Baba Chaula: Polisi niambieni mwanangu kama yu hai tu basi inatosha, nahisi roho yangu inashindwa kuvumilia haya maumivu

Miongoni mwa mambo ambayo baada ya kuona hayaeleweki awamu ile yenye kufanana na haya ikabidi watu kila mtu kwa imani yake amsihi Mwenyezi Mungu wake kuingilia kati aonavyokufaa,
 
Ila wana dhambi.
Milioni 5 wamechukua na.
mtu wao wamemchukua.turudishieni basi hela zetu.au kiendacho kwa mganga hakirudi😁😁😁
 
Enzi za Mwl. Watu walikuwa wakiwekwa vizuizini ilikuwa inatangazwa,
Sasa hata zama hizi hayo mambo Basi yanafanyika kwenye chama vingi ambapo Uhuru wa kutoa maoni umeimarishwa zaidi na ndio maana siku hizi hakuanaga ule usemi wa β€œ zidumu fikra za Mwenyekiti β€œ
 
Mtoto wa watu wazazi wake watakuwa hawalali. Watakuwa wanajiuliza maswali mengi usiku na mchana. πŸ€”πŸ€”
Hatima ya watoto wao itakuwa vipi kwa mfano ?
Wa hai au kifani ?!
 
Yeye ndie supreme leader kwa sasa alipewa dhamana ya usalama wa wananchi na uhai wao,
Hivyo Mwenyezi Mungu anaanza kumwamgalia yeye kwanza ,
Je moyoni mwake anawiwa kiasi gani juu ya haya ?
Je anachukua hatua gani ktk kuingilia kati?
Je msimamo wake ni upi?

Hata kama Serikali ni taasisi lakini msemaji au Mwamuzi wa mwisho wa hiyo taasisi ni nani ?

Je ameamuaje kuhusu swala hilo la kutekwa wananchi ?
 
Uongozi wa SSH nao unabariki UOVU huu?

Imekwisha!!
 
Vijana kama unaweza ku avoid matatizo na serikali basi kaa pembeni tulia

Utaishia kuitesa familia yako bure na sacrifice yako haitakua na impact yoyote ile

Tutalalamika kidogo mitandaoni then tutakusahau kabisaa
akili zako zinatabirika sana!
 
Vijana kama unaweza ku avoid matatizo na serikali basi kaa pembeni tulia

Utaishia kuitesa familia yako bure na sacrifice yako haitakua na impact yoyote ile

Tutalalamika kidogo mitandaoni then tutakusahau kabisaa
Yaani badala ya kuona kwamba mtu/ watu kutekwa au kupotea katika mazingira tatanishi ni tatizo linalotakiwa watu kupaza sauti ili lisiendelee wewe unawanyamazisha watu. Tuna vyombo mbalimbali kama mtu ametenda kosa si inatakiwa achukuliwe hatua badala ya kutekwa?
 
Simlimchukulia poa Samia,sasa mnashughulikiwa na deep state nadhani sio Samia tena, kilio chenu wamekisikia cha kumnanga samia na kumkumbuka magufuli, kwaiyo wanamuenzi jiwe pamoja nanyi
hao deep state wao wako fiti kwenye mambo yasiyo na tija tu, ulinzi wa rasilimali za taifa haiwahusu?
 
Vijana kama unaweza ku avoid matatizo na serikali basi kaa pembeni tulia

Utaishia kuitesa familia yako bure na sacrifice yako haitakua na impact yoyote ile

Tutalalamika kidogo mitandaoni then tutakusahau kabisaa
Unawezaje kuepuka matatizo na serikali wakati upo kwenye mateso ya serikali?
Ukiona mpaka kijana anafungua mdomo wake kuikosoa serikali basi ujue amepita kwenye mateso ya serikali katika maisha yake mpaka amechoka kuvumilia na kuamua na liwalo liwe?

Wewe bado hujafikia hiyo hatua ukifikia utafunguka.
 

Mkazi wa Kijiji cha Ntokela wilayani Rungwe, Mkoa wa Mbeya, Yusuph Chaula (56) amemwomba Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati suala la mwanawe Shadrack Chaula kutekwa na watu wasiojulikana.

Shadrack anadaiwa kutekwa na watu hao Agosti 2, 2024 ikiwa ni takribani siku 20 kupita tangu alipotoka Gereza la Ruanda Mkoa lililoko mkoani Mbeya, alipokuwa amehukumiwa kifungo cha miaka miwili au kulipa faini ya Sh5 milioni.

Kijana huyo mwenye miaka 24 alitiwa hatiani na Mahakama ya Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya na kuhukumiwa kifungo hicho baada ya kukiri kosa la kuchoma picha ya Rais. Baadaye alichangiwa faini na watumiaji wa mitandao ya kijamii kisha kuachiwa huru.

Leo Jumatano, Agosti 7, 2024, baba mzazi wa Shadrack amezungumza na Mwananchi iliyotaka kujua nini kinaendelea au kama kuna taarifa zozote amezipata juu ya mwanawe.
Baba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…