Baba wa Taifa na tatizo la Udini

Makaveli...
Kinauzwa Ibn Hazm Media Centre Msikti wa Manyama, Mtoro na Mtambani.

Pia unaweza kukipata Soma Bookshop na Elite Bookshop Mbezi Samaki shs. 10,000.00.

Kipo kwa Kiswahili na Kiingereza.
Shukrani mzee wangu.
 
Pep,
Mwalimu angeacha misingi mizuri leo tusingejikuta kwanza tunaandika upya historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Pili tusingekuwa na mjadala huu uliotukutanisha hapa.
Nafikiri sababu kubwa ni Geography na ukoloni, maeneo ambayo mkoloni alikuwa analima au kupata malighafi alijenga shule nyingi na aliwafanya wengi wa eneo hilo kwa wakristu, kwa hiyo wasomi wengi walikuwa wakristu hata baada ya uhuru na ndio hao walikuja kushika nchi, waislam nafikiri hawakupata Elimu kama wenzao kwa hiyo ikawa ngumu kushindana kupata hizo nafasi za utawala, lakini sasa naamini hatuna hilo tatizo ni juhudi yako tuu na hata maraisi wetu ni waislam na wakristu bila matatizo
 
Kong...
Tatizo si hilo.
Uhuru ulikuja na changamoto zake.

Nimeeleza yaliyotokea baada ya uhuru katika sehemu ya tatu na ya mwisho ya kitabu cha Abdul Sykes.

Hayo ndiyo yaliyotufikisha hapa.

Watafiti wengine wameeleza tatizo hili mfano wa Bergen (1981), Sivalon (1992) na Njozi (2002).
 

Shida yako kubwa ni kutaka waislamu wapewe special status Tanzania, kwa sababu ambazo kusema kweli hazina mashiko kabisa. Kila unapomuongelea baba wa Taifa, unaona kama hakufanya haki kuwapa waliokuwa waislamu katika kudai uhuru special favors.
Unalopigania kusema kweli hutalipata duniani na wala mbinguni maana lina lengo la kutugawa watanzania bila sababu
 
Tangawizi,
Soma kwa utulivu utaelewa kuwa ninachozungumza ni kuwa kuna tatizo serikali wanalikwepa toka enzi ya Mwalimu.

Hakuna popote nilipozungumza kuhusu, "special status," kwa Waislam.

Unadhani hii 20:80 ni sawa?

Ukishakuwa na hali hii tayari serikali yenyewe ishawagawa raia wake katika matabaka makubwa mawili.
 
Boss hii 20:80 ni nini? fafanua kidogo
 
Kwani mkuu si kazi zinatangazwa watu wanaomba na wanafanyiwa usahili ama ni hizi za kuteuliwa.
Yaani hata Kama wamefaulu wote waislamu wachukuliwe ,mana kigezo sio dini kukaa pale.
Mwishowe tutakuja mpaka darasani tutaanza kuona ratio ni ndogo so itabidi wawe wanabebwa kisa wao wapo wachache.
Kama vipi tuanze kucheki kila kabila liwe katika kila ofisi mkuu.
Tukikuta watu wame qualify hata watano Kati ya 20 position afu wote ni wamwera watolewe wawekwe wamang'ati ama wabarbaig
 
Boss hii 20:80 ni nini? fafanua kidogo

Kei...
Unaandika hivi kwa kuwa hujui tatizo lilipo.
Sikulaumu.

Ili kujua tatizo lilipo inahitaji usome historia ya tatizo hili wapi lilikotokea.
Chanzo ni ukoloni.

Wakati wa kupigania uhuru Waislam walijitolea sana kupita kiasi na katika azma yao ilikuwa kuondoa dhulma ambayo wamishionari na serikali ilikuwa inawafanyia kubwa kuwanyima elimu.

Elimu ikitolewa kwa ubaguzi wa dini.

Waislam waliamini uhuru ukipatikana na kwa kuw wao ndiyo walikuwa mstari wa mbele dhulma hii itaondolewa.

Rejea nyuma msikilize Mwalimu alisema nini katika Hotoba yake ya Jamhuri ndani ya Bunge mwaka wa 1962 na alisema nini alipoacha urais mwaka wa 1985.

Naamini utaelewa.
Lau ikiwa bado rejea tena hapa nitakuongozea.
 
Boss hii 20:80 ni nini? fafanua kidogo
Kong...

Uadilifu II

Serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani Mwaka (2015), Rais alifanya uteuzi wa Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Wilaya na Wakurugenzi mbalimbali. Uteuzi wake ulikuwa kama ifuatavyo:

Mawaziri na Manaibu: 30.

Waislamu 10, sawa na asilimia 33%.

Wakristo 20, sawa na asilimia 67%.

Makatibu Wakuu na Manaibu: 50.

Waislamu 10, sawa na asilimia 20%.

Wakristo 40, sawa na asilimia 80%.

Wakuu wa Mikoa na Wilaya: 166.

Waislamu 41, sawa na asilimia 25%.

Wakristo 125, sawa na asilimia 75%.

Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya: 163.

Waislamu 24, sawa na asilimia 15%.

Wakristo 139, sawa na asilimia 85%.

Wakurugenzi mbalimbali: 249.

Waislamu 45, sawa na asilimia 18%.

Wakristo 204, sawa na asilimia 82%.

Manaibu Kamishna wa Polisi: 25.

Waislamu 5, sawa na asilimia 20%.

Wakristo 20, sawa na asilimia 80%.

Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi: 33

Waislamu 7, sawa na asilimia 21%.

Wakristo 26, sawa na asilimia 79%.

Jumla Kuu ya Uteuzi:

Waislamu asilimia 20%.

Wakristo asilimia 80%.


Uteuzi huo umekuwa kama Sera kwa teuzi zinazoendelea ndani ya miaka yote mitano. Vilevile kama Mwongozo kwa wateule wenye mamlaka ya kuteuwa. Mwelekeo huo unakinzana na Katiba ya nchi ibara ya 13(4)(5), inayokataza ubaguzi wa aina zote. Kwa hakika Taifa halihitaji kiongozi wa nchi akiwa Muislamu basi ateuwe idadi kubwa ya Waislamu wenzake katika nafasi mbalimbali za uongozi wa nchi au akiwa Mkristo atumie uongozi wake kuteua idadi kubwa ya Wakristo wenzake katika uongozi nchini. Au akiwa Mzanaki ateuwe idadi kubwa ya Wazanaki wenzake katika nafasi mbalimbali za uongozi na mfano wa hayo.

 
Pep,
Usikae mbali na mimi.
Nina mengi sana katika historia ya Waislam wa Tanganyika.

Nimekuwa nikitafiti na kuandika toka niko kijana mdogo sana labda wa 20s.
Wewe upo bize na mwelekeo wa udini sana ktk mada zako nyingi nilizowahi kufuatilia.Eti una mengi sana ktk historia ya waislam.Kama umeamua kuchukua upande wa dini moja endelea na akili zako za kijahazi.Kwaiyo wewe badala ya kujielekeza kwenye weledi kwemye teuzi wewe upo bize na teuzi ktk misingi ya dini.Umewahi kujiuliza Misri ni wangapi wasio wa dini ..waliopo madarakani?
 
Makaveli...
Kinauzwa Ibn Hazm Media Centre Msikti wa Manyama, Mtoro na Mtambani.

Pia unaweza kukipata Soma Bookshop na Elite Bookshop Mbezi Samaki shs. 10,000.00.

Kipo kwa Kiswahili na Kiingereza.
Mi pia nakihitaji na nipo Tabora.
 
Boss hii 20:80 ni nini? fafanua kidogo

Mount...
Umeanza kuandika na "Wewe..." dalili ya ghadhabu.
Naam umri wangu wote nimetafiti historia ya Waislam wa Tanganyika

Sababu ni kuwa hapakuwa na msomi aliyetaka kuandika historia yao.

Kimambo na Temu (1969) wameandika historia ya uhuru Waislam ambao ndiyo walikuwa mstari wa mbele hawamo.

Leo mimi nimeandika upya historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Huijui historia ya Misri.
Zungumza unachokijua.

Nchi zenye Waislam wengi hakuna wapagani.
Jifunze utafahamu.

Soma "In Search of Identity," tawasifu ya Anwar Sadat utajua nani wanaongoza serikali ya Misri.

Soma "The Road to Ramadan," cha Mohamed Heykal utaijua Misri na walioko madarakani.

Dini ni muhimu kupita kiasi katika kutawala nchi yenye dini kubwa mbili.
Ukiachia serikali itawaliwe na watu wa imani moja utasababisha farka na fitna katika jamii.

Hutoweza kujenga umoja na amani ya kweli nchini.


Niko Alexandria, Egypt 1988.
 
Huyu mzee mi namwona wakala wa Ibilisi kabisa!! Kazi kubwa ya Ibilisi ni kupinduapindua maneno, giza lionekane mwanga na mwanga eti tuseme ni giza. Narudia huyu ni mhalifu!
 
Aamin mkuu.Tuendelee kuelimishana.
 
Mambo ya wewe dini gani? Au wewe kabila gani ni mabaya sana...
Smart...
Ni hatari kuliko hatari yenyewe.

Ukiwa na watu wa dini moja wamehodhi fursa zote wakati wenzao wako nje ya hizo fursa unajenga chuki katika jamii.

Lazima hali hii iondoshwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…