Baba wa Taifa na tatizo la Udini

Baba wa Taifa na tatizo la Udini

Mohamed Said kwa mujibu wa takwimu zenu ni dini ipi yenye wafusi wengi hapa nchini kati ya Wakristu na Waislam?
Kinyungu,,,
Hili si muhimu hata kama kutakuwa na takwimu za kuaminika.

Muhimu ni kutazama tatizo hili la watu wa dini moja kuhodhi madaraka ya serikali na wenzao wakawa nje.

Na serikali iko kimya haijasema kuwa hawa wanahodhi madaraka kwa kuwa wao ni wengi.
 
H
Belo,
Tunaweza tukafanya mjadala wa adabu na heshima bila ya kejeli na kebehi.

Mathalan ukishanisoma na ukaona kuna jambo una fikra tofauti na zangu ukaeleza.

Sasa hii "kulia," na maneno ya kukashifiana yanatoa ladha ya mjadala.
Heshima yako Mkuu Mohamed Said. Mwaka wa 1976 au 77 nilipokuwa sekondari tulisoma kitabu " Kiu" kilichoandikwa na mtu mwenye jina la Mohamed Said, je huyu mtu ni wewe? Natanguliza Shukrani zangu
 
Kong...

Uadilifu II

Serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani Mwaka (2015), Rais alifanya uteuzi wa Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Wilaya na Wakurugenzi mbalimbali. Uteuzi wake ulikuwa kama ifuatavyo:

Mawaziri na Manaibu: 30.

Waislamu 10, sawa na asilimia 33%.

Wakristo 20, sawa na asilimia 67%.

Makatibu Wakuu na Manaibu: 50.

Waislamu 10, sawa na asilimia 20%.

Wakristo 40, sawa na asilimia 80%.

Wakuu wa Mikoa na Wilaya: 166.

Waislamu 41, sawa na asilimia 25%.

Wakristo 125, sawa na asilimia 75%.

Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya: 163.

Waislamu 24, sawa na asilimia 15%.

Wakristo 139, sawa na asilimia 85%.

Wakurugenzi mbalimbali: 249.

Waislamu 45, sawa na asilimia 18%.

Wakristo 204, sawa na asilimia 82%.

Manaibu Kamishna wa Polisi: 25.

Waislamu 5, sawa na asilimia 20%.

Wakristo 20, sawa na asilimia 80%.

Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi: 33

Waislamu 7, sawa na asilimia 21%.

Wakristo 26, sawa na asilimia 79%.

Jumla Kuu ya Uteuzi:

Waislamu asilimia 20%.

Wakristo asilimia 80%.


Uteuzi huo umekuwa kama Sera kwa teuzi zinazoendelea ndani ya miaka yote mitano. Vilevile kama Mwongozo kwa wateule wenye mamlaka ya kuteuwa. Mwelekeo huo unakinzana na Katiba ya nchi ibara ya 13(4)(5), inayokataza ubaguzi wa aina zote. Kwa hakika Taifa halihitaji kiongozi wa nchi akiwa Muislamu basi ateuwe idadi kubwa ya Waislamu wenzake katika nafasi mbalimbali za uongozi wa nchi au akiwa Mkristo atumie uongozi wake kuteua idadi kubwa ya Wakristo wenzake katika uongozi nchini. Au akiwa Mzanaki ateuwe idadi kubwa ya Wazanaki wenzake katika nafasi mbalimbali za uongozi na mfano wa hayo.

Mbona katika hiyo list sijaona atheist hata mmoja na mi silalamiki?

Kwanini waislamu ambao wamepewa vitengo wawe wa kwanza kuonekana kama wanatengwa kwasababu ya kuwa out numbered na wakristo ilihali kuna kundi la atheist ambapo hakuna hata kiongozi mmoja aliyepewa fursa?
 
Kuna watu mngezaliwa Kule Afghanistan,Iraq,Iran etc mngekua Magaidi tu,mnajifunga mabomu na kujilipua tu.Mshukuru Mungu tu mmezaliwa huku Tz,so mnashindwa tu kutekeleza Jambo hilo.Mna kila element za radicalism.
 
Okay mzee, Mohamed

Nadhani tuyaache kama ulivyoshauri.

Kama nilivyosema awali, inawezekana hayati alikua na mapungufu mengi tu (kama sisi wote)

Lakini hata kama ni kwa uchache.....alituunganisha sana.

Inawezekana hapa kwetu upo ubaguzi, sikupingi....ila nimetolea mfano Nigeria ambap kule ubaguzi ni wazi wazi.

Kila mtu anaona, na anajua namna wale jamaa wanapeana joto ya jiwe
Aiseee uko vzr sana[emoji122][emoji122][emoji122]
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Sijui mimi ni Kipofu..., Eti Sioni Waislamu wala Wakristo bali kila nikiangalia naona Watanzania..., Ingawa wapo wachache (wakaidi) ambao wanatumia tofauti ndogo ndogo kututofautisha kuliko mengi ambayo yanatuunganisha...
 
Kinyungu,,,
Hili si muhimu hata kama kutakuwa na takwimu za kuaminika.

Muhimu ni kutazama tatizo hili la watu wa dini moja kuhodhi madaraka ya serikali na wenzao wakawa nje.

Na serikali iko kimya haijasema kuwa hawa wanahodhi madaraka kwa kuwa wao ni wengi.
Ni la muhimu sana kwa sababu inawezekana wanahodhi madaraka kwa sababu ni wengi.

Suala la wepi ni wengi halikwepeki.
 
H

Heshima yako Mkuu Mohamed Said. Mwaka wa 1976 au 77 nilipokuwa sekondari tulisoma kitabu " Kiu" kilichoandikwa na mtu mwenye jina la Mohamed Said, je huyu mtu ni wewe? Natanguliza Shukrani zangu
Waji...
Hapana si mimi.
 
Ni la muhimu sana kwa sababu inawezekana wanahodhi madaraka kwa sababu ni wengi.

Suala la wepi ni wengi halikwepeki.
Kinyungu,
Sikupenda niliseme hili lakini nitalisema kukutoa shaka.

Mwaka wa 2011 nilialikwa University of Iowa, Marekani.

Likaja swali kama hili lako katika mhadhara niliofanya pale.

Wao wakaja na takwimu za CIA kuhusu "religious distribution," Tanzania na kueleza kuwa madaraka yamehodhiwa kwa wingi uliokuwapo.

Jibu langu lilikuwa swali kwa hadhira yangu ambayo yote ni hao watupu ukumbi mzima na wote ni maprofesa wa historia.

Nikawaomba wanipe mfano wa nchi moja duniani ambayo imevamiwa na wakoloni kutoka nje na waliosimama kunyanyua silaha na kupigana na wavamizi wakawa ni wale wachache.

Hapa nikatoa mfano wa Vita Vya Maji Maji.

Kwa bahati katika hadhira ile alikuwapo Prof. James Giblin ambae ameandika kitabu cha Maji Maji.

Nikatoa mfano mwengine nikauliza harakati za Waafrika kujitambua na kudai uhuru zilipoanza Tanganyika nani waliokuwa mstari wa mbele kudai nchi yao?

Nikawafanyia rejea katika kitabu cha Abdul Sykes ambacho wao wanakifahamu na wanakisomesha kama rejea katika historia ya Afrika.

Nikauliza historia yote ya kupigania uhuru wa Tanganyika nani waliokuwa mstari wa mbele?

Je ni hawa wachache?

Nikawaomba watoe mfano wa nchi moja tu duniani ambako wachache walisimama kuikomboa nchi yao.

Ukumbi ulikuwa kimya.
Hapakuwa na jibu.

Ukweli ni kuwa siku zote wale wengi ndiyo wanaokuwa na nguvu ya kupambana na adui na wengine huwa nyuma kuongeza nguvu.

Picha hiyo niko darasani nasomesha University of Iowa kushoto ni Prof. James Giblin.

Screenshot_20220128-121707_Photos.jpg
 
Shida yako kubwa ni kutaka waislamu wapewe special status Tanzania, kwa sababu ambazo kusema kweli hazina mashiko kabisa. Kila unapomuongelea baba wa Taifa, unaona kama hakufanya haki kuwapa waliokuwa waislamu katika kudai uhuru special favors.
Unalopigania kusema kweli hutalipata duniani na wala mbinguni maana lina lengo la kutugawa watanzania bila sababu
Mwaka huu Kuna Sensa, tusubiri mzee aanze kuchochea waislamu wakatae kuhesabiwa mpaka pale dodoso la Sensa litakapowekwa kipengele cha dini.
 
Mbona katika hiyo list sijaona atheist hata mmoja na mi silalamiki?

Kwanini waislamu ambao wamepewa vitengo wawe wa kwanza kuonekana kama wanatengwa kwasababu ya kuwa out numbered na wakristo ilihali kuna kundi la atheist ambapo hakuna hata kiongozi mmoja aliyepewa fursa?
Scars,
Hatuna Wapagani.

Tujaalie wapo.

Uliwaona Wapagani wakati wa Maji Maji au kupigania uhuru wa Tanganyika?

Huwezi kuwapambanisha Waislam hata na Wakristo katika historia ya Tanganyika.
 
Sijui mimi ni Kipofu..., Eti Sioni Waislamu wala Wakristo bali kila nikiangalia naona Watanzania..., Ingawa wapo wachache (wakaidi) ambao wanatumia tofauti ndogo ndogo kututofautisha kuliko mengi ambayo yanatuunganisha...
Key...
Wazee wetu waliwaona Watanganyika wakati wanapigania uhuru wa nchi hii.

Leo tuko katika 20:80.
Wewe uko katika 80.

Hi ndiyo sababu huna unachokiona.
 
Key...
Wazee wetu waliwaona Watanganyika wakati wanapigania uhuru wa nchi hii.

Leo tuko katika 20:80.
Wewe uko katika 80.

Hi ndiyo sababu huna unachokiona.
Unajuaje kama mimi sipo kwenye 0% ya representation..., Unajua Watanzania wote sio Wakristu au Waislamu..., kuna Traditional African Religions na wengine ni Unaffiliated...

Kwahio na mimi nianze kudai representation sababu ya Imani yangu na sio Weledi wangu ? Nadhani hii vita tungeipigana wote kuondoa uduni wa kila Mtanzania / Mtanganyika na sio kugawana umasikini (as I see it watanzania wengi ni duni no matter their beliefs)
 
Mwaka huu Kuna Sensa, tusubiri mzee aanze kuchochea waislamu wakatae kuhesabiwa mpaka pale dodoso la Sensa litakapowekwa kipengele cha dini.
Mose...
Mimi nadhani hunifahamu.

Jitahidi kunielewa mimi nani nini nafasi yangu katika jamii ya Waislam utajua nini la kusema kuhusu mimi.
 
Mose...
Mimi nadhani hunifahamu.

Jitahidi kunielewa mimi nani nini nafasi yangu katika jamii ya Waislam utajua nini la kusema kuhusu mimi.
Sihitaji kukujua kwasababu hujawahi kuwa na Jambo lolote la maana, hate wewe mwenyewe unajua.

Ndio maana unachochea watu huku wewe uko nyuma.
 
Sihitaji kukujua kwasababu hujawahi kuwa na Jambo lolote la maana, hate wewe mwenyewe unajua.

Ndio maana unachochea watu huku wewe uko nyuma.
Mose...
Umeghadhibika.

Ningekuwa mchochezi siku nyingi ningeshitakiwa.

Wala siko nyuma katika kudai haki za Waislam.

Niko katika YouTube na nimeandika vitabu kadhaa na vinauzwa madukani.

Kitabu changu cha kwanza ni 1998 na cha mwisho ni 2020 na vyote vimependwa na wasomaji vingine vimechapwa mara 4.

Nafahamika kwa sura na sauti.

PUBLICATIONS/RESEARCH PAPERS/ARTICLES
1. The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 –1968 The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press London, 1998 translated into Kiswahili as Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968 Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza, Phoenix Publishers, Nairobi, 2002.
2. The Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press, Nairobi, 2006
3. Contributing author for an African anthology: The Mermaid of Msambweni and Other Stories, Oxford University Press 2007, Nairobi.
4. Contributing author Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press 2011, New York.
5. Uamuzi wa Busara, Abantu Publications 2008, Dar es Salaam.
6. Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No. 1, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam.
7. Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No.2, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam
8. Dar es Salaam na Wazalendo Wake Mashujaa Katika Kupigani Uhuru wa Tanganyika Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaaam
9. Watu Mashuhuri Katika Kuulingania Uislam Tanzania, Sheikh Ilunga, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam
10. Dola, Kanisa na Tatizo la Udini Tanzania, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam
11. The School Trip to Zanzibar, Africa Proper Education Network 2020, Dar es Salaam
12. Rajabu Ibrahim Kirama, Jemadari wa Vita Kuwa Jemadari wa Uislam, Readit, 2020, Dar es Salaam
13. In Praise of Ancestors (1987) Africa Events (London).
14. Abdulwahid Sykes: Founder of Political Movement (1988) Africa Events (London).
15. Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)
16. The Plight of Tanzanian Muslim (1993) Change (Dar es Salaam).
17. Tanzania - The "Secular" Unsecular State (1995) Change (Dar es Salaam).
18. The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).
19. Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).
20. Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004).
21. Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro 11th April 2004).
22. Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and African Development University of Ibadan, Nigeria 8th - 10th February 2006).
23. Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma bin Khamis (1940 – 1994) and the Pork Riots of 1993. (Paper Presented at the Regional Conference on Islam in Eastern Africa: Islam Encounter with the Challenges of the 21st Century 1st - 3rd August 2006, Kenyatta University, Nairobi.
24. Muslim Bible Scholars of Tanzania – The Legacy of Sheikh Ahmed Deedat (1918 – 2005) Paper Presented at the International Symposium on Islamic Civilisation in Southern Africa Organised by The Organisation of Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA) The National AWQAF Foundation of South Africa (AWQAF SA 1 – 3 September 2006 University of Johannesburg.
25. Tanzania: A Nation Without Heroes Seminar Organised by IFRA French Institute for Research in Africa and BIEA British Institute in East Africa 23rd and 24th September 2013 at IFRA Nairobi.
26. Awards: Several Awards
27. Visiting Scholar: (2011)
28. University of Iowa, Iowa City, USA
29. Northwestern University, Chicago, Illinois, USA
30. Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin.
31. OTHER COUNTRIES VISITED
32. Zambia, Ethiopia, Great Britain, Swaziland, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia, Sudan, Egypt, Saudi Arabia, United Arab Emirates, Oman, Yemen, Uganda, Switzerland, Iran, France, Netherlands, Turkey and Abu Dhabi.

Sijapata kuwa na jambo lolote la maana unasema.

Naamini sasa umenijua.
Haya ndiyo niliyotaka uyajue.
 
Back
Top Bottom