Baba Askofu Munga: Akili na hekima. Corona sio sawa na Wapinzani

Baba Askofu Munga: Akili na hekima. Corona sio sawa na Wapinzani

HAPA TANZANIA KWA SASA VIRUSI VITATU HATARI NI CORONA, CCM NA POLEPOLE
 
Kweli Askofu amenena kifalsafa. Polepole tatizo lake hashirokishi hekima ktk kupayuka kwake COVID-19 ni janga la KIDUNIA, unalihisishaje na CHADEMA. CCM haijapata mwenezi ina mlopokaje. Wazee wa CCm kama Mzee Mkapa, Msekwa, Kikwete, Magufuli, Mwandosa, Mwinyi kweli hawamuoni huyu mzee Kijana kuwa kweny hiyo nafasi ya anapwaya? CCM ni chama kikubwa san kinaitaji mwenez wa kuunganisha Taifa sio huyu Mzee Polepole anayehubiri migawanyiko.

Sent using Jamii Forums mobile app
Usihofu, kuwa na amani. Kikao kijacho Cha nec ccm kitaondoka nae na kumrejesha aliyeomba radhi! Na wenye ajenda yao ni wenyeviti wastaafu na waliokuwa mashuhuri enzi zao! Na hoja yao ikikataliwa watasusa kumsaidia kupiga kampeni! Polepole analo Safari hii.
 
Wakati huu dondoo kubwa ya taifa na ambayo serikali yetu inaipa msukumo mkubwa ni mapambano dhidi ya kirusi corona. Mapambano haya hayana mzaha wala kebehi na yanadai umoja na mshikamano wa kitaifa. Usemi wa Ndg. Polepole kwamba corona ni sawa na wapinzani ni lugha ya mtu anayeligawa taifa katika kipindi hiki kigumu.

Malezo yake mengine juu ya corona na madhara yake sina shida nayo. Bali kauli hii ya kebehi na kugawa watu katika makundi ya kisiasa wakati huu inamuonyesha yeye ni mtu wa jinsi gani. Kauli hiyo japo ya maneno machache imechujua hata mambo mengine aliyozungumza.

Wakati mwingine tunatamani kuwa mbali na baadhi ya watu kwa sababu uwepo wao huongeza mahangaiko ya mioyo. Mtu ni utu. Na utu ni kutambua uwepo wako na uwepo wa wengine hali tukitambua kuwa kila mtu anayo nafasi yake ya kuishi na kuitawala himaya yake ya maisha (personal doom).

Haya twaweza kuyatambua ama kwa akili au kwa hekima ambapo vyote viwili ni vipawa tulivyopewa na Mungu. Wakati mwingine akili zetu zaweza kushindwa kuchambua na kufikia maamuzi ya nini cha kusema au kufanya. Katika hatua kama hiyo ndipo huruhusu hekima kuingilia mchakato wa kufikiri kwa akili na kutupa mwongozo. Mara nyingi hekima hutuambia kwamba tutulie kwanza na kuahirisha maamuzi. Hekima hukinga maangamizi yawezayo kusababishwa hata na akili zetu.

Tunapomuomba Mungu atupe vipawa iwe pamoja na kumuomba kwamba vipawa anavyotupa vifanye kazi kwa ushirikiano. Kwa akili na hekima ushirikiano huo huwa wa kwenda sambamba pale tunapoamua mambo mema. Lakini pia wakati mwingine vipawa hivyo hufanya kazi pamoja kwa kutofautiana. Pale akili zinapofanya maamuzi kwa pupa hasa katika mambo ya maangamizi ni vema hekima ipewe nafasi ya kukataa ili kuepusha madhara.

Wakati huu wa kupambana na janga la kirusi corona tutapingana na mtu yeyote anayethubutu kutugawa na kuhangaisha mioyo ya watu kwa maneno yake. Tayari hofu ya corona inaleta mahangaiko mioyoni mwa watu. Taifa halihitaji kuongezewa hofu. Kinachohitajika sasa ni faraja na kuwapa watu matumaini ya kuishi. Sasa tunapambana na janga hili kama Watanzania na wala sio kama CCM na wapinzani. Pale akili zetu zinaposhindwa kufikiri au zinapofikiri vibaya basi tuipishe hekima itupe muongozo wa mambo ya kuzungumza na kufanya.

Mungu ibariki Tanzania!
Mungu tupiganie kama taifa
Mchungaji pole sana kwa majukumu mazito ya kuendelea kuisimamisha kazi ya ukombozi ktk taifa letu na ulimwengu kama ambavyo aliinzisha kristo. Unaitenda kazi kwa uaminifu mkubwa wakati ambao tanzania ipo kwenye giza kuu. HAKIKA MCH. BWANA POLEPOLE ANA KIRUSI CHA AJABU ROHONI MWAKE NA KIRUSI HICHO NI HATARI KWA ROHO NYINGI ZA WATANZANIA 😂😂😂
 
wakati wa vita hilo laweza kutokea, nilikuwa na dharura ya kusafiri na nikabanwa kwenye foreni pale kipawa wakati nimebakiza robo saa ya check-in ndege ya kwenda Mwanza nilitelemka toka taxi nikakimbia kwa miguu, kuna wakati akili inajam; huku corona imebana huku Mbowe anahamasisha mikutano kabla ya wakati lazima maneno yapandane. pamoja na chadema kuwa ICU lakini huwezi kubeza kauli za kishawishi na kuleta shaka inayoweza kuleta sintofahamu ya usalama. Polepole hakudhamilia kutenda kosa. Askofu asituzingue apige goti aombee, ngome ya shetani imeingiliwa pembe yake imeinuka lakini nguvu za Mungu zitashinda asomaye na afahamu.
 
Back
Top Bottom