Ni lazima ujibiwe, Uislamu wako ni bora kuliko utanzania wako? Kama babu zako walikua na aina hii ya fikra sintoshangaa ni kwanini haw Abdulakuandikwa katika historia ya Tanganyika, Inaonekana wazi walipanga kujinufaisha wao binafsi na kuleta u dini hapa nchini.
Masta...
Hujui historia ya uandishi wa historia ya uhuru wa Tanganyika na nini ilikuwa sababu ya wazee wangu kufutwa.
Nitakusomesha kidogo ili ujue usiwe unajadili jambo hulijui.
Matatizo ya kuandika histori hii yalianza mwaka wa 1962 TANU yenyewe ilipoamua kuandika historia yake na waandishi wa mradi huu wa historia walikuwa Abdul Sykes na Dr. Wilbard Kleruu.
Historia hii ilianza na Kleist Sykes 1929 na ilikuwa imeshaandikwa na Kleist kabla hajafa mwaka wa 1949.
Mswada huu alikuwanao Abdul Sykes na sasa uko katika kitabu na nakala halisi Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (Daisy Sykes Buruku, ''The Townsman: Kleist Sykesí, katika Iliffe (ed) Modern Tanzanians, Nairobi, 1973, uk. 95-114. Angalia A.D. Sykes ''The Life of Kleist Sykes,'' University of Dar es Salaam Ref. No. JAN/HIST/143/15).
Kuna watu hawakupenda historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika ianze na ukoo wa Sykes.
Abdul Sykes akajitoa katika ule mradi.
Mwaka wa 1963 Judith Listowel alikuja Dar es Salaam kuafanya utafiti wa historia ya Tanganyika na mwenyeji wake alikuwa Ally Sykes.
Listowel aliandika kitabu, ''The Making of Tanganyika,'' (1965).
Kitabu hiki kimeeleza mengi kwa ukweli wake.
Mwalimu amelalamika kuhusu hiki kitabu na alimwandikia Listowel kumfahamisha hisia zake.
Yako mengi sana lakini nadhani haya yanatosha kwa kukufahamisha tatizo la uandishi wa historia ya uhuru wa Tanganyika na wazee wangu hawahusiki na lolote katika matatizo haya ya kuandika historia ya TANU.