Red black
JF-Expert Member
- Nov 29, 2019
- 5,962
- 17,648
Mtoto ni wewe unaelia kisa mwanao kakosa mumeacha utoto,hujui uchungu wa mwana
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mtoto ni wewe unaelia kisa mwanao kakosa mumeacha utoto,hujui uchungu wa mwana
Upo sahihi, Biblia inasema, matarajio ya Moyo ni ya anadamu jawabu la ulimi lapatikana kwa baba Mungu...Muda mwingine unaweza kutaka kuwa sawa na wengine au jamii inavyotaka uwe.
Ila Mungu akawa amekuandalia njia yako ili uwe salama na sio njia ambayo jamii inataka upite.
Kuna watu baada ya kuzaa maisha yao yamekuwa ya mateso na majuto mpaka kufa kwao.
sawaMwambie kilamtu hufa na historia yake,kama amekosa mume na atapewa mtoto basi aishi maisha yake
mpuuzi weweMtoto ni wewe unaelia kisa mwanao kakosa mume
Wewe sio baba bora,kama uliruhusu Binti yake azae bila ndoa.......yamkini ndio uliyeruhusu tabia hatarishi za binti yako,.........atolewe bikira,afanye uzinzi,huku ukichekelea,kisha utegenee mwanaume aje kuoa "used item",..........Hayo ni maombi ya mdada mmoja ambae,nilimlea toka akiwa na miaka 3 hadi kumfikisha chuo kikuu,kwa ngazi ya shahada ya uzamili,sasa ana miaka 34,hajazaa,hajaolewa.
Kila akipata mwanaume hafiki nae mbali,japo ni mdada ambae hanywi pombe,havuti sigara,sio mtu wa kutoka out na nimemlea kwa dini ya kikatoliki japo mie ni muislamu,kwani ndio dini ya wazazi wake ambao kwa sasa hawako duniani
Ana kazi yake na kipato japo sio kikubwa.Kasubiri sana kupata mchumba hapati,tunaongea nae sana,nilimuomba padri wake anakosali amuombee,lakini hakuna kitu,alipata wanaume kama 3 hivi na kumbe walikuwa wanamtapeli maana wote wana wake.
Sasa jana kanipigia simu,baba niruhusu tu ni zae bila ndoa, umri unapita,aisee bila kuficha nililia sana,mwishowe nimemwambia sawa,fanya roho yako itakavyokuongoza
Money is not everything!Sio wote Kuna wanawake wanagombewa na wanaume hadi unashangaa nafikiri ni bahati lakini pia atafute hela sana akiwa nazo atapendwa tu na ataolewa Hata kama umri umeenda
Binti yako ana ujasiri sana mm kuongea mambo hayo na mzee huo ujasiri naona kama sijajaaliwa.ni mwanangu,hakuna afanyacho haniambii,nampenda sana na kila siku namuombea mema
inategemea makuzi na utamaduni,mimi ni mchotara,mama ni mtz na baba ni mtu kutoka ulaya so hivyo ndivyo tulivyolelewa,japo huo uchotara wangu sio subject ya mjadala maana hua sipendi kuutajaBinti yako ana ujasiri sana mm kuongea mambo hayo na mzee huo ujasiri naona kama sijajaaliwa.
Ni kweli basi tumuombee Mungu tu mwananguPoleni sana, mambo ya kuoana siku hizi yamekuwa magumu sana. Wapo wanawake wengi ninawafahamu umri unaenda na hawaolewi, mahusiano yapo ila hayadumu. Sisi wanaume tunawakimbia tunakwenda kuona kwingine, hii ni mbaya sana. Unafikia muda inatakiwa uwe na familia lakini huna mara nyingi inaumiza hata ujikaze vipi.
kweliMoney is not everything!
Wapo wenye pesa tunawaona na wana ukame wa kupata wanaume.
unajua wewe ni mjinga usiyejua jambo hili na umelidandia tuWewe sio baba bora,kama uliruhusu Binti yake azae bila ndoa.......yamkini ndio uliyeruhusu tabia hatarishi za binti yako,.........atolewe bikira,afanye uzinzi,huku ukichekelea,kisha utegenee mwanaume aje kuoa "used item",..........
Na ushauri wako ni dhambi kwa mujibi wa uislam
kwamba mwanaume huwa halii? mwanaume huwa analia japo kwa style yake iliyo tofauti na mwananamke. Huwa tunalilia moyoni!Mwanaume uliaje bhana, unazingua
huyo hajui asemalo na hajawahi kukutana na shidakwamba mwanaume huwa halii? mwanaume huwa analia japo kwa style yake iliyo tofauti na mwananamke. Huwa tunalilia moyoni!
JESUS IS LORD&SAVIOR
ndoa Ina heshima yake. Ndio mpango wa Mungu kwa mwanadamu. Tafuta kujua ni nini mapenzi ya Mungu kwako, ili uyafanye. Usidhani kuzaa ni lazima.Kumbe tupo wengi.story yake inafanana na yangu kwa asilimia kubwa. mimi nilipofikisha umri huo nikaamua kuzaa bila ndoa. sasa hivi ni 36 na katoto kangu kana miaka miwili. nina mfurahia sana mtoto wangu sasa napambana kwa ajili yake. na nina amani mambo ya ndoa nilishayaweka kwenye dampo la taka sasa ni kupambana tu na maisha. unaweza subiri ndoa mwisho wa siku umri ukakuacha kabisa ndoa ukakosa na mtoto ukakosa vilevile.
Kasongo ye ye eeMwanaune unajua hadi wanaune aliopita nao binti wa kumlea
Wengi wakifika hapo ikasoma 35 hata anaepumua anaanza kutafutwamiaka 34
tumuombee kwa MunguKuwa baba wa binti ni kazi kubwa sana, machungu yake sio madogo hasa kwa hiki kizazi tunacholea.
Atazaa sawa, at that age tunategemea hawezi kuishi mwenyewe. Ni aibu sana mwanamke 35+ huna stable relationship, anakuja huyu anadumu 1yr, anakuja yule six months, hata stara unakosa.