Benny Haraba
JF-Expert Member
- Dec 7, 2012
- 15,670
- 14,647
Nadhani nikauli ya CCM hakuna aliye msahihisha viongozi wa kitaifa wanapaswa kutunza kauli zao wengi wakiwa nyuma ya mikamera hujitoa ufahamu 'a public figure has to keep his words'
Hili mbona halina ubishi, Humphrey Polepole ndiye msemaji wa CCM, alilosema ndiyo kauli ya CCM.Kauli ipi hiyo? Sikupata bahati ya kuisikia
Sasa mtu akikosa hekima inakuwaje? Tumlaani?Wakati huu dondoo kubwa ya taifa na ambayo serikali yetu inaipa msukumo mkubwa ni mapambano dhidi ya kirusi corona. Mapambano haya hayana mzaha wala kebehi na yanadai umoja na mshikamano wa kitaifa. Usemi wa Ndg. Polepole kwamba corona ni sawa na wapinzani ni lugha ya mtu anayeligawa taifa katika kipindi hiki kigumu.
Malezo yake mengine juu ya corona na madhara yake sina shida nayo. Bali kauli hii ya kebehi na kugawa watu katika makundi ya kisiasa wakati huu inamuonyesha yeye ni mtu wa jinsi gani. Kauli hiyo japo ya maneno machache imechujua hata mambo mengine aliyozungumza.
Wakati mwingine tunatamani kuwa mbali na baadhi ya watu kwa sababu uwepo wao huongeza mahangaiko ya mioyo. Mtu ni utu. Na utu ni kutambua uwepo wako na uwepo wa wengine hali tukitambua kuwa kila mtu anayo nafasi yake ya kuishi na kuitawala himaya yake ya maisha (personal doom).
Haya twaweza kuyatambua ama kwa akili au kwa hekima ambapo vyote viwili ni vipawa tulivyopewa na Mungu. Wakati mwingine akili zetu zaweza kushindwa kuchambua na kufikia maamuzi ya nini cha kusema au kufanya. Katika hatua kama hiyo ndipo huruhusu hekima kuingilia mchakato wa kufikiri kwa akili na kutupa mwongozo. Mara nyingi hekima hutuambia kwamba tutulie kwanza na kuahirisha maamuzi. Hekima hukinga maangamizi yawezayo kusababishwa hata na akili zetu.
Tunapomuomba Mungu atupe vipawa iwe pamoja na kumuomba kwamba vipawa anavyotupa vifanye kazi kwa ushirikiano. Kwa akili na hekima ushirikiano huo huwa wa kwenda sambamba pale tunapoamua mambo mema. Lakini pia wakati mwingine vipawa hivyo hufanya kazi pamoja kwa kutofautiana. Pale akili zinapofanya maamuzi kwa pupa hasa katika mambo ya maangamizi ni vema hekima ipewe nafasi ya kukataa ili kuepusha madhara.
Wakati huu wa kupambana na janga la kirusi corona tutapingana na mtu yeyote anayethubutu kutugawa na kuhangaisha mioyo ya watu kwa maneno yake. Tayari hofu ya corona inaleta mahangaiko mioyoni mwa watu. Taifa halihitaji kuongezewa hofu. Kinachohitajika sasa ni faraja na kuwapa watu matumaini ya kuishi. Sasa tunapambana na janga hili kama Watanzania na wala sio kama CCM na wapinzani. Pale akili zetu zinaposhindwa kufikiri au zinapofikiri vibaya basi tuipishe hekima itupe muongozo wa mambo ya kuzungumza na kufanya.
Mungu ibariki Tanzania!
Mungu tupiganie kama taifa
Afai kuongoza bali yafaa aongozwe
Wakati huu dondoo kubwa ya taifa na ambayo serikali yetu inaipa msukumo mkubwa ni mapambano dhidi ya kirusi corona. Mapambano haya hayana mzaha wala kebehi na yanadai umoja na mshikamano wa kitaifa. Usemi wa Ndg. Polepole kwamba corona ni sawa na wapinzani ni lugha ya mtu anayeligawa taifa katika kipindi hiki kigumu.
Malezo yake mengine juu ya corona na madhara yake sina shida nayo. Bali kauli hii ya kebehi na kugawa watu katika makundi ya kisiasa wakati huu inamuonyesha yeye ni mtu wa jinsi gani. Kauli hiyo japo ya maneno machache imechujua hata mambo mengine aliyozungumza.
Wakati mwingine tunatamani kuwa mbali na baadhi ya watu kwa sababu uwepo wao huongeza mahangaiko ya mioyo. Mtu ni utu. Na utu ni kutambua uwepo wako na uwepo wa wengine hali tukitambua kuwa kila mtu anayo nafasi yake ya kuishi na kuitawala himaya yake ya maisha (personal doom).
Haya twaweza kuyatambua ama kwa akili au kwa hekima ambapo vyote viwili ni vipawa tulivyopewa na Mungu. Wakati mwingine akili zetu zaweza kushindwa kuchambua na kufikia maamuzi ya nini cha kusema au kufanya. Katika hatua kama hiyo ndipo huruhusu hekima kuingilia mchakato wa kufikiri kwa akili na kutupa mwongozo. Mara nyingi hekima hutuambia kwamba tutulie kwanza na kuahirisha maamuzi. Hekima hukinga maangamizi yawezayo kusababishwa hata na akili zetu.
Tunapomuomba Mungu atupe vipawa iwe pamoja na kumuomba kwamba vipawa anavyotupa vifanye kazi kwa ushirikiano. Kwa akili na hekima ushirikiano huo huwa wa kwenda sambamba pale tunapoamua mambo mema. Lakini pia wakati mwingine vipawa hivyo hufanya kazi pamoja kwa kutofautiana. Pale akili zinapofanya maamuzi kwa pupa hasa katika mambo ya maangamizi ni vema hekima ipewe nafasi ya kukataa ili kuepusha madhara.
Wakati huu wa kupambana na janga la kirusi corona tutapingana na mtu yeyote anayethubutu kutugawa na kuhangaisha mioyo ya watu kwa maneno yake. Tayari hofu ya corona inaleta mahangaiko mioyoni mwa watu. Taifa halihitaji kuongezewa hofu. Kinachohitajika sasa ni faraja na kuwapa watu matumaini ya kuishi. Sasa tunapambana na janga hili kama Watanzania na wala sio kama CCM na wapinzani. Pale akili zetu zinaposhindwa kufikiri au zinapofikiri vibaya basi tuipishe hekima itupe muongozo wa mambo ya kuzungumza na kufanya.
Mungu ibariki Tanzania!
Mungu tupiganie kama taifa
Ccm ya mwalimu ilikuwa ya maadili sio hii sawa Na certified gang terrorist ambao iko sawa Na gang criminals kama vile mafia.Ccm imepoteza legitimacy ya kuongoza watu,Daima sitasema uongo
Hii ni ahadi ya mwana ccm
Mwambie muhashamu achukue kadi na kutangaza nia,mahaba yamepitiliza
Mkuu hivi kwa mtazamo wako, ktk hekma nani ana unafuu kati ya Magu na polepole?Kweli Askofu amenena kifalsafa. Polepole tatizo lake hashirokishi hekima ktk kupayuka kwake COVID-19 ni janga la KIDUNIA, unalihisishaje na CHADEMA. CCM haijapata mwenezi ina mlopokaje. Wazee wa CCm kama Mzee Mkapa, Msekwa, Kikwete, Magufuli, Mwandosa, Mwinyi kweli hawamuoni huyu mzee Kijana kuwa kweny hiyo nafasi ya anapwaya? CCM ni chama kikubwa san kinaitaji mwenez wa kuunganisha Taifa sio huyu Mzee Polepole anayehubiri migawanyiko.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona hujawaona viongozi wa CHADEMA hii vita ya maneno wameianza Chadema Muda tu. Sema ni vile tu CCM wamewajibu basi ishakuwa jambo??Sijui ni nini kimewapata viongozi wa CCM wa awamu hii. Hivi wamelogwa, wamelaaniwa au vyote kwa pamoja? Walahi kuna damu za watu zinawatesa. Haiwèzekani viongozi wajitoe ufahamu namna hii kama sio laana? Polepole think out my brother, Unalipeleka wapi hili taifa?
Kumbuka wewe ni kiongozi wa chama tawala tena msemaji. Kila unalosema watu wanaamini limesemwa na chama na umetumwa na chama kulisema. Kila neno unalotoa linahifadhiwa kama kumbukumbu kwa vizazi vijavyo.
na Chadema unafki ni kanuni ya roho zao au??CCM uongo ni kanuni ya imani
Hakuna la kumung'unya maneno katika swala la Korona.Wakati huu dondoo kubwa ya taifa na ambayo serikali yetu inaipa msukumo mkubwa ni mapambano dhidi ya kirusi corona. Mapambano haya hayana mzaha wala kebehi na yanadai umoja na mshikamano wa kitaifa. Usemi wa Ndg. Polepole kwamba corona ni sawa na wapinzani ni lugha ya mtu anayeligawa taifa katika kipindi hiki kigumu.
Malezo yake mengine juu ya corona na madhara yake sina shida nayo. Bali kauli hii ya kebehi na kugawa watu katika makundi ya kisiasa wakati huu inamuonyesha yeye ni mtu wa jinsi gani. Kauli hiyo japo ya maneno machache imechujua hata mambo mengine aliyozungumza.
Wakati mwingine tunatamani kuwa mbali na baadhi ya watu kwa sababu uwepo wao huongeza mahangaiko ya mioyo. Mtu ni utu. Na utu ni kutambua uwepo wako na uwepo wa wengine hali tukitambua kuwa kila mtu anayo nafasi yake ya kuishi na kuitawala himaya yake ya maisha (personal doom).
Haya twaweza kuyatambua ama kwa akili au kwa hekima ambapo vyote viwili ni vipawa tulivyopewa na Mungu. Wakati mwingine akili zetu zaweza kushindwa kuchambua na kufikia maamuzi ya nini cha kusema au kufanya. Katika hatua kama hiyo ndipo huruhusu hekima kuingilia mchakato wa kufikiri kwa akili na kutupa mwongozo. Mara nyingi hekima hutuambia kwamba tutulie kwanza na kuahirisha maamuzi. Hekima hukinga maangamizi yawezayo kusababishwa hata na akili zetu.
Tunapomuomba Mungu atupe vipawa iwe pamoja na kumuomba kwamba vipawa anavyotupa vifanye kazi kwa ushirikiano. Kwa akili na hekima ushirikiano huo huwa wa kwenda sambamba pale tunapoamua mambo mema. Lakini pia wakati mwingine vipawa hivyo hufanya kazi pamoja kwa kutofautiana. Pale akili zinapofanya maamuzi kwa pupa hasa katika mambo ya maangamizi ni vema hekima ipewe nafasi ya kukataa ili kuepusha madhara.
Wakati huu wa kupambana na janga la kirusi corona tutapingana na mtu yeyote anayethubutu kutugawa na kuhangaisha mioyo ya watu kwa maneno yake. Tayari hofu ya corona inaleta mahangaiko mioyoni mwa watu. Taifa halihitaji kuongezewa hofu. Kinachohitajika sasa ni faraja na kuwapa watu matumaini ya kuishi. Sasa tunapambana na janga hili kama Watanzania na wala sio kama CCM na wapinzani. Pale akili zetu zinaposhindwa kufikiri au zinapofikiri vibaya basi tuipishe hekima itupe muongozo wa mambo ya kuzungumza na kufanya.
Mungu ibariki Tanzania!
Mungu tupiganie kama taifa
Nina wasiwasi hujanielewa. Sijamaanisha vita ya maneno. Nimemaanisha athari ya maneno anayoyatoa kwa jamii kulingana na muda au jambo ambalo liko kwenye hiyo jamii hasa anapokuwa kiongozi "mwenye dhamana"Mbona hujawaona viongozi wa CHADEMA hii vita ya maneno wameianza Chadema Muda tu. Sema ni vile tu CCM wamewajibu basi ishakuwa jambo??
MOJAWAPO MAMBO NILIYOYAHIFADHI KWA KUMBUKUMBU NA REJEA KWA MIAKA IJAYO NI PAMOJA NA HII KAULI YA POLEPOLE. HIVI HUYU CCM ILIMWOKOTA WAPI?Sijui ni nini kimewapata viongozi wa CCM wa awamu hii. Hivi wamelogwa, wamelaaniwa au vyote kwa pamoja? Walahi kuna damu za watu zinawatesa. Haiwèzekani viongozi wajitoe ufahamu namna hii kama sio laana? Polepole think out my brother, Unalipeleka wapi hili taifa?
Kumbuka wewe ni kiongozi wa chama tawala tena msemaji. Kila unalosema watu wanaamini limesemwa na chama na umetumwa na chama kulisema. Kila neno unalotoa linahifadhiwa kama kumbukumbu kwa vizazi vijavyo.
WEWE ASKOFU, NI KAMA UNAMPIGIA MBUZI GITAA. UCHAFU NA MAASI WALIYOYAFANYA HAWA AKINA POLEPOLE NA CHAMA CHAO IMEKUWA LAANA KWAO. WANA MACHO LAKINI HAWAONI, WANA MASIKIO LAKINI HAWASIKII, WANA AKILI LAKINI HAWANA HEKIMA. NI USHETANI KWA KWENDA MBELE! SINA UHAKIKA KAMA POLEPOLE ALIWAHI HATA KUWAZA KUWA KUNA MUNGU AU KUNA KUFA. YEYE MAWAZO YAKE NI KWAMBA WATATAWALA MILELEWengi wanaelewa kama askofu aliyosema lakini mhusika sidhani kama ana akili hiyo ambayo askofu anaafikiri kuwa anayo.