Baba Diamond aomba mwanae amkatie angalau bima ya afya

Baba Diamond aomba mwanae amkatie angalau bima ya afya

Jamaa anagawa misaada anashindwa kumkatia dingi ake hata CHF ya Tsh.30,000/=?
 
Aaha kimsingi ukiwa mama wa nyumbani unaletewa chakula na kila kitu inabdi uwe mpole tuu.. Ila mwanamke mtafutaji aisee hakubali huo Upuuzi...[emoji3][emoji3][emoji3][emoji1787][emoji1787] Yani moto unawakaa...
Huwajui wanawake ww, anaweza akawa mtafutaji lakini aking'ang'ania lake huwezi badili, mimi dada ni mwalimu sasa ndio ushangae.
 
Wewe unazani Diamond hatengi muda wake au unataka kila akifanya akuambie wewe.
Bahati mbaya Diamond na mama yake Ni watu wa mitandaoni karibia Kila anachofanya kuhusu maisha yao ya Kila siku kipo mtandani na hata hao wanawake aliozaa nao Ni watu wa mitandaoni wanapost karibia Kila kitu
 
Hajaendaaa south...!! Huo ndo ukweli.. Hata kwenye birthday zao hakwenda.
Sawa mwezi huu hajaenda na hujaisha, je unaijua hiyo miezi ya nyuma. Alafu kazi ya mziki sio kwamba kila siku utakuwa busy ila kwa sasa ni msimu wa siku kuu, kwa msanii yoyote lazima uwe busy.
 
Sawa mwezi huu hajaenda na hujaisha, je unaijua hiyo miezi ya nyuma. Alafu kazi ya mziki sio kwamba kila siku utakuwa busy ila kwa sasa ni msimu wa siku kuu, kwa msanii yoyote lazima uwe busy.
Haya sawa mkuu...Mwisho wa siku Jua zari ndo ataamua Love ya Watoto kwa Diamond huo ndo ukwelii...!!
 
Kwa hiyo sababu hujaona makamera una conclude Diamond haiangalii familia yake.
Mkuu hao wanawake aliozaa nao huwa wanalalamika mtandaoni jamaa hatengi muda na watoto wake. Hasa Zari Mara nyingi huwa anarusha madongo.
Kina kipindi diamond mwenyewe alilalamika Zari amemkatilia asiongee na watoto wake kwenye simu ikafika miezi 5 ndio babutale akaingilia kati akafunga Safari Hadi south kuweka Mambo sawa unajua waganda walivyo na dharua na kiburi
 
Jamaa anagawa misaada anashindwa kumkatia dingi ake hata CHF ya Tsh.30,000/=?
Ndio ushangae sasa,anamuona baba yake ana makosa kwa kumuacha mama yake wakati yeye akiwa mdogo,wakati yeye kafanya kosa lile lile kawaacha wale watoto wadogo kule SA,ndio ujue kuwa hiyo laana haitamuacha salama NA ukimuuliza kwanini kaachana na Zari atasema Zari ndio kamuacha yeye,sasa ndio wakati wa kujirudi kwa kuona kuwa it can happen to anyone and stop those accusation to his father...
 
Huwajui wanawake ww, anaweza akawa mtafutaji lakini aking'ang'ania lake huwezi badili, mimi dada ni mwalimu sasa ndio ushangae.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Huyo itakuwa kafa kaozaa...!! Ila hakuna mwanamke anakubali kuendelea kuwa na mwanaume anaeonyesha umalaya waziwaziii... Labda awe desparate sana na ndoaa yani yeye anachojali kaolewa bhasi...
 
Bahati mbaya Diamond na mama yake Ni watu wa mitandaoni karibia Kila anachofanya kuhusu maisha yao ya Kila siku kipo mtandani na hata hao wanawake aliozaa nao Ni watu wa mitandaoni wanapost karibia Kila kitu
Tatizo mnakalili, Diamond sasa yupo katika peak na ndio maana hata ratiba yake ipo busy na mziki sio kazi ambayo itakuweka busy miaka yote, Kuna kipindi mziki utamkataa ataangalia na atakuwa yupo karibu na familia yake, huku akisimamia biashara zake.
 
kitu mapenzi au mahusiano ni mambo magumu sana yanaweza kukufanya ukasahu damu yako kwa hasira diamond bana hajifunzi tu wanawaake walivyo tangu wema na wengine haon japo sawa ila huwez juaa mpk form one mama chib ndio anaachan na baba chibu kunanamna hapo kwa huyu mama
 
Ndio ushangae sasa,anamuona baba yake ana makosa kwa kumuacha mama yake wakati yeye akiwa mdogo,wakati yeye kafanya kosa lile lile kawaacha wale watoto wadogo kule SA,ndio ujue kuwa hiyo laana haitamuacha salama NA ukimuuliza kwanini kaachana na Zari atasema Zari ndio kamuacha yeye,sasa ndio wakati wa kujirudi kwa kuona kuwa it can happen to anyone and stop those accusation to his father...
Mkuu hii ndo Point ya msingi kabisaa..!!
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Huyo itakuwa kafa kaozaa...!! Ila hakuna mwanamke anakubali kuendelea kuwa na mwanaume anaeonyesha umalaya waziwaziii... Labda awe desparate sana na ndoaa yani yeye anachojali kaolewa bhasi...
Si ingiliagi uhuru wa kihisia wa dada zangu hata siku moja na mapenzi ni upofu.
 
Tatizo mnakalili, Diamond sasa yupo katika peak na ndio maana hata ratiba yake ipo busy na mziki sio kazi ambayo itakuweka busy miaka yote, Kuna kipindi mziki utamkataa ataangalia na atakuwa yupo karibu na familia yake, huku akisimamia biashara zake.
Eehe yani hata mzee wake alikuwa busy na Kazi tena malori hata miezi mitatu upo njiani tu unasafirisha mzigoo...!![emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] So its a same story hakuna tofauti...
 
Kuna somo la kujifunza hapa.

-SIna uhakika anayosema huyo mzee kwamba aliachana na mama diomond wakati yupo form 1......Mzee kakosea sana hata kama aliachana na mkewe ilibidi atoe matunzo ya mtoto,historia ya diomond inaonekana alikuwa anaokota makopo na sisal,kisha akawa anauza mitumba,ni wazi mzee alitupa mti na jongoo,diamond aliiba cheni ya mama yake ndio akaenda studio kutengeneza ngoma.

-Diamond samehe 7 mara 70 mzee kakubali kosa mpe msahada ingawa mama anaona ukimsaidia atenda kwa michepuke yake ila mbona hata mama yako naye ana ben10? We msaidie tu kashajirekebisha.
 
daimond kama upo humu mmu naomba itazame hii picha kwa makini.
 
Attachments

  • tapatalk_1541694405616.jpeg
    tapatalk_1541694405616.jpeg
    53.7 KB · Views: 14
Akifanya mahojiano na gazeti mwananchi baba mzazi wa msanii diamond platnumz ambemuomba mwanae angalau amkatie bima ya afya kwani Hali yake kwa Sasa sio nzuri. Ilinichukua muda kumshawishi na baadaye kufanya mahojiano na Abdul Juma Isack ambaye ni baba wa msanii wa maarufu wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz. Ungeweza kukata tamaa ya kuendelea kumshawishi kwa sababu ana hoja nyingi na pengine nzito.

“Sioni mabadiliko kwangu,” anasema baba huyo mwenye umri wa miaka 52 wakati akieleza sababu za kukataa kufanya mahojiano. “Tangu nianze kuhojiwa, nilikuwa nikiamini kuwa ningeweza kubadili msimamo wa mwanangu anayetajwa kuwa msanii tajiri namba moja Tanzania. “Badala yake naonekana kama nalilia kusaidiwa na mtoto wangu. Pamoja na kuwa na mtoto maarufu ndani na nje ya nchi, maisha yangu ndio kama hivi unavyoyaona. Naishi Magomeni Kagera na nyumba yangu ya kawaida tu, ambayo naamini hata siku Diamond akikwama kimaisha atakuja kuishi kwa kuwa hapa ni kwao, japokuwa simuombei hilo.”

Abdul anasema kwa muda mrefu Diamond amekuwa hafanyi mawasiliano naye na hajui sababu . “Najiuliza ni nini kikubwa namna hiyo nilichomkosea?” anahoji baba huyo. “Ninatamani siku moja nikutanishwe katika mahojiano na Diamond na mama yake ili kila mmoja atoe alilonalo moyoni.“Huyu mtoto kanipa majina mengi kutokana na yanayoongelewa mtaani kwamba nilimtelekeza, wakati hakuna ukweli wowote. Mimi niliachana na mama yake wakati akiwa kidato cha kwanza.

Kwa umri hu alikuwa anajielewa na anajua sababu za kuachana kwetu. Kama kuna jingine wanalolijua wao kwamba nimewakosea, basi tuhojiwe hata mbele za watu ili lifahamike na kuyamaliza kuliko hiki wanachofanya kwangu. “Kasababisha kila kona ninayopita nanyooshewa vidole kuwa niliwatosa. Ifike mahali haya mambo tuyaweke sawa kwa kuwa naumia sana, hawajui tu. Si kwamba, labda ni kwa kutaka msaada wao, hapana. Bali kila mtu awe ameitakasa nafsi yake na kuondokana na vinyongo.”

Baba huyo wa Diamond anasema hata mawasiliano na mzazi mwenzake ni pale anapojisikia. “Tena wakati mwingine na maneno ya karaha, lakini ana afadhali kuliko mtoto ambaye mara ya mwisho tuliwasiliana akiwa na Wema Sepetu ambaye alikuwa akija naye hapa mara kwa mara kunisalimia,” anasema.

Kwa sasa maisha si mazuri. Abdul anajihusisha na biashara ya viatu. Huchukua viatu kwa malikauli katika soko la Karume na kuvipeleka kwa wateja wake mahali walipo. “Lakini maisha kwa sasa si mazuri kwa kuwa nasumbuliwa na tatizo la miguu. Inanifanya wakati mwingine nishindwe kutembea muda mrefu,” anasema mzazi huyo.“Kama unavyoniona miguu inaniuma na wakati mwingine nashindwa kuinuka hata kitandani.

“Naona ni wakati sasa na mimi kuwa na eneo la kufanya biashara hii, lakini ndio hivyo uwezo, walau ningekuwa na gari ningeweza kuzunguka nalo hata kwa kuendeshwa ili nisiwapoteze wateja wangu, lakini sina namna.” Anasema hata uwezi wa kugharimia matibabu, hana. “Labda ningekuwa na bima ya afya ingekuwa msaada kwangu lakini ndio hivyo sina,” anasema.
Apata msaada mtandaoni

Hata hivyo, msaada wake mkubwa uko kwa mtoto wake wa hiari anayeishi London, Uingereza anayeitwa Zubeda. Walijuana na mtoto huyo katika mitandao ya kijamii baada ya kuona mahojiano yake akielezea maisha anayoishi.

Mwananchi sourceView attachment 968793
Mzee Abdul anavuna alichopanda akubali matokeo asonge mbele na maisha yake kwa umri wake apambane tuu na hali yake
 
Back
Top Bottom