Baba niruhusu nizae

Baba niruhusu nizae

Moja ya tatizo kubwa la binadamu ni kutafuta dosari kwenye kila kitu,basi tambua yafuatayo:
1.mimi ni suriyama wazazi wangu mmoja alikuwa mtanzania na mwingine anatokea ulaya na makuzi yetu,tumelelewa kwa tamaduni mbili
2.huyo mwanangu hakuwa anachagua watu wenye kipato na ndio maana kaamua kuzaa ni mtu ambae uwezo wake ni mdogo sana
3.ukaribu wangu na mwanangu una mipaka,sio kwamba namtawala au namregulate,la niko nae karibu sana lakini with limitations
4.japo amesoma vizuri lakini ni mwanamke mwenye heshima na nidhamu ya juu sana na namjivunia sana
Mkuu, unajua wazazi kuna upande wa watoto wao huwa hawauju kabisa. Mfano mimi mwenyewe wazazi wangu wanaamini kabisa kijana wao nimenyooka vibaya mno. Hii ni kwa sababu kuna upande wangu wa pili huwa siwaoneshi wao. Ila siku wakiujua ndio watajua mm nipoje.

Sasa mkuu kwa maelezo yako inaonekana hakuna shida upande wako wala hakuna shida upande wa binti, basi tuseme ni dunia imeamua kumfanyia hivyo na si kingine. Kwa maana nyingine yanayomkuta yapo nje ya uwezo wa binadamu, hivyo hatuna cha kurekebisha bali ni kuacha iwe hivyo.

Kila la heri mkuu
 
Hayo ni maombi ya mdada mmoja ambae,nilimlea toka akiwa na miaka 3 hadi kumfikisha chuo kikuu,kwa ngazi ya shahada ya uzamili,sasa ana miaka 34,hajazaa,hajaolewa.

Kila akipata mwanaume hafiki nae mbali,japo ni mdada ambae hanywi pombe,havuti sigara,sio mtu wa kutoka out na nimemlea kwa dini ya kikatoliki japo mie ni muislamu,kwani ndio dini ya wazazi wake ambao kwa sasa hawako duniani

Ana kazi yake na kipato japo sio kikubwa.Kasubiri sana kupata mchumba hapati,tunaongea nae sana,nilimuomba padri wake anakosali amuombee,lakini hakuna kitu,alipata wanaume kama 3 hivi na kumbe walikuwa wanamtapeli maana wote wana wake.

Sasa jana kanipigia simu,baba niruhusu tu ni zae bila ndoa, umri unapita,aisee bila kuficha nililia sana,mwishowe nimemwambia sawa,fanya roho yako itakavyokuongoza
As a father najua unacho feel, pole ndo ukubwa. Katika watu wanaoteseka ni wanawake kuhusu ndoa tena akiwa anatoka familia ina kauwezo ka kumlisha, huwa wanachagua wanaume na kizazi hiki kama unavyoona kina ujinga mwingi pia vijana waoga wa kuanzisha famikia mana wanatishwa. Mruhusu sometime sio kila fungu analoomba apate.
 
Kuolewa na kuoa sio lazima, ni hiyari.

Huyo dada Atafute bwana Azae, maana ndo hitaji lake kwa sasa.
Lol
 
Ndo hivyo ndugu yangu dunia hii haijawahi kuwa na usawa unaepata hili anakosa lile. ila bado watu hataacha kukunyoshea kidole utafikiri wao hawana makosa. kikubwa ni kutokuwajali na kufanya kile unaamini.
no one perfect
 
Kumbe tupo wengi.story yake inafanana na yangu kwa asilimia kubwa. mimi nilipofikisha umri huo nikaamua kuzaa bila ndoa. sasa hivi ni 36 na katoto kangu kana miaka miwili. nina mfurahia sana mtoto wangu sasa napambana kwa ajili yake. na nina amani mambo ya ndoa nilishayaweka kwenye dampo la taka sasa ni kupambana tu na maisha. unaweza subiri ndoa mwisho wa siku umri ukakuacha kabisa ndoa ukakosa na mtoto ukakosa vilevile.
Njoo basi tuzae mwengine.
Nitakupa mapacha..!!!

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
sitaki kuolewa na kitunguu maji. kile hivi mtu hajui maisha nini si kwamba ni mtoto mdogo ni mtu mzima na hana familia wala mtoto ila majukumu hataki wa nini sasa.
Ulijitombesha kwake ili iweje, pambania kombe
 
Toka dunia iumbwe Wanawake ni wengi kuliko Wanaume,cha ajabu kuna mifumo iliibuko hapo ya mke moja na mwanaume moja imeharibu kila kitu.
Ingekuwa zamani,asingekosa Mume.
 
Hahaha..........kuweni na huruma na Wazee, si mnajua hela yetu ya mauzo ya Tumbaku yametoka 🤗

Fanyeni mje ili mtusaidie kuzihesabu😜
Babu naomba hela🤪🤪😋😋😋
 
Hayo ni maombi ya mdada mmoja ambae,nilimlea toka akiwa na miaka 3 hadi kumfikisha chuo kikuu,kwa ngazi ya shahada ya uzamili,sasa ana miaka 34,hajazaa,hajaolewa.

Kila akipata mwanaume hafiki nae mbali,japo ni mdada ambae hanywi pombe,havuti sigara,sio mtu wa kutoka out na nimemlea kwa dini ya kikatoliki japo mie ni muislamu,kwani ndio dini ya wazazi wake ambao kwa sasa hawako duniani

Ana kazi yake na kipato japo sio kikubwa.Kasubiri sana kupata mchumba hapati,tunaongea nae sana,nilimuomba padri wake anakosali amuombee,lakini hakuna kitu,alipata wanaume kama 3 hivi na kumbe walikuwa wanamtapeli maana wote wana wake.

Sasa jana kanipigia simu,baba niruhusu tu ni zae bila ndoa, umri unapita,aisee bila kuficha nililia sana,mwishowe nimemwambia sawa,fanya roho yako itakavyokuongoza
Pole zake. Kuna kitu hakipo sawa, wapo watumishi wa Mungu wanaweza msaidia
 
Back
Top Bottom