Baba wa Taifa na tatizo la Udini

.Si Dhani kama Picha inaendana na maswali niliyouliza.Labda naomba unisaidie Mzee wangu kuelewa maana ya hii picha na majibu ya maswali yangu.


Sent from my TECNO CD7 using JamiiForums mobile app
 
Mzee wangu naomba kujua tu kwamba ikiwa kutakuwa na balance baina ya idadi ya waislamu na wakristo katika wizara fulani hilo jambo lina faida gani kwa waislamu ?

Mfano waziri wa mambo ya ndani kwa sasa ni muislamu,je waislamu wamefaidika vipi na huyu mtu kuwa waziri ?
 
Saf...
Kinachotafutwa si faida au hasara.

Kinachotafutwa ni uwiano na haki kwa wananchi wote kushiriki katika uongozi.

Kuachia watu wa dini moja kuhodhi serikali kunaleta fitna katika jamii.

Kinachotafutwa ni kuondoa hii fitna ili upatikane umoja.

Waza kwa dakika moja hayo majina hapo chini wangekuwa Waislam watupu.

Balaa lake lingekuwa kubwa.

 
Sawa sawa.
Kinachotafutwa si faida au hasara
Unafikiri hakuna haja ya kuwaelimisha watanzania kwamba kuwepo kwa watu wa dini moja sehemu fulani hakuna manufaa na dini hiyo hivyo watanzania tusianzishe fitina,unafikiri hakuna haja ya kuwaelimisha hivi watanzania ?

Kwa sababu kumbe watanzania wanaweza kuleta fujo na fitina katika jambo ambalo wala halina madhara yoyote .

Hii inakuwa ni hatari kwamba watanzania waanze kuingia fitina wao kwa wao kwa jambo ambalo hata wakiliwacha halina shida.
Kuachia watu wa dini moja kuhodhi serikali kunaleta fitna katika jamii.
Naomba kujua hii fitina si inaletwa kwa sababu ya fikra za wananchi kudhami kwamba watu wa dini fulani watanufaika zaidi kuliko watu wa dini ambayo haijachaguliwa.

Je kwa nini wewe kama mzee wetu usianzishe kampeni ya kuwaelimisha watanzania hasa watu wa dini yako kwamba wasije kuleta fitina ikiwa watu wa dini fulani wamechaguliwa kwani hakuna madhara yoyote,je kwa nini usiwaelimishe watz mzee wangu ?
Kinachotafutwa ni kuondoa hii fitna ili upatikane umoja.
Mfano mzuri wakati wa mwalimu tumefaidika kusoma kwako kwamba alipokewa na waislamu wengi sana.

Na waislamu wale walikuwa na umoja na mshikamano kwa nyerere.

Kama kuwa na watu wa dini moja kunaweza kuleta fitina na kuondoa mshimamano kwa nini wakati huo waislamu walionesha mshikamano na nyerere wala hawakuleta fitina yeyote kama ambavyo wewe unahofia leo ?
 
Saf...
Tuanze kwa kuchagua Waislam watupu tuangalie itakuwaje?
 
Saf...
Tuanze kwa kuchagua Waislam watupu tuangalie itakuwaje?
Hapana tuangalie zanzibar kwanza ambako kuna waislamu watupu kabla yatujafanya huku.

Je kwa zehemu kama zanzibar wizara zote zina waislamu wewe unadhani wamenufaika ama kupata jambo gani kubwa katika uislamu au kwa waislamu alafu ikawa uislamu wa huku bara haujalipata jambo hilo kutoka katika serikali ya bara ambako kuna wakristo wengi ?
Tuanze kwa kuchagua Waislam watupu tuangalie itakuwaje?
Kwa nini umechagua waislamu na tusianze na wakristo wachaguliwe kwanza ?
Tuanze kwa kuchagua Waislam watupu tuangalie itakuwaje?
Pia mzee wangu hii haitokuwa kampeni itakuwa ni kuendeleza lile linaloitwa tatizo kwa sababu raia hujawapa kampeni yoyote ya kukabiliana na jambo hilo
 
Scars,
Hatuna Wapagani.

Tujaalie wapo.

Uliwaona Wapagani wakati wa Maji Maji au kupigania uhuru wa Tanganyika?

Huwezi kuwapambanisha Waislam hata na Wakristo katika historia ya Tanganyika.
Kwa hiyo unakusudia kumbe vyeo vya madaraka vinatakiwa vitolewe kuzingatia dini ambazo kipindi hicho cha uhuru watu wa dini hiyo walipambana kuikomboa tanganyika?

Kwa maana hiyo mkristo au muislamu ambaye baadaye akaja kuwa atheist tafsiri yake ni kwamba hapaswi kuwa sehemu ya madaraka kwasababu tangu aache ukristo anakuwa amekosa sifa?
 
Huwezi kuwapambanisha Waislam hata na Wakristo katika historia ya Tanganyika
Mzee wangu waarabu wa makka waliutetea uislamu kwa hali na mali kuliko watu wengine wowote duniani

Je hii ina maana ya kwamba katika uislamu waarabu wa makka wana haki zaidi kuliko waislamu wengine wowote wale duniani ?
 
Saf...
Mjadala mzuri nimependa hoja zako.
 
Scars,
Najifunza mengi hapa.
 
Hawezi kujibu maswali ya msingi lazima atayakimbia ataendelea kurudia hoja zake zile zile,angalia mada zake anazoanzisha akibanwa maswali anayakwepa
Belo,
Sikujua kama unaona nakwepa maswali ya msingi wala sikuwa natambua kuwa nabanwa.
 
Huyu mzee Mohamed Said anaona kama anatetea dini kumbe anajitia ujinga kichwani...
 
Hapa nasoma maoni tu ya wachangiaji.
Huyo Nyerere sikuwahi hata kumwona.
Ila namshukuru sana kwa kuondoa Ukabila hapa nchini.
 
Scars,
Najifunza mengi hapa.
Wote tunajifunza hapa na ndio maana tunafanya mjadala kubadilishana mawazo tupate maarifa mapya

Nataka nijue nchi hii mtu asiyekuwa na dini amepewa kipaumbele gani kwenye rank za madaraka

Lakini pia ningependa kujua ni vigezo gani ambavyo vinaangaliwa sana linapokuja swala la kupeana madaraka

Hapo juu nimeona umeelezea 80:20 ambayo imehusisha wakristo na waislamu

Lakini sijakuona ukijitokeza kuwasemea kundi lililosahaulika hapo (atheists) kuwa wanabaguliwa na viongozi wa dini hizo mbili (islam&christian) badala yake umeongelea uislam kua umezidiwa na ukristo katika rank za madaraka, ila atheists ambao hawajapata hata mtu mmoja serikalini umeona ni sawa

Kwanini iwe hivyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…