Baba Diamond aomba mwanae amkatie angalau bima ya afya

Baba Diamond aomba mwanae amkatie angalau bima ya afya

Wala hata sihitaji ukaribu naye.

Hata namba yake sina.

Juzi mdogo wangu wa kike kanipigia simu eti "baba" amemwomba namba yangu, amempa lakini kaogopa kunipigia.

Hatukuwa na ukaribu tangu zamani, sioni kama tunahitaji kuwa na ukaribu sasa. Ila hatuna ugomvi.
Usiwe na moyo uliobeba visasi
Kusamehe ni kujiweka huru
 
Kwaiyo Kama kalea mwingine ndo ampotezee? Kwani hao wengine anawapa misaada wote wanapenda
Dini inasema kabla ya kuzihusia nafsi zingine iusie Kwanza nafsi yako
Ampotezee vipi wakati hajawahi kuwa na ukaribu naye ?
 
Usiwe na moyo uliobeba visasi
Kusamehe ni kujiweka huru
Kisasi gani tena ?

Kwani wewe una ukaribu na mimi ?

Huna, kwani inamaana nalipa kisasi au nina ugomvi na wewe ?

Tunaishi tu maisha ambayo tumekuwa tukiyaishi tangu zamani, kwanini alazimishe tuwe na ukaribu sasa hivi.

In short, nishamsamehe ila sihitaji ukaribu wowote.
 
Amkaushie tu pengine kamzaa njeee ya ndoa ndiyo maaana mond ana M harass
 
Kisasi gani tena ?

Kwani wewe una ukaribu na mimi ?

Huna, kwani inamaana nalipa kisasi au nina ugomvi na wewe ?

Tunaishi tu maisha ambayo tumekuwa tukiyaishi tangu zamani, kwanini alazimishe tuwe na ukaribu sasa hivi.
Mzazi ni tofauti na Mimi, bado Kuna nafasi kurekebisha palipoharibika.
Inawezekana mzee ametambua alipokosea.
 
Ukisoma comments nyingi humu ni zile zimeegemea upande mmoja!
Kwamba huyu Mzee alimtelekeza diamond! (inaweza kuwa kweli au laaa km Mzee alivyosema aliwaacha akiwa form one)
Sababu anazijua mwenyewe ...

Ila iliponigusa ni vile Huyu Mzee inaonekana ameshateseka vya kutosha mpaka kuomba hata akutane nao ili waweke mambo sawa ila inaonekana hili linashindikana!

Na kuna mahali anasema sababu ya kuachana na mama yake hata Diamond anaijua ~~~~nadhani hapa kuna jambo lipo chini ya kapeti ambalo Mzee hataki kuliweka wazi!

Ingawa inaumiza kutelekezwa na mzazi ila nadhani diamond angemsamehe mzazi wake inatosha sasa!
 
Wapumbavu sana nyinyi
Kwa nini?
Hakuna muda wa kujiuliza chochote na kuanza kutafuta excuses za kijinga linapokuja suala la kumsaidia mzazi wako even binadam mwenzako hasa unapokuwa ktk kiwango cha juu cha mafanikio yako,anachokifanya huyu ni kuendelea kujitafutia umaarufu kupitia matatizo ya baba yake jambo ambalo ni baya hakuna namna ya kulielezea likaeleweka.

Huyo mtoto ametoka kwenye kiuno cha huyu mtu kama siyo yeye huyo daimond angekuwepo leo?hivi ulishawahi kujiuliza ni kiasi gani amekosa utu hata ule wa kawaida wa binadam aliyekamilika?kuna siku nimesoma mahali alimpa mwanamke BMW zawadi ya kuzaliwa na wewe mpaka hapo bado hujajua kwanini mmeitwa"wapumbavu"?

Dude!!!you must be kidding.
 
Diamond ni mjinga sanaa,asichokijua kuwa mayeso ya mzee wake ndiyo yaliyompa hasira hadi akapambana hadi kufikia Hapo alipo kwanza angetakiwa amshukuru sanaa mzee .huenda baba asingefanya aliyomfanyia basi angekuwa bado kitaa anapambana na hali hii mbovu mbovu.
Co hilo tu angesoma na kufauru angekuwa mwalimu WA primary auto na degree yake anahaha na vyeti mtaan kusaka ajira auto pia angekuwa amepta ajira ila mshahara ndo ule WA kwenye kijiko ambao ni maden kwa mangi kila ck
 
Na ww tumechoka sema unalolijua
Achaneni na biashara ya Mond na Baba yake... Uzi wa aina hii si wa kwanza hapa.

LAKini kuna uzi kibao pia hapa za Diamond akimpiga dingi tough... Na diamond alishasema mara kibao anamsaidia mzee wake . Ujinga wa wapuuzi wengi hapa na waandishi wapumbavu kama huyo wa mwananchi of which siamini habari hiyo kama kweli ni MCL...Diamond anapokuwa na event maarufu basi ndo yanaona ndio mahala pa kuraise ishu yake na Baba yake... Lakini majinga hayohayo wala hayazungumzii all the charities done.

Wapuuzi kama hao huko Tabora ndo wa kusukuma ndani na kufyeekelea mbali....
 
Co hilo tu angesoma na kufauru angekuwa mwalimu WA primary auto na degree yake anahaha na vyeti mtaan kusaka ajira auto pia angekuwa amepta ajira ila mshahara ndo ule WA kwenye kijiko ambao ni maden kwa mangi kila ck
Umeonaee
 
Ukiachana na mkeo kwa vita, halafu mtoto abaki mikononi mwake.. Umekwisha!

Kuna sumu kali sana mtoto hulishwa na mama dhidi ya baba.. Tujitahidi kutunza ndoa zetu na hata ikibidi kuachana, tuwe makini tuachane kwa wema..

Halafu mzee Abdul bishoo kinoma. Ana tattoo za kibabe... Miaka 52? Inaonekana ujana wake ulikuwa wa motooo!
 
Achaneni na biashara ya Mond na Baba yake... Uzi wa aina hii si wa kwanza hapa.

LAKini kuna uzi kibao pia hapa za Diamond akimpiga dingi tough... Na diamond alishasema mara kibao anamsaidia mzee wake . Ujinga wa wapuuzi wengi hapa na waandishi wapumbavu kama huyo wa mwananchi of which siamini habari hiyo kama kweli ni MCL...Diamond anapokuwa na event maarufu basi ndo yanaona ndio mahala pa kuraise ishu yake na Baba yake... Lakini majinga hayohayo wala hayazungumzii all the charities done.

Wapuuzi kama hao huko Tabora ndo wa kusukuma ndani na kufyeekelea mbali....
Msaada wa Diamond kwa baba yake HAUONEKANI kama unavyoonekana kwa mama yake..
 
Duu kumbe
Mimi nimezaliwa mpaka namaliza kidato cha sita simjui baba.

Nimesoma kwa shida kubwa sana, kwa kuhangaika sana, kwa uongo uongo na kusaidiwa na wapita njia.

Baada ya kuhitimu kidato cha sita nilikutana na "baba" nikajua labda kwa kuwa hakunilea, sasa atatimiza majukumu yake bila shida, kumbe nilijidanganya tu.

Nimehangaika "mnooo" nimeshinda njaa mpaka siku 4, nimenusulika kuzimia kwenye daladala kwa njaa hapa Dar wakati wa kufukuzia kazi ya ulinzi. Nimekunywa sana juisi za kwenye makopo yaliyotupwa barabarani, nimelala sana mitaani Dar.

Najua alichopitia Diamond na wala hata sioni kama anamkosea huyo mzee. Hana tatizo naye ila ni kuacha kila mtu aendelee na maisha yake kama ilivyokuwa tangu zamani. Tusifuatane fuatane kama ilivyokuwa zamani.
 
Anapolilia bima ya afya, inamaanisha ni hii ya Tsh 50400? Au ni bima gani? Maana Chibu keshamzingua na hamtaki tena, kama dingi kaweza kuchora tatuu na cheni kavaa japo ya Kaliakoo, akomae kivyake, atafute hiyo fifty akipie bima ya afya maisha yaendelee. Kulia lia mitandaoni anaendelea kujitia aibu na kudharauliwa!
 
Back
Top Bottom