<div class="bbWrapper"></div>
- Tunachokijua
- Papa Fransisko ni kiongozi wa kanisa Katoliki duniani kote ambaye alianza majukumu yake tarehe 13 Machi 2024 akipokea kijiti hiko kutokea kwa mtangulizii wake Papa Benedict wa 16. Wakristo huwa na mfungo wa siku 40 ukitanguliwa na siku ya jumatano ya majivu ukijulikana kama Kwaresma. Papa Fransisko amekuwa akitoa ujumbe wa pasaka kuanzia mwaka 2014.
Madai
Kumekuwepo na ujumbe unaosambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ukieleza kuwa Papa Fransisko ametoa ujumbe wake katika mfungo wa kwaresima akiwataka watu wale chochote katika kipindi hiki kwani mfungo siyo kufunga kula bali ni moyoni.
“Kula chochote unachotaka katika Wiki Takatifu, dhabihu haiko tumboni bali moyoni.
Watu wanajizuia kula nyama, lakini hawaongei na ndugu zao, jamaa zao, hawatembelei wazazi wao na hawawatunzi watoto wao.
Hawagawi chakula chao kwa wale wanaohitaji, wanawatenga watoto wao na baba/mama na/au babu zao, wanakemea maisha ya wengine, wanamtesa mwenzao n.k. Nyama haikufanyi wewe kuwa mtu mbaya, vile vile minofu ya samaki haitakufanya kuwa mtakatifu.
Afadhali kutafuta uhusiano mzuri na Mungu kwa kuwatendea wengine mema. Hebu tupunguze kiburi na tuwe wanyenyekevu zaidi wa moyo.”
Uhalisia wa Ujumbe huo
JamiiCheck imefuatilia na kubaini kuwa ujumbe huu unaosambazwa haujawahi kutolewa na Papa Fransisko na hivyo si wa kweli. Kupitia ufuatiliaji wa wa Jumbe za pasaka alizozitoa Papa kuanzia mwaka 2014 tumebaini hakuna ujumbe ambao papa aliongelea swala la watu kula chochote kipindi cha kwaresima. Tazama hapa kuona jumbe za papa Francis kuhusu kwaresma kuanzia mwaka 2014.
Ufuatiliaji pia umebaini kuwa ujumbe huo umekuwepo tokea Februari 2024, kutokea katika mtandao wa Facebook na baadae kusambazwa katika mitandao mingine ya ikiwemo X zamani, Twitter.
Ujumbe wa papa kuhusu kwaresima kwa mwaka 2025 kwenda kwa wakatoliki uliotolewa Februari, 6 una kichwa kinachosema “Tusafiri kwa pamoja kwa matumaini” ambapo katika ujumbe huo ameeleza ni kwa namna gani waumini wanaweza kushiriki katika safari ya matumaini. Tazama hapa