Hayo ni maombi ya mdada mmoja ambae,nilimlea toka akiwa na miaka 3 hadi kumfikisha chuo kikuu,kwa ngazi ya shahada ya uzamili,sasa ana miaka 34,hajazaa,hajaolewa.
Kila akipata mwanaume hafiki nae mbali,japo ni mdada ambae hanywi pombe,havuti sigara,sio mtu wa kutoka out na nimemlea kwa dini ya kikatoliki japo mie ni muislamu,kwani ndio dini ya wazazi wake ambao kwa sasa hawako duniani
Ana kazi yake na kipato japo sio kikubwa.Kasubiri sana kupata mchumba hapati,tunaongea nae sana,nilimuomba padri wake anakosali amuombee,lakini hakuna kitu,alipata wanaume kama 3 hivi na kumbe walikuwa wanamtapeli maana wote wana wake.
Sasa jana kanipigia simu,baba niruhusu tu ni zae bila ndoa, umri unapita,aisee bila kuficha nililia sana,mwishowe nimemwambia sawa,fanya roho yako itakavyokuongoza