Baba niruhusu nizae

Baba niruhusu nizae

niacheni jamani niko bize na mtoto wangu. habari za baba yake hazinihusu mtu kama hajui majukumu yake wa nini sasa.
Mkuu, ulimwambia, mkakubaliana uzae atatimiza majukumu halafu hayatimizi au ulibeba mimba mwenyewe kwa malengo yako ya kutokuzeeka bila mtoto?
 
Poleni sana, mambo ya kuoana siku hizi yamekuwa magumu sana. Wapo wanawake wengi ninawafahamu umri unaenda na hawaolewi, mahusiano yapo ila hayadumu. Sisi wanaume tunawakimbia tunakwenda kuona kwingine, hii ni mbaya sana. Unafikia muda inatakiwa uwe na familia lakini huna mara nyingi inaumiza hata ujikaze vipi.
Hivi sasa kinachofanya muwakimbie wanawake ni nini? Tufanye huyo mwanamke ni wife material.
Moja ya sababu inayofanya wadada wengi wasiolewe ni kwasababu wanaomba sana hela, siwaelewagi kwa kweli, sijui wanakua wamejikatia tamaa ya kukutana na mwanaume wa maana Joline Donatila Dadakidoti
Sio wamejikatia tamaa mtu anayaishi malengo yake kwa namna anavyoyatazama maisha. Kama yeye anaamini kuwa hatakiwi kujitafutia bali ni wa kupewa ni ngumu sana kuishi na mtu wa hivyo kama mke sababu maisha kusaidiana . Kazi ni kwako muoaji.
 
Hayo ni maombi ya mdada mmoja ambae,nilimlea toka akiwa na miaka 3 hadi kumfikisha chuo kikuu,kwa ngazi ya shahada ya uzamili,sasa ana miaka 34,hajazaa,hajaolewa.

Kila akipata mwanaume hafiki nae mbali,japo ni mdada ambae hanywi pombe,havuti sigara,sio mtu wa kutoka out na nimemlea kwa dini ya kikatoliki japo mie ni muislamu,kwani ndio dini ya wazazi wake ambao kwa sasa hawako duniani

Ana kazi yake na kipato japo sio kikubwa.Kasubiri sana kupata mchumba hapati,tunaongea nae sana,nilimuomba padri wake anakosali amuombee,lakini hakuna kitu,alipata wanaume kama 3 hivi na kumbe walikuwa wanamtapeli maana wote wana wake.

Sasa jana kanipigia simu,baba niruhusu tu ni zae bila ndoa, umri unapita,aisee bila kuficha nililia sana,mwishowe nimemwambia sawa,fanya roho yako itakavyokuongoza
Naomba uniunganishe nae!! Nani najitaji mwanamke.
 
Kila kiumbe aliyekuja duniani alipangwa aje. so dont be shy kama namba inatembea we zaa usisubiri treni ikakupita. Mchungaji mmoja alikuwa anapiga kelele tumechoka kubatiza watoto wasiotokea kwenye ndoa. nikajichekea tu mwenyewe moyoni namwambia mbona hili ni trela but in 5 year to come hii itakuwa ni norm. maana wadada wenye 28 to 40 ambao hawatakuja kuolewa ni wengi aisee na no wazuri tu. unadhani watakubali saa iyoyome bila kuwa na mtoto Big No! so wachungaji wawe wapole tu wapokee viumbe hawa wa Mungu wasio na hatia
 
Kumbe tupo wengi.story yake inafanana na yangu kwa asilimia kubwa. mimi nilipofikisha umri huo nikaamua kuzaa bila ndoa. sasa hivi ni 36 na katoto kangu kana miaka miwili. nina mfurahia sana mtoto wangu sasa napambana kwa ajili yake. na nina amani mambo ya ndoa nilishayaweka kwenye dampo la taka sasa ni kupambana tu na maisha. unaweza subiri ndoa mwisho wa siku umri ukakuacha kabisa ndoa ukakosa na mtoto ukakosa vilevile.
Poleni ila ndoa tamu asikwambie mtu,
 
Back
Top Bottom