Baba " mwanangu upo tayari taratibu za ndoa ziendelee'' @Etugrul bey" ndio baba''

Upele humuota aisiee na kucha aisee.. maana wengne kila kukicha tunatafuta wake wakuwaweka ndani.. ila polee mkuu
 
Nakuelewa ndugu yangu!

Kuna mahala uligusia baadhi ya sifa alizonazo mkeo (uliyemtaliki). Kwa sifa ulizoziainisha ni nzuri na ni aina ya mwanamke ambaye tunamgombania wanaume katika jamii.

Ninachokihofia juu yako ni kuwa chanya ya kitu kwa binadamu inatambulika baada ya kukikacha hicho kitu.

Maadamu unaona utafamnyia dhuluma pengine inaweza ikawa endelevu ndani ya ndoa basi talaka ndio njia iliyobakia na ni ndio njia uliyoifuata.

Mungu akupatie la heri kwenye kuchagua jema. Ikiwa umepata mwengine usiingie katika msukumo wa maamuzi ulifanyika kwenye ndoa yako ya kwanza.

Na ikiwa moyo wako utarudi nyuma jambo pekee unaweza kufanya ni kumuomba Mungu akupatie mahaba kwa mke wako.

Kama binadamu nina hisia (naguswa). Sisi wanaume ni tofauti na wanawake; namuonea huruma sana huyo mwanamke uliyemtaliki.
 
Asante mkuu Kwa maoni yako mazuri sana
 
Mimi niseme Tu nashukuru Kwa maoni yako mkuu....wanasema ukitaka kujua uhondo wa Ngoma basi ucheze! Mwenzio nimecheza wewe bado kwahiyo sikulaumu Kwa mtazamo wako
 
Mimi niseme Tu nashukuru Kwa maoni yako mkuu....wanasema ukitaka kujua uhondo wa Ngoma basi ucheze! Mwenzio nimecheza wewe bado kwahiyo sikulaumu Kwa mtazamo wako
Napenda sana watu wa kweli, kwenye suala la ndoa nipo na nimeona.

Shida huwa hamtaki kuwa wa kweli, ulikiri kabisa kuna muda ndoa ilikuwa ya furaha na amani,halafu unakuja kutupanga. Hapo inaonyesha wazi mke ndiyo ameomba Talaka.
 
Mjinga nae ni mtu mkuu...godoro usilolilalia hujui kunguni wake!

Hlf huu upuuzi WA kusema kuwa mwanamke akikupenda ndio mambo Safi mmetoa wapi?
 
Napenda sana watu wa kweli, kwenye suala la ndoa nipo na nimeona.

Shida huwa hamtaki kuwa wa kweli, ulikiri kabisa kuna muda ndoa ilikuwa ya furaha na amani,halafu unakuja kutupanga. Hapo inaonyesha wazi mke ndiyo ameomba Talaka.
Mkuu mke hajaomba talaka...Mimi ndo nimetoa talaka....sio tatizo langu wewe kukubali au kutokubali
 
Hizi habari za hisia mbona sizielewi? Vidume mbona mnakamua Malaya kila siku ambao hamna hisia nao? Kuna wale mnawala kimasihara hisia hutoka wapi?
Kaka ndoa na Kula Malaya vitu viwili tofauti....ukioa ndio utaelewa vizur mkuu
 
Kuna kutokumpenda mtu na kutokuwa na hisia naye. Inabidi utofautishe haya.

Huyo mtoa mada huyo mwanamke alimpenda sema huko katikati yakatokea ya kutokea.

Napenda sana watu wakweli.
Okay naona wengi hamkunielewa....huyo mwanamke sijampenda na ndio maana nikatumia kutokuwa na hisia nae...na kama mtu humpendi hisia zitatoka wapi? Au hisia kwenu ni za kufanya mapenzi Tu au?
 
Okay naona wengi hamkunielewa....huyo mwanamke sijampenda na ndio maana nikatumia kutokuwa na hisia nae...na kama mtu humpendi hisia zitatoka wapi? Au hisia kwenu ni za kufanya mapenzi Tu au?
Sasa kuna hisia nyingine zaidi ya Mapenzi tunazo zihusisha na ndoa ?

Nipe faida hizo hisia nyingine tuzijue. Mfano wanao chukua malaya huwa wanawapenda au anakuwa na hisia tu za kukidhi haja ?

Ndiyo maana sisi tukasema kukosa hisia siyo sahihi ukisema hukumpensa hilo jambo moja lakini katika maelezo yako ulituambia ya kuna kitambo mliishi kwa furaha na amani. Hili lilitokana na hisia au upendo ?

Naendelea kusisitiza ya kuwa napenda sana waru wakweli.

Haya si maeneo yangu, ngoja nirudi nilipo toka.

Shukrani sana.
 
Mkuu kinyume cha furaha na Amani ni ugomvi na kutokuwa na maelewano....kuwa na furaha na Amani haimaanishi kwamba ndo kumpenda mtu...niambie kama tumeelawana hapa Kwanza?
 
Mkuu kinyume cha furaha na Amani ni ugomvi na kutokuwa na maelewano....kuwa na furaha na Amani haimaanishi kwamba ndo kumpenda mtu...niambie kama Kwanza tumeelawana hapa Kwanza?
Huyo ni mke hatuongelei mtu kando. Furaha na amani kwenye ndoa inaletwa na mapenzi na upendo.

Sisi tumeoa tuna wake, usione nakuweka sawa juu ya hili, sababu uko mbali na uhalisia.
 
Huyo ni mke hatuongelei mtu kando. Furaha na amani kwenye ndoa inaletwa na mapenzi na upendo.

Sisi tumeoa tuna wake, usione nakuweka sawa juu ya hili, sababu uko mbali na uhalisia.
Tatizo unataka kile unachoamini wewe ndo kiwe kwangu.....hapa tutatofautiana Hadi kesho
 
Huyo ni mke hatuongelei mtu kando. Furaha na amani kwenye ndoa inaletwa na mapenzi na upendo.

Sisi tumeoa tuna wake, usione nakuweka sawa juu ya hili, sababu uko mbali na uhalisia.
Lete hoja nyingine.....Ila nitarudi baadae nachek tamthilia sasa hivi
 
Tatizo unataka kile unachoamini wewe ndo kiwe kwangu.....hapa tutatofautiana Hadi kesho
Hapa naongelea uhalisia sababu uhalisia upo. Sasa unapoleta habari ambazo hazina uhalisia tunazirudisha katika uhalisia ambao ndiyo mzani wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…