KCMC Mr, Masenga ajuwe limefikia 95% ya mafanikio. Lkn kama siyo lengo kutoa kitengo cha utabibu kibakie chuo pekee, namsihi achukuwe hatua za haraka mno. Laptop walizo nazo wanachuo wodini ni za kuchati muda wote, na baadae wanaenda kudanga Mimi'z, na kwenye Virokonya vya jirani, tena kwa kuwatapeli wazazi wao ety, kuna topic natakiwa nii downlood toka chuo flani america ama ulaya wazazi wanaenda kukopa kumbe hakuna chochote wanaibiwa.
Mfano Rafiki yangu nahifadhi jina, bint yake alipata ajali Dar, wakati ni mwanachuo KCMC wakati mchana wake aliwasiliana nae kumjulia hali na kamwambia yuko darasani KCMC.
 
Madaktari wengi wanapita hapo hospital kuelekea KCMC university,kufundisha,wanakimbia kutibu wagonjwa.

Kuna haja KCMC kuunda timu ya kugawa wanaotaka kufundisha chuo waende na wasitibu wagonjwa,na wanaotaka kutibu wagonjwa wasiende kufundisha chuoni hapo

Bila utaratibu huu, vifo vitakuwa vingi kupita maelezo.
Serikali pia ihusishwe as hizi hospital zinaendeshwa jointly kati ya kanisa na serikali
 
Masenga Yuko busy kujenga hospital yake karibu na shule ya msingi JK Nyerere..bonge la nyumba..juzi Kati kapigwa mifuko ya cement zaidi ya 100 na ndugu yake,aliomweka Kama msimamizi mkuu..well sad
 
Hiyo ni Hatari!
Swala la mishahara na stahiki nyingine liangaliwe!
Huenda ndiyo chanzo cha matatizo!
cc: Mwl.Gen Mhagama-for the action.
 
Msikilize huyu mtanzania!!

Mkurugenzi wa Hospital hiyo kubwa nchini,amejikita kwenye miradi ya ujenzi,akiachilia mbali maisha ya watu!

Idadi ya vifo ni kubwa mno, na Kuna uwezekano mkubwa mmiliki wa duka kubwa la majeneza nje ya hospital hiyo ni la wa Mkurugenzi wa KCMC

Manesi wamezidiwa kazi, wagonjwa ni wengi , madaktari wameanzisha vituo na hospital zao mjini kibao na Kila Kona na hazitumii Wala bima😭😭😭

Kuna tabia imezuka hospital ya KCMC, intern ni wengi kuliko manesi na madaktari.

Matokeo yake, huduma inatolewa below standard kupitia intern.

Kuna wazungu wapo intern,hawajui kitu chochote na sijui wanatokea nchi Gani ,ndio wanatunika kutibu watu ambao wengi wanafariki kukosa umakini na madaktari bingwa

Angalizo: Serikali ifanye ukaguzi WA mara Kwa mara kukagua mochwari ya hospital ya Rufaa ya Kanda ya KCMC, ilibkujua idadi ya watu waliofariki na sababu za vifo vyao,Hali ni mbaya mochari Kila siku imejaa!*
Hospitali za Mission waliziweza wazungu zijui kwanini waliwafukuza, kwasasa ni hospitali moja tu nchini zingine zote zikajifunzie huko "Consolatha Farthers Ikonda Makete"
 
Back
Top Bottom