Hapa kuna vitu vingi vya kujifunza.
Hivi vyombo vya habari hasa magazeti ambayo yametumia picha zake kwenye front page ni kwamba.
Yanaenda kumuhoji lengo kuu sio kumsaidia lengo ni wao kuuza Magazeti yao.Maana hii habari sio mpya,ila wametega wapi pa kupata Kiki nzuri na wameona ni leo siku Ya ZARI Party.
Sasa naamini wameuza na kupata pesa lukuki,sasa wampelekee mgao na baba yake Diamond kwa kuwezesha wao kupata pesa nyingi kwenye hii Story.
Pili,Diamond atakuwa anajua mengi sana kuhusu mzee wake kuliko hata sie tunao comment.
Na pia huyo mzee anatumika kwa maadui wa Diamond hadi hii leo,hasa kwa kuzuazua hizi habari za ajabu ajabu.
We jiulize hii habari haina tofauti ya ya Marema Kanumba.Baba yake kanumba alilalamika eeee,mwisho wa siku kanumba alipofariki akaanza kugombania mali.Wakati malezi alikimbia.Sasa kwenye kipato ndio wao wanaangalia na wala sio kwenye msamaha.
Hawa wazee wengine watu tuwaangalie tu.Wauza magazeti naomba pesa nyingi mliopata kwenye Story mumtibu Baba yake Diamond ili muendelee kupata Story.
Labda pia niwaambie kitu kingine,maana mie napendelea sana kufuatilia Tv shows anazohojiwa huyu Diamond.
Diamond ni miongoni mwa wasanii wenye usiri mkubwa sana wa kutoa misaada kwa watu.Anasaidia watu wengie sana,na vijana wengi sana,na taasisi nyingi sana ila kimya kimya.Na kama akisema basi ujue ni ile ambayo ipo wazi sana.
Maana kama sikosei ana project kubwa ya vijana wa Mbagala,ambapo uwezo wa kufanikiwa ni mkubwa sana kulingana na plan alizoelezea siku anahojiwa.Na inaweza ndio kuwa project kubwa kuwahi kufanywa na msanii yoyote Africa Mashariki.
Amini msiamini,huyo mzee anasaidiwa na Diamond,ila mzee yoyote ambao aliwahi kushika pesa,sikufichi basi msaada mdogo kwake yeye anaona hakuna kitu.Na wengine wana Command kabisa wanachotaka.
ziada tu: Mzee mwenyewe kwenye picha anaonekana sharo wa kasi,sasa mnajuaje kama hiyo miguu inamuuma baada ya kuchukua wake za watu.Sasa amtibu aendelee kuchukua madem wa watu.
Familia zina siri nzito sana