The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Mbunge mteule wa Kigoma Mjini, Clayton Revocatus (Baba Levo), amesema kuwa alitumia kila aina ya mbinu ili kushinda uchaguzi kutokana na nguvu na uzoefu aliokuwa nao mpinzani wake Zitto Kabwe katika jimbo hilo.
Mbubge huyo Mteule ameyazungumza hayo jijini Dodoma, ambapo ameeleza kuwa ushindi alioupata haukuwa rahisi kwani jimbo hilo lilikuwa na ushindani mkubwa kutokana na ushawishi mkubwa aliokuwa nao mpinzani wake.
"Baada ya uchaguzi nilimtumia ujumbe Zitto, lakini hakujibu chochote. Nadhani ni kwa sababu ya hasira baada ya kupoteza. Hata hivyo, bado kuna mambo mazuri ambayo Zitto anayo, na mimi nataka kuyatumia kwa ajili ya maendeleo ya Kigoma Mjini,” amesema Baba Levo.
Aidha, Baba Levo amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa majina matatu kwa ajili ya uchaguzi wa Spika wa Bunge, ambapo yeye ameweka wazi kuwa kura yake itamwendea Mussa Azzan Zungu kuwa Spika wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.