Baba Diamond: Usisubiri nife mwanangu, nipeleke Hospitali

Baba Diamond: Usisubiri nife mwanangu, nipeleke Hospitali

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
So sad! Kuelekea Zari show. Baba yake Diamond ambae anaumwa sana miguu ameshindwa hata kutembea ameomba mwanae amsamehe kama baba na pia ameomba aje kumtembelea ampeleke hospitali asisubiri kufa.

Sisemi kwa ubaya, mi ni mmoja kati ya watu wanaojua maisha ya baba na mama waliotengena. Ukweli haijalishi uko level gani ugomvi wa mama yako na baba yako usiingilie hata siku moja tafadhalini...

Narudia tena, Diamond akifa leo baba yako hutopata Baba wa kukodi.

Kila la kheri..

==============

DIAMOND MWANANGU USISUBIRI NIFE!


Maskini! Wakati leo akiangusha pati ya nguvu na mpenzi wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady' inayokwenda kwa jina la Zari All White Party kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar, baba mzazi wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz', Abdul Jumaa yu hoi kitandani huku akimtaka mwanaye huyo kuonesha msamaha wa kweli aliotangaza kwenye vyombo vya habari na kwamba asisubiri hadi afe.


abdul jumaa.jpg
Baba mzazi wa ‘Diamond Platnumz'


TUJIUNGE NA CHANZO
Habari kutoka kwa chanzo makini kilicho karibu na baba Diamond kilidai kwamba kutokana na hali tete ya mzazi huyo ambapo kwa sasa anasumbuliwa na miguu kwa mara nyingine huku ikitoka magamba na kushindwa kutembea kwa muda mrefu, amekuwa akimlaumu mwanaye huyo kupita kiasi.


Chanzo hicho kilisema kuwa mzazi huyo amekuwa akisema kama alimkosea Diamond, alishamuomba msamaha na akasema amemsamehe lakini hakuonesha mabadiliko yoyote kwake wakati alikiri hadharani kupitia vyombo vya habari.

Kiliendelea kueleza kwamba kutokana na jambo hilo baba Diamond amekuwa akiumia kwani mwanaye huyo baada ya kutangaza amemsamehe hajaonesha mabadiliko yoyote ya kumjali.


MALALAMIKO
Chanzo hicho kilidai kwamba, baba Diamond amekuwa akilalamika kuwa ameugua kwa muda mrefu lakini Diamond hajawahi kwenda kumjulia hali hata siku moja.

"Ukweli baba Diamond anaumia sana. Sasa hivi anaumwa, ameshindwa hata kutoka nje, miguu imevimba na ina muonekano wa ajabu, amekuwa akisema hajui ni kwa nini mwanaye anashindwa kulegeza moyo wake na kumsamehe wakati alishakiri kwenye vyombo vya habari."Anasema bora akaenda sasa hivi wakasameheane kuliko asubiri hadi siku akifa ndipo aende," kiliongeza chanzo hicho.


BOFYA HAPA KUMSIKIA BABA DIAMOND
Baada ya kupata habari hizo, gazeti hili lilitinga nyumbani kwa baba Diamond au Dangote maeneo ya Magomeni-Kagera, Dar na kumkuta akiwa katika hali mbaya kwani miguu imevimba huku ikiwa imepoteza muonekano wa kawaida na kuwa na ngozi ya ajabu.

Baada ya salamu, wanahabari wetu walimuuliza kulikoni yupo katika hali hiyo na kama Diamond alikuwa amekwenda kumjulia hali ambapo alikuwa na haya ya kusema:"Ukweli nimeugua kwa muda mrefu lakini mwanangu Diamond hajawahi kuja kuniona.

AMTUMIA MESEJI
"Hali hiyo ilinifanya juzikati kumwandikia meseji ya kukata tamaa na kumwambia kwamba anaona ameshanizika kutokana na kunisahau kwake lakini Diamond hakunijibu.

"Namshukuru Mungu kwa sababu nina kibanda changu cha kulala, silipi kodi kuna watu walishanishauri eti niwatume watu wakaongee naye lakini nilikataa kwa sababu haoni thamani yangu.


ANASUBIRI NIFE?
"Kama ni tofauti na mama yake (Sanura Kassim), tulishamaliza na kabla hajaugua alikuwa anakuja kuniona, nikimuuliza kuhusu Diamond alikuwa akiniambia alishaongea naye lakini kila siku alikuwa akisema atakuja tu kuniona mpaka leo sijamuona labda anasubiri hadi nife ndiyo aje.

"Mara ya mwisho kumuona ilikuwa ni kipindi kile alivyomvisha pete ya uchumba Wema Sepetu ndiyo alimleta kwangu kumtambulisha, tangu hapo huwa namsikia tu kwenye vyombo vya habari. Inauma sana; "Yote kwa yote haya ni maisha tu."

DIAMOND YUPO BIZE
Ijumaa lilimtafuta Diamond ili kumfikishia habari juu ya baba yake ambapo hakupatikana hewani lakini watu wake wakaribu (Wasafi Classic Baby) walidai kwamba bosi wao huyo alikuwa yupo bize na Zari kwa ajili ya pati yao leo.

Chanzo: GPL
 

Attachments

  • ijumaafrontcopy.gif
    ijumaafrontcopy.gif
    93.8 KB · Views: 4,050
Mpwa vp! Niaje ni vp ni poa, leo utakuwa pande zp nkucheki
 
kwa hiyo analipiza kisasi?du jamani binadamu hatari kwa nini asimsamehe ili nae aje asamehewe hapo mbele ya safari,wengi tuliachwa na baba zetu kwa sababu moja au nyingine na siyo lazima kujua kwa nini baba yako alipotea,tunasubiri akianza kupukutika na kurudi mitaani kama kawaida ya wasanii wa bongo ndiyo tutaongea sana
 
Mkuu una point ila kwa nini unayaandika haya leo? Tena unaandika kabisa kulekea Zari Show???? Mambo ya kifamilia hayawezi kumalizwa namna hii!
 
huo msamaha amwombe mkewe labda ndio almasi atamwelewa
 
kwa hiyo analipiza kisasi?du jamani binadamu hatari kwa nini asimsamehe ili nae aje asamehewe hapo mbele ya safari,wengi tuliachwa na baba zetu kwa sababu moja au nyingine na siyo lazima kujua kwa nini baba yako alipotea,tunasubiri akianza kupukutika na kurudi mitaani kama kawaida ya wasanii wa bongo ndiyo tutaongea sana

Baba zetu nao wanazinguaga wana subiria wakishaona mtoto Kawa vizuri ndy hao wanaibuka
 
Pole Baba Diamond,ila iwe funzo kugombana na mama sio chanzo cha kuwatupa na watoto moja kwa moja,Diamond alilelewa na mama tu....Diamond Muangalie Mzazi wako kashaomba msamaha yaliyopita si ndwele ganga yajayo.
 
Mkuu una point ila kwa nini unayaandika haya leo? Tena unaandika kabisa kulekea Zari Show???? Mambo ya kifamilia hayawezi kumalizwa namna hii!

kwa zari show ndio nn what the hell kudos

baba ni baba tu zari show tupa kule .kwa hospital bei gani kipi zaid ya radhi ya mzazi na show za kijinga

wazazi ni Munguvwa pili haijarishi amekufanyia nn.

hingera pdidy kwa kumkumbusha domo
 
kwa zari show ndio nn what the hell kudos

baba ni baba tu zari show tupa kule .kwa hospital bei gani kipi zaid ya radhi ya mzazi na show za kijinga

wazazi ni Munguvwa pili haijarishi amekufanyia nn.

hingera pdidy kwa kumkumbusha domo

Hahahaha
 
mkuu una point ila kwa nini unayaandika haya leo? Tena unaandika kabisa kulekea zari show???? Mambo ya kifamilia hayawezi kumalizwa namna hii!

mkuu. Nimesoma kwenye web leo ya burudan..nisingesomanosingemwomba amsamehebabayake kingine malaika awaji. Marambili pengine. Mungu. Anamakusudi. Kaka abarikiwe. Kikamilifu kukumbusha und hayamatatizo yanaenda nakwamtoto. Anaezaliwa msipprekebisha.mnammtesa. Namtoto nae. Anakuja. Kumchukia. Babayake

heri wenye moyo safi maana wao watamwona mungu
 
Anasubiri rambi rambi nyiiingi akifa.
 
machimbo we pdidy hatari sanaaa ndugu yangu, m nakaa kivule bhana......
 
Duh hii inanikumbusha sakata la Dr Kigwangallah na Baba yake hali ilikuwa hivi hivi.
 
Back
Top Bottom