soine
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 2,113
- 2,329
Shikamoo Mzee Said. Hongera kwa uandishi wako kwa njia ya vitabu na makala.Belo,
Tunaweza tukafanya mjadala wa adabu na heshima bila ya kejeli na kebehi.
Mathalan ukishanisoma na ukaona kuna jambo una fikra tofauti na zangu ukaeleza.
Sasa hii "kulia," na maneno ya kukashifiana yanatoa ladha ya mjadala.
Hongera pia kwa kutetea usawa katika jamii.
Mzee Said nimekuwa mfanyakazi wa umma sehemu mbalimbali, kiukweli sijawahi ona sehemu ambayo ilifanyika makusudi na viongozi au sekretariati ya ajira kutoajiri mtu kwa sababu ya dini yake. Kikubwa ni sifa ya mtu wala sio dini. Ungesema kabila na ukanda hapo tungekuelewa kidogo maana kuna baadhi ya taasisi huko nyuma (sio enzi hizi za sekretariati ya ajira) zilijaa watu wa kabila au kanda fulani.
Udini kidogo umeanza kurise kuanzia 2000s tena kwa baadhi ya taasisi.
Huko nyuma ni kweli kulikuwa na gap kubwa kati ya mkristo na muislamu (sababu kubwa ilikuwa elimu, kuna upande uliwekeza zaidi elimu ya dini kuliko elimu dunia), ila kwa sasa wengi wa vijana na watoto wa kitanzania wamesoma bila kujali dini wala kabila....hata jamii za waokota matunda na mizizi pamoja na wafugaji wako wengi kwenye mfumo wa elimu na ajira.
Hivyo, Mzee wangu tambua hilo gap la elimu lilivyokuwa huko nyuma ukizingatia taasisi nyingi za elimu zilikuwa chini ya dini fulani.