Baba wa Taifa na tatizo la Udini

Allah uwahifadhi waja wake.Bila shaka atakuwa mahali salama.
 
Umekuwa kimya maana tukiuliza maswali unajibu kwa picha.
Mtoa mada ukienda kinyume nae Hana majibu.
Ila stori kama hizi ndo ulikuwa unazihitaj.Enjoy now

Sent from my TECNO CD7 using JamiiForums mobile app
 
Hatari hizi zote hawa watu wanagoma kuzipokea kwa sababu ya chuki zao tu.Lakini wakati utafika na kila kitu kitakuwa wazi.
 
Umekuwa kimya maana tukiuliza maswali unajibu kwa picha.
Mtoa mada ukienda kinyume nae Hana majibu.
Ila stori kama hizi ndo ulikuwa unazihitaj.Enjoy now

Sent from my TECNO CD7 using JamiiForums mobile app
Day ...
Najitahidi kujibu kila swali na picha naweka kukazia maelezo.

Kwani picha inasema maneno 1000.
Wasomaji wengi nimewavutia kwa ajili ya hii Maktaba yangu ya picha .

Waingereza wana msemo, "Seeing is believing."
Kuona ndiyo kuamini.
 
Yamekuingia. Ukweli siku zote huwa mchungu.

Dini yake, wewe inakuhusu nini hata uumie?
 
Ni kenge mwenye roho ya kibaguzi kama wewe unaumia mpaka leo unapoona ni wahindi na waarabu ndio wenye hela nchi hii, lakini hujui pia ndio wapo waliomchangia huyo Nyerere katika pilika zake za kudai uhuru.
Zee zima mvi mpaka utopoloni, lakini bado akili ya kibaguzi kuona hata wale waliojitolea kudai uhuru hawastahili kuwa watanzania kwa kuwa wana asili ya afrika kusini...Kenge wewe endelea kula kipensheni chako za CCM ambacho hata hakitoshelezi kwenda choo kila siku....
 
Day ...
Najitahidi kujibu kila swali na picha naweka kukazia maelezo.

Kwani picha inasema maneno 1000.
Wasomaji wengi nimewavutia kwa ajili ya hii Maktaba yangu ya picha .

Waingereza wana msemo, "Seeing is believing."
Kuona ndiyo kuamini.
Ni Baki tu kuamini mada hii ulikuwa na lengo Mfu

Sent from my TECNO CD7 using JamiiForums mobile app
 
Yani rais akishakuwa muislam hizi mada za kijingajinga huwa zinakuwa nyingi sana. Akili mnaweka wapi? embu kafanye kazi acha kulalama vitu vya kusadikika. Umaskini na ujinga wako unao mwenyewe na uwezo wa kuutoa ni wewe mwenyewe na sio dini wala imani yako. Over.
 
Pale tunapoacha vigezo vya msingi katika utendaji na kukimbilia dini tunaenda kuua taifa. Nchi yetu haina dini, bali watu wake. Imani, kwa maana yoyote ile, isiwe kigezo cha utumishi kwenye taifa. Kwa muktadha huu, tusiache kujadili ndugu zetu wa-hindu, hawa tumewabagua zaidi. Mwisho, mzee wangu imani ya dini ni chombo cha kumsaidia binadamu ili amfikie Mungu wake, sasa wewe unataka kutumia imani kustahilisha mambo ya kidunia. Embu, tafakari malengo mahususi ya imani yako alafu utathmini fikra zako katika hicho unachodhani ni elimu unayoitoa.
 
Mixo...
Hii ni makala yangu ya tatu.
Naamini umezisoma mbili zilizotangulia.

Haya mambo yanetokea miaka 9 iliyopita:

MADINA YAKATAZWA KUWA SEHEMU YA MAKAZI KWA AMRI YA MKUU WA MKOA TANGA CHIKU GALAWA a

Nyaraka zimefika Dar es Salaam zinazoonyesha kuwa wakazi wa Madina kijiji kilichovamiwa kwa kisingizio kuwa kilikuwa na uhusiano na Al Shabab wamelazimishwa kuweka sahihi makubaliano kati yao na uongozi wa kata ya Negero kuhama eneo hilo kwa kuwa haparuhusiwi kuishi watu.

Kutokana na nyaraka hizo amri hiyo imetoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa.

Nyaraka inaonyesha kuwa waliotilishwa sahihi amri hiyo ya kuondoshwa Madina ni Muhamadi Mwandalo na Salimu Mwalimu na viongozi waliotia sahihi kwa niaba ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi Ofisi ya Afisa Mtendaji Kata ya Negero ni Paul A. Mnyeke na Ramadhani A. Mwamilinga.

Nyaraka ina muhuri wa Afisa Mtendaji Kata Negero.

Makubaliano hayo yanasema wanakijiji hao wamepewa siku 10 kuishi Madina kuanzia tarehe 19 hadi 24 Desemba 2013 wawe wameshaondoka Madina na wamevunja nyumba zao na kuondoa vifaa vyao.

Makubaliano hayo yanataka nyumba ziwe zimevunjwa ingawa nyumba zilishavunjwa siku nyingi na vifaa vya wanakijiji hao kupotea katika uvamizi ule.

Makubaliano hayo nyaraka inaonesha yalifanywa tarehe 17 Desemba 2013.
Manazi wa Kijerumani waliwafanyia dhulma mfano wa hii Wayahudi wakati wa Vita Kuu Vya Dunia.

Wanasheria wanaweza kusaidia katika dhulma hii.
Kuna wanavijiji waliondoka Madina zamani kwa sababu mbalimbali.

Kijiji kiliposhambuliwa na kesi kufunguliwa dhidi ya Waislam Mahakama ya Handeni wakazi hawa waliohama walikuwa kimya na walipozungumza walitoa picha iliyokuwa wakati mwingine inamtisha msikilizaji.

Taratibu baada ya kusikia kuwa nyumba zimevunjwa na kuchoma moto na ardhi zao sasa wananyang'anywa wameanza kuhaha kutaka kujua kulikoni.

Wanazungumza kuhusu mali zao na mashamba yao na viwanja vyao na ardhi zao.

Kubwa sana na hili wengi hawakuwa wanalijua wanazungumza kuhusu machimbo ya dhahabu huko Madina...waliyokuwa wakimiliki kihalali na nyaraza za umiliki wanazo...

Halikadhalika tumepokea hapa ujumbe mkali kuwa hawa Waislam wa Madina hawastahili kuhurumiwa na kutetewa...

Jibu limekuwa wanastahili kuhurumiwa na kutetewa kwani hata kama tujaaliwe walikuwa katika makosa hapakuwa na sababu ya kuuliwa na nyumba na misikiti yao kuchomwa moto.

Ilikuwa hawa ''wakosaji'' wakamatwe wapelekwe mahakamani.

Anaetaka kujua zaidi kuhusu hili na atembelee Ubao.

Ukurasa huu uko wazi kusikiliza yanayoanza kujitokeza kutoka Madina.
 
Historia ya nchi hii inatakiwa itazamwe upya kwa nia ya kuondoa upotoshaji mwingi uliyopo ambao umepelekea watu wengi waliopigania uhuru wa Tanganyika kutokujulikana.
 
Historia ya nchi hii inatakiwa itazamwe upya kwa nia ya kuondoa upotoshaji mwingi uliyopo ambao umepelekea watu wengi waliopigania uhuru wa Tanganyika kutokujulikana.
Imeloa,
Kilipotoka kitabu cha Abdul Sykes mwaka wa 1998 kila aliyekisoma alishangazwa na aliyoyakuta ndani.

Kitabu kimependwa sana kwani watu walikuwa wanaisoma upya historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
 
Imeloa,
Kilipotoka kitabu cha Abdul Sykes mwaka wa 1998 kila aliyekisoma alishangazwa na aliyoyakuta ndani.

Kitabu kimependwa sana kwani watu walikuwa wanaisoma upya historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Hii tabia ya kupotosha mambo muhimu ya nchi inafanywa na Ccm kwa lengo la kuwapa sifa za uongo viongozi wao wa juu hasa yule anayeshika mamlaka ya urais.

Tulipoanza shule mwanzoni kabisa ya miaka ya sabini tulikaririshwa mashuleni kwamba Nyerere ndiye aliyeleta uhuru na watu walifanywa wamwabudu kabisa kama vile asingekuwepo Tanganyika isingepata huo uhuru.

Kumbe swala la uhuru ni mkakati ulioanzishwa wakati huyo Nyerere akiwa bado mtoto mdogo kabisa na yeye alikuja tu kudandia train ya uhuru baadaye sana jambo ambalo limefanywa siri na watawala.

Historia ya Tanganyika na baadaye Tanzania inatakiwa iandikwe upya kwa kuzingatia ukweli na kuachana na propaganda na porojo zisizo na maana zinazolenga kuwapa watu wengine sifa wasiostahili.
 
hii hapa kitaalam inaitwa akili kubwa kuijibu akil ndogo. Mzee yan nakuelewa sana yan huo mwaka upo Egypt weng wapo mikoan kwao mwenye gar ni mkuu wa mkoa na waarabu na wahind wachache enz za Bedford
asome vitab hivyo ataelewa???
mzee wangu anaenda gulf Oman mwaka 1990 karibu kata nzima ilijua na barua tu sim ghali enzi hizo.
nikirithi magazet ya sani, vitabu vya Joram Kiango Msako wa Jambazi
Star wars, The ThirdReich,James HadleyChase,
Ustadh una nondo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu una uwezo mkubwa ktk kujenga hoja,hapo nakupa saluti kuubwa.Ushauri wangu jikite kwenye weledi achana na mambo ya kuangalia ktk mitizamo ya kidini.Unakoelekea sasa utaanza kuhoji hata timu ya taifa ina waislam wangapi badala ya kuangalia uwezo,maadili,maarifa...Kama ulivyonishauri niachane na mambo ya Misri basi hebu nawe jiulize ni wakristo wangapi waliopo serikalini kwenye teuzi SMZ?Kwani uliambiwa teuzi zinafanyika ktk misingi ya uwiano kidini?Mbona hujawai kuhoji kwanini waislam wana vyuo na shule chache?
 
Hata mi nashangaa sana, siyo lazima nduguzanguni waislamu muajiliwe serikalini, [emoji23],kazi zipo nyingi sana, kilimo, ujenzi majumba, barabara,
Hata mpira kucheza nayo kazi nduguzanguni
 
Asante ningependa sana kupata majibu ya hoja zangu kwa sababu sijauliza ili nisifiwe bali nimeuliza ili nijibiwe

Nina imani nitajifunza tu kwenye majawabu yako mzee wangu
Political marginalization means that some groups of people are not able to PARTICIPATE democratically in the DECISIONS MAKING PROCESS
 

KUKATOKEA MALALAMIKO KUWA ZOEZI HILO LINA SURA YA UBAGUZI NA WAATHIRIKA NI WAISLAM

Nayakumbuka mambo matatu kama mifano mnasaba wa uzi huu:

1. Bodi Taifa ya Parole hapa nchini iliteuliwa na Frederick Tluway Sumaye aliyekua Waziri Mkuu wakati wa Urais wa Marehemu Benjamin Mkapa.

Sumaye aliteuwa wajumbe wote wa bodi wa imani moja bika kuwepo Muislam hata mmoja.

Miongoni mwao walikuwepo padri mmoja na mchungaji mmoja.

Alipoulizwa kwa nini kafanya hivyo akajibu kwa ukali sana kwamba watu waache kupanda mbegu za udini maana hatukukelewa hivyo na Mwalimu Nyerere.

Uteuzi uliofanyika ulizingatia ''merits,'' za walioteuliwa.

Siku chache baadae Marehemu Mzee Mkapa akatengua uteuzi wa bodi nzima na akaagiza iundwe upya kwa kuzingatia uwiano wa kijamii kama maeneo wanapotoka wajumbe na pia uwiano wa imani za watu kwa maana ya dini.

2. Professor mmoja wa UDOM aliyekua VC alipata malalamiko kuhusu baadhi ya watu kutotendewa haki kwenye ''admission.''

Wakati huo TCU ilikua haijaundwa.

Alipoamua kuitisha ''applications'' zote akakutana na maajabu. Kuna zaidi ya ''applicants'' 350 walikua wameachwa huku wakiwa wame ''qualify'' huku kukiwa na idadi ya kutosha kabisa wakiwa wamepata ''admission'' wengine wakiwa ''below cut-off point'' ya chuo.

Kwa “sudfa” au ''coincidence'' wote waliokua wameachwa kwa dhulma walikua na majina ya Kiislamu na wote walioku ''admitted'' walikua na majina ya Kikristo.

VC akatoa ''order'' mchakato urudiwe tena japo jambo hilo lilikua ''down played.''

3. Miaka ya karibuni kulikua na zoezi la kuwaondoa waalimu wa masomo ya arts sekondari waajiriwa wa serikali kuwarudisha shule za msingi. Zoezi husika halikuwahusu waalimu wa masomo ya sayansi na hesabu

Nilikua mkoa fulani kipindi zoezi hili linaendelea.

Kukatokea malalamiko kua zoezi hilo lina sura ya ubaguzi na waathirika ni Waislamu.

Ofisa mmoja Muislamu katika idara ya elimu ambaye hapo awali alikua amejaribu kuomba uhamisho kwenda mkoa mwingine kwa zaidi ya miaka miwili bila mafanikio alipokea malalamiko hayo na baada ya kujiridhisha ni ''genuine'' akayapeleka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri.

Kikaitwa kikao kati ya Mkurugenzi, Afisa Elimu, Afisa Elimu Taaluma, Ofisa Utumishi na yule ofisa aliyeipeleka ''issue'' kwa Mkurugenzi.

Wahusika wote kasoro yule aliyepeleka malalamiko walikua Wakristo na ilivyoonekana baada ya kikao kuanza ni kutaka kum ''pin'' huyo ofisa kwa nini analeta udini kwenye utendaji wa kazi za Halmashauri na hususan hilo zoezi la kitaifa.

Walianza kumpa maneno makali kabda hata hawajamuuliza kuhusu ushahidi.
Walipomuuliza atoe ushahidi wa madai yake akaoonyesha majina wa wahusika waliohamishwa.

Shule ina waalimu 68 kati yao Waislamu 18.
Waalimu wanaotakiwa kupelekwa primary schools ni 21.

Basi wakaondolewa wale wote 18 wenye majina ya Kiislamu na hao wengine 3 wasiokua Waislamu.

Kikao bado kikasema huo sio ushahidi maana Mkuu wa Kituo (Headmaster) ana ''discretion'' ya kuchagua mradi anafata ''secular'' iliyotolewa na Wizara (TAMISEMI).

Ndipo akaangusha bomu la''Atomic'' ambalo alikua hajawaambia ''before. Kwamba katika wale waalimu Waislamu 18 watatu ni wa Mathematics na sita ni wa masomo mengine ya sayansi na akawaonyesha.

Kikao hakikuendelea.

Mkurugenzi akamwambia Afisa Elimu akarekebishe hilo tatizo.

Wiki hiyo hiyo yule Afisa akapata barua ya uhamisho aliouomba kwa miaka miwili bila mafanikio.
 
Hata mi nashangaa sana, siyo lazima nduguzanguni waislamu muajiliwe serikalini, [emoji23],kazi zipo nyingi sana, kilimo, ujenzi majumba, barabara,
Hata mpira kucheza nayo kazi nduguzanguni
"Muajiriwe."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…