Baba mtoto kanitelekeza

Baba mtoto kanitelekeza

Duuuh! ulishindwa kufanya jitihada za kumbadilisha huyo baba mtoto?
Pole sana kwa kuingia kwenye usingomadha,ulikua na nafasi yakuepuka USIMBE,vijana watakusifia sana na kumponda jamaa,ili uwaone wao wa maana,uwachanulie miguu,hadi watakapowapata wenza wao wa kuwaoa.Pole sana.
 
Habarini?

Ninaomba nieleweke kwamba mimi si mgeni, nimekua nikisoma mijadala mbalimbali lakini leo nami nimewiwa nilete kisa changu ambacho ninaamini kwa namna moja au nyingine kitawasaidia watu kadhaa.

Mimi mwanamke wa miaka 32, nimeajiriwa mahala Fulani. Kiukweli, nilikua kwenye mahusiano Kwa muda mrefu sana tangu nikiwa chuo hadi hivi majuzi. Hali ya mahusiano yetu yalikua ya kusuasua mno. Leo mko poa, kesho majanga hali ambavyo ilinikatisha tamaa sana. Ingawa jamaa alinitamkia ndoa wakati Fulani lakini binafsi kwa tabia za jamaa, sikuona hata kivuli endapo tungefunga ndoa.

Mwenzangu kwanza ni mnywaji sana wa pombe kiasi kwamba mara kadhaa ilimletea shida kwenye ajira yake na alisimamishwa mara nyingi sana. Mbali na hiyo, ni mtu ambaye bado hajui anataka nini. Leo mtapanga hiki, kesho mtagombana muanze upya so mnakua mara kadhaa hakuna mtakachokamilisha.

Mara nyingine anadai anataka kuoa mtu wa kabila lake, mara anaweza kuanzisha mahusiano na vitoto vya chuo ingawa yeye ana 36 years.

Kwa mahusiano yetu ya miaka Zaidi ya nane, hatukuwai kujaliwa mtoto ingawa jamaa alinitamkia mara moja akisema ananiacha sababu simpi mtoto then baadaye akaomba msamaha na maisha yakaendelea.

Mungu si Athuman! Mwezi wa tano nilijigundua ni mjamzito. Nikamshirikisha mwenzangu ambaye hakuwa na furaha nayo kabisa. Akanishauri sana tutoe tukizingatia bado tunajitafuta and blablabla.

Kiukweli mimi nilifurahi mno nilipojigundua ni mjamzito. Hata wazo la kutoa sikua nalo kichwani. Niliamua moyoni hata kama jamaa ataamua kuondoka lakini priority ya kwanza ni mtoto wangu.

Kweli, jamaa alihangaika sana kunishawishi kutoa ili tuendeleze mahusiano (ambayo hayana dura) nikaamua kuweka msimamo wangu kwamba akijisikia kuondoka, aondoke ila mtoto kama lolote likitokea basi liwe limepangwa na Mungu ila sipo yeye. Aliamua kuondoka na wala sikujushughulisha naye kabisa.

Ninamshukuru sana Mungu kwa kunisaidia safari yangu ya ujauzito hadi sasa, hakuna kilichonisumbua. Kiukweli, nina furaha na amani zote, sielewi ni kwa nini. Nimejikuta natamani kuwaambia wanawake wenzangu, wasikubali kuendeshwa na wanaume wa namna hii ili kuendeleza mahusiano.

Focus na unachokichagua kwani hata ningetoa, sio kweli kwamba mahusiano yangeboreka, tena yangekua mabaya zaidi. Ninamshukuru sana na niwatakie jioni njema.
Pole mkuu lakini kwann ulijitesa kukaa miaka mingi kwenye mahusiano yasioleweka aisee
 
Pole sana miaka 8 si kitoto ni mingi sana. Sema dada zetu hawa nao kuna muda akili zao hazina akili, anaweza tokea mtu wa maana anataka kujenga nae future na amuoe, dada mwenyewe sasa kakomaa na limtu lisilo na dira kabisa, mipombe, kubeti, visuruali vya kubana. Hovyo sana wadada
 
Duuuh! ulishindwa kufanya jitihada za kumbadilisha huyo baba mtoto?
Pole sana kwa kuingia kwenye usingomadha,ulikua na nafasi yakuepuka USIMBE,vijana watakusifia sana na kumponda jamaa,ili uwaone wao wa maana,uwachanulie miguu,hadi watakapowapata wenza wao wa kuwaoa.Pole sana.
Mkuu uwezi kumbadilisha mtu tabia ni ngozi aisee moja kati ya kitu kinachofanya ndoa za siku hizi zisidumu ni kuingia kwenye ndoa ukiamini mwenza wako atabadilika tabia zake mbaya inakua tofauti na matarajio mnaishia kuachana tu.
 
Habarini?

Ninaomba nieleweke kwamba mimi si mgeni, nimekua nikisoma mijadala mbalimbali lakini leo nami nimewiwa nilete kisa changu ambacho ninaamini kwa namna moja au nyingine kitawasaidia watu kadhaa.

Mimi mwanamke wa miaka 32, nimeajiriwa mahala Fulani. Kiukweli, nilikua kwenye mahusiano Kwa muda mrefu sana tangu nikiwa chuo hadi hivi majuzi. Hali ya mahusiano yetu yalikua ya kusuasua mno. Leo mko poa, kesho majanga hali ambavyo ilinikatisha tamaa sana. Ingawa jamaa alinitamkia ndoa wakati Fulani lakini binafsi kwa tabia za jamaa, sikuona hata kivuli endapo tungefunga ndoa.

Mwenzangu kwanza ni mnywaji sana wa pombe kiasi kwamba mara kadhaa ilimletea shida kwenye ajira yake na alisimamishwa mara nyingi sana. Mbali na hiyo, ni mtu ambaye bado hajui anataka nini. Leo mtapanga hiki, kesho mtagombana muanze upya so mnakua mara kadhaa hakuna mtakachokamilisha.

Mara nyingine anadai anataka kuoa mtu wa kabila lake, mara anaweza kuanzisha mahusiano na vitoto vya chuo ingawa yeye ana 36 years.

Kwa mahusiano yetu ya miaka Zaidi ya nane, hatukuwai kujaliwa mtoto ingawa jamaa alinitamkia mara moja akisema ananiacha sababu simpi mtoto then baadaye akaomba msamaha na maisha yakaendelea.

Mungu si Athuman! Mwezi wa tano nilijigundua ni mjamzito. Nikamshirikisha mwenzangu ambaye hakuwa na furaha nayo kabisa. Akanishauri sana tutoe tukizingatia bado tunajitafuta and blablabla.

Kiukweli mimi nilifurahi mno nilipojigundua ni mjamzito. Hata wazo la kutoa sikua nalo kichwani. Niliamua moyoni hata kama jamaa ataamua kuondoka lakini priority ya kwanza ni mtoto wangu.

Kweli, jamaa alihangaika sana kunishawishi kutoa ili tuendeleze mahusiano (ambayo hayana dura) nikaamua kuweka msimamo wangu kwamba akijisikia kuondoka, aondoke ila mtoto kama lolote likitokea basi liwe limepangwa na Mungu ila sipo yeye. Aliamua kuondoka na wala sikujushughulisha naye kabisa.

Ninamshukuru sana Mungu kwa kunisaidia safari yangu ya ujauzito hadi sasa, hakuna kilichonisumbua. Kiukweli, nina furaha na amani zote, sielewi ni kwa nini. Nimejikuta natamani kuwaambia wanawake wenzangu, wasikubali kuendeshwa na wanaume wa namna hii ili kuendeleza mahusiano.

Focus na unachokichagua kwani hata ningetoa, sio kweli kwamba mahusiano yangeboreka, tena yangekua mabaya zaidi. Ninamshukuru sana na niwatakie jioni njema.
Hii dunia ina watu wa ajabu sana. Mmoja wapo ni wewe mleta mada.
 
Pole sana wakati mwingine usilazimishe mtu akupende ukiona hauelewi piga chini endelea na maisha yako, furaha yako ipo kwenye hatma yako mwenyewe.
 
Back
Top Bottom