Kelele misikitini sio mamlaka, inatusumbua wengine tusio amini kama wao. Sina tatizo na mamlaka yao, naomba utulivu nikiwa kwangu.Ujumbe wenyewe ni huu hapa....
Tiini mamlaka...BWANA ASEMA!
Hakika...Nina maana hii kuwa;
Hawataweza kuzuia wala kuzifungia imani wala ibada za watu. Wao ndio watafungwa na kufungiwa kwenye mateso..
Mungu wa mbinguni lazima ataabudiwa tu na kila ulimi utakiri kuwa yeye ni Mungu Yehova na ni Bwana wa wote wenye mwili na kila goti lazima litapigwa mbele yake
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Umemjua wakati mwenzio ananyea debe wewe upo na familia yako mnatizama tv huku ukiendelea kubofya bofya smartphone yako?
Kweli si Rwanda...Kwanza hapa siyo Rwanda, pili matusi yako hayana mashiko, tatu Serikali ya Samia haitafanikiwa kwenye hili jambo na mwisho huyo jamaa atashinda rufaa yake.
Una haki hiyo....Kelele misikitini sio mamlaka, inatusumbua wengine tusio amini kama wao. Sina tatizo na mamlaka yao, naomba utulivu nikiwa kwangu.
Nilijaribu nikaambiwa mimi na wenzangu ni wachochezi. Tulianza ngazi ya serikali ya mtaa, tukajaribu wilaya, tulijaribu mkoa enzi za Makonda, na tumejaribu Taifa NEMC tumeshindwa, hakuna anayetaka kupoteza chakula cha wana.Una haki hiyo....
Fuata utaratibu ili wasiendelee kukukera na kukupoka haki yako ya kiraia.....
Kelele ni "disturbance"...Nilijaribu nikaambiwa mimi na wenzangu ni wachochezi. Tulianza ngazi ya serikali ya mtaa, tukajaribu wilaya, tulijaribu mkoa enzi za Makonda, na tumejaribu Taifa NEMC tumeshindwa, hakuna anayetaka kupoteza chakula cha wana.
Wanaliona ila walisema ni gumu kwao sasa hatufahamu tutaishi na hali hii mpaka lini.Kelele ni "disturbance"...
NEMC wasipoliona hili.....
Hiiiiiiii bagoshaaa
Kimsingi, ni kweli Mbarikiwa alikuwa ana changamoto ya kiakili na alikuwa anaishambulia na kujifanya mbabe dhidi ya serikali na ndio maana wamemfunga ila sio kwa kosa hilo la kutosajili Huduma.Tukitoka hapo tuanze kuangalia na misikiti ya Ijumaa. Maana kila mtaa inaota km uyoga tena bila vibali.
Serikali kwa kesi hiyo imekosea ni bora wangetafuta kosa lingine.
Maana makanisa na misikiti kila baada ya nyumba wanapiga kelele na hawana vibali.
Vp kuhusu mfalme Zumaridi, mbona hakufungwa?
Nabii Tito je?
Maana wote hao hawakuwa na vibari na ilisibitishwa baada ya kukamatwa.
Hapo issue sio kanisa, issue ni Mbarikiwa Personal na kukashfu dola huku akijifanya kupambana na dola ndio kilichomfunga. Hakuna mtumishi anayeefungwa kwa kosa la kutosajili huduma mkuu. Kama hujasajili, hufungwa huduma na sio mtu.Huku mkoa wa pwani yako makanisa uchwara mengi yasiyo hata na kibali Cha balozi mbona haziguswi?
Madhehebu ya kishenzi yanafahamika, mengi ni haya ya walokoleUkiipa serikali mamlaka ya kudhibiti madhehebu unayoyaita ya kishenzi, halafu serikali ikasema hizi dini zote ni ushenzi wa kigeni, makanisa yote na misikiti yote ni ukoloni wa kiutamaduni, futa yote, kuanzia leo marufuku.
Utakubali? Utafurahia?
Serikali inaweza wala usilete ngonjera zako hapa. Unawalinganisha hawa washenzi na crusaders wakati wa byzantine era? You are wrong on that na hujamuelewa kabisa huyo anayeitwa Mbarikiwa. Mbarikiwa ni mental case and unfortunately anajenga cult yake.Mkuu,
Hata hao kina Mackenzie na Kibwetere kama kweli ni washenzi tu cult leaders, njia ya kuwadhibiti ni kuwaelimisha wananchi wajue kuchambua wenyewe mbivu na mbichi.
Unaweza kutandika busati dunia nzima ili mguu wako usikanyage mchanga wa ardhi, au unaweza kuvaa viatu tu na ukafikia lengo lile lile, wewe unataka kutandika busati dunia nzima badala ya kuvaa viatu tu.
Ukiwafunga na kuwanyima vibali hawa wachungaji unawazidishia umaarufu tu, wanakuweka katika narrative yao kwamba hata Biblia ilitabiri kutakuja mpinga Kristo, na hii serikali inayowafungia ndiyo mkono wa huyo mpinga Kristo.
Tushaanza kuona hayo maneno hata kwenye thread hii tayari.
Dini ina nguvu sana, walioweka sheria za kuheshimu uhuru wa ibada hawakuwa wajinga. Waliona mengi sana.
Yani kifupi kuwafungia ndiyo kutakuwa kunawazidishia umaarufu, na ukifanya hivyo watatumia huruma ya watu kujipatia wafuasi zaidi. Wataenda underground usiwaone kabisa.
Kumbuka Ukristo ulianzia underground enzi za Warumi, umesha survive government persecution, unajua kutambaa chinichini sana. Utakachofanya ni kuwafanya waende underground usijue kabisa wanafanya nini.
Serikali inajikuta katika litu kinaitwa "The Law of Unintended Consequences".
Katika jitihada za kuwazima, ndiyo inawaongezea umaarufu.
Halafu watakuwa wanakutana kisiri, wanafanya mambo yao.
Weka ushahidi hapa unao onyesha DG TISS alimuua mwanayeKwani kuua mpaka ushike panga? Hata kuagiz tu nayo ni kuua.
Aaaaaah Mudi nawe una visa
Hilo kanisa analomiliki bila vibali ndilo anaeneza itikadi ya chuki. Kwa hiyo amehukumiwa kumiliki kanisa kinyume na sheria za Serikali. Unataka tujadili nini zaidi?Kwani kafungwa kwa kosa gani mkuu?
Km ni kuzusha uongo kesi ingekuwa ni hiyo.
Ila kosa lililompeleka jela ni kumiliki kanisa bila vibali.
Tujadili hilo sio hisia zako
Kweli kabisaHili halina ubishi wowote kuwa wamemwonea huyu mchungaji...
Wametumia kigezo cha "kanisa kutokuwa na usajili" ili kumfunga lakini nyuma ya pazia ni chuki za "wakubwa" tu ndani ya serikali kwa mtu huyu kwa sababu jamaa huwa anausema uovu na madhambi yao hadharani mchana kweupe bila kupepesa macho!
Nyuma ya huu mgogoro na kumfunga jela Mch. Mbarikiwa Mwakipesile, yupo Dr Tulia Ackson (Spika wa Bunge la JMT) na ndiye anaye dictate kila kitu huku polisi na baadhi ya maafisa wa TISS wakiongozwa na RSO wa Mbeya wakiwa kama mbwa tu wa kuambiwa uma hapo, acha pale....
Kama ni ishu ya usajili wa taasisi za kiimani na kidini zinazoendesha shughuli zao za kiimani na ibada, basi ziko nyingi sana kwa mamia ambazo ziko kienyeji tu zimezagaa nchi nzima zikiendelea na shughuli zao
Nonsense, mnachuja mbu mnameza ngamia. Watembea uchi, waimbaji wa matusi na ngono hamuwakamati, majizi na mabadhilifu hamkamati. Mungu wao yu hai, atawatetea.Wale wanaohubiri masokoni na stendi na kwenye mabasi waache mara moja. Rungu hili litawashukia.