Baba mzazi wa Mchekeshaji Hakika Ruben adai amekata tamaa na mwanaye, asema Dunia ndio itamfunza

Baba mzazi wa Mchekeshaji Hakika Ruben adai amekata tamaa na mwanaye, asema Dunia ndio itamfunza

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
FVD_3.jpg
Baada ya taarifa kuibuka mitandaoni na kusambaa kwa kasi zikimhusisha mchekeshaji Hakika Reuben kuwa anajihusisha na mapenzi ya jinsia moja, kuna mengi kadhaa yameendelea kuzungumzwa na kuacha maswali mengi.

Licha ya kuwa Hakika mwenyewe hajatoka hadharani na kutoa ufafanuzi rasmi kuna mambo kadha wa kadha ambayo yanaweza kukufungua na kukufanya ufahamu kuhusu msanii huyo ambaye aliwahi kunukuliwa akisema yeye pia ni mmiliki wa shule binafsi ya T.Y Primary English Medium iliyopo Mkoani Iringa.

HAKIKA AAMUA KUWA KIMYA
Baada ya skendo hiyo ni kama Hakika ameamua kutokuwa karibu na mitandao ya kijamii au na Wanajamii kwa kuwa moja ya namba ya simu haipatikani, ni kama ameamua kuizima.

Kwenye mitandao ya kijamii amefunga komenti, hali inayoonesha hataki usumbufu au anajua presha itakuwa kubwa kwake.

Katika page yake ya Instagram kwa siku kadhaa amekuwa akiweka Insta Story pasipo kuweka post za kawaida.
Kucha.JPG

Hakika akitengenezwa kucha, amepost kupitia IG Story

BABA YAKE AFUNGUKA
Ruben Ndendya, ni baba mzazi wa msanii huyo ameelezea kuhusu kinachoendelea, anasema:

“Vijana hawa wanaliputa tu mitandaoni, mimi ndiye mmiliki wa shule hiyo, kwa kawaida pale shuleni yeye (Hakika) anafanya kazi kama part time, anatunza documents za Kihasibu.

“Vitu vyake vingi mimi nilishamkatalia, analopoka sana, mara sijaoa mara hivi…. Ana maneno mengi naona mtandaoni wanamshabikia sana, mimi huwa naona ni mambo ya kipuuzi tu.

“Nafasi yake pale shuleni hana ajira ya moja kwa moja, yeye huwa anazunguka na mambo yake muda mwingi.

Taarifa ya Polisi
“Kuhusu hizo tuhuma (mapenzi ya jinsia moja) nimeona Polisi wanachakata, unajua uhuru ukipita kiasi inakuwa tatizo.

“Mimi kama mzazi ninaendelea kuangalia kinachoendelea, kuhusu shuleni hakuna kitu chochote kinachoendelea kibaya na hizo taarifa tunaziona tu mitandaoni lakini hatujatoa tamko lolote kama taasisi.

“Uzuri shule sio ya bweni na yeye hashughuliki na Wanafunzi moja kwa moja kwa kuwa utambulisho wake pale shuleni tunamtambua kama Mhasibu.

“Pia kwa nafasi yangu kama baba na kama Mchungaji hilo suala nimeliacha kwanza, ni mapema kutoa tamko kwa sasa.

“Kuhusu Polisi kuzungumza na Hakika, nimezipata kutoka kwa dada yake ambaye anasema aliambiwa na kaka yake (Hakika) kuhusu taarifa hizo za Polisi.

Mazungumzo baba na mtoto
“Hajaniambia chochote na wala siwezi kuingilia, mimi niwe mkweli nimekata tamaa, shughuli zake sikikubali kabisa, naona tu watu wanamfurahia huko mitandaoni lakini anachokifanya naona hakina mashiko.

“Unajua wanasema ukimuonya mtoto kama asiposikia basi Dunia itamfundisha yenyewe, hawezi kuja kuniambia hayo yanayoendelea kwa kuwa anajua ni mambo ambayo mimi nimekuwa nikiyakataa kwake.”

JESHI LA POLISI
Alipotafutwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi kuhusu suala hilo na kama kweli wamemuhoji Hakika Ruben amesema atafuatilia suala hilo kwa wasaidizi wake wa chini kama kuna ripoti ya aina hiyo na kama ipo apatiwe kwa maandishi ndiyo atatoa taarifa.


Pia soma:

Skendo ya ushoga yamtafuna Hakika Ruben baada ya video zake kuvuja
Nini hatma ya shule anayomiliki Hakika Reuben baada ya video clips zake chafu kuvuja mitandaoni?
 
Kama mzazi akikuonya kwenye haki ukapuuza na ni jambo zito, Mungu huondoa kibali cha ulinzi wake na kuacha nature iamue! Hiyo ndio kufunzwa na ulimwengu.

Amri za Mungu ya 4 inasema waheshimu baba na mama upate MIAKA MINGI na HERI duniani! Hivyo usijaribu kupuuza mzazi na kujiona huhitaji muongozo wao.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Kama mzazi akikuonya kwenye haki ukapuuza na ni jambo zito, Mungu huondoa kibali cha ulinzi wake na kuacha nature iamue! Hiyo ndio kufunzwa na ulimwengu.

Amri za Mungu ya 4 inasema waheshimu baba na mama upate MIAKA MINGI na HERI duniani! Hivyo usijaribu kupuuza mzazi na kujiona huhitaji muongozo wao.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Kwa jinsi mzazi alivyo flow inaonekana kuna mambo hayapo sawa kichwani mwa mtoto.
 
Ahsante kwa taarifa, mzazi alishaamua mambo yake kumuachia mwenyewe...
 
Back
Top Bottom