PreGE2025 Baba Levo na kampeni ya mama hana deni, Bilioni 56 zatolewa kukamilisha mradi wa umwagiliaji Iringa

PreGE2025 Baba Levo na kampeni ya mama hana deni, Bilioni 56 zatolewa kukamilisha mradi wa umwagiliaji Iringa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mpepetaji

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2025
Posts
346
Reaction score
213
Kampeni ya Mama Hana Deni inayoongozwa na Msanii na Mtangazaji Baba levo imefika kwenye mradi mkubwa na wa kisasa wa Umwagiliaji Mkoani Iringa na kushuhudia namna ambavyo maji yanasafilishwa kwa zaidi ya kilometa 20 kuyafuata mashamba ya mpunga ya Wananchi wakulima Mkoani humo.

Zamani wakulima hao walikuwa wanateseka sana na upatikanaji wa Maji kwenye mashamba yao ya mpunga hadi kupelekea mazao kukauka na kupata mavuno kidogo au kutopata kabisa, walitumia njia za asili za kuchepusha maji kwa kutumia viroba lakini maji yaliwafikia wachache na yalikuwa hayafiki mashamba yaliyoko mbali na mto.

Serikali imetoa zaidi ya Bilioni 56 kwenye mradi huo ambao umekuwa mkombozi wa Wakulima wa mpunga kwani unaongeza mavuno kwa zaidi ya mara sita ya mavuno ya awali, na Wananchi wakisema kwa mradi huo Mungu atamlipa Rais Samia Suluhu Hassan kwani wao hawana cha kumlipa.

 
Back
Top Bottom