Baba, mtoto wako yuko huru kukueleza jambo lolote?

Baba, mtoto wako yuko huru kukueleza jambo lolote?

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,648
Wakuu,

Wewe unayeitwa baba, uwe mlezi au mzazi, mtoto wako yuko huru kuongea na wewe kuhusu jambo lolote ikiwa anahitaji kusikilizwa na wewe? Au ndio wawe wale wazazi wakali mpaka mtoto akueleze kitu inabidi atume barua ya maombi kwanza?

dad and daughter.jpg


Mbali na kuwa na uangalizi wa mama, kusikilizwa na baba ni muhimu pia. Kuna watoto wananyanyaswa sana na mama zao wa kambo (siyo mama kambo wote ni waovu, wengine wana roho nzuri sana Mungu awaongezee baraka) au hata mama zao wa kuwazaa (tumeona na kusikia matukio mengi kwenye haya) wafanyakazi wa ndani, shuleni nk. Ikiwa mtoto ana changamoto au anataka kuongea tu na wewe akueleze wiki yake ilikuaje, amepata rafiki mpya shuleni, kuna tatizo nyumbani, amejifunza kitu kipya, yupo huru kuongea na wewe bila uoga?

dad and son.jpg


Kwa upande wangu aisee Mzee aliwakuwa mkali sana. Yaani mkimuona baba anajukuja kila mtu anatafuta kazi ya kufanya, na ukifanya kosa siku hiyo ukaambiwa ngoja baba yako arudi aisee siku hiyo inakuwa kama kiama. Wakati mwingine ikiwa unahitaji kitu ilibidi uandike barua na humpelekei mkononi, unaenda kuitegesha chumbani kwake ambako itaonekana unakaa unasubiri majibu!

Wewe baba mzazi/mlezi mtoto wako yupo huru kuongea na wewe ikiwa amepata tatizo au tu kucatch up na kupiga story na wewe?
 
Back
Top Bottom