Baba wa Taifa na tatizo la Udini

Baba wa Taifa na tatizo la Udini

Acha janja janja.
Jibu swali. Umepimaje au umejuaje kuwa hao ni wakristo au waislam?
Nan...
Sina ujanja nami sipendi kusema neno nikaonekana nakejeli.
Ndiyo nakueleza kuwa unazungumza na Mohamed Said.
 
ksk,


Uamuzi huu ulifanyika nyumbani kwa Hamza Mwapachu Nansio mwaka wa 1953 miezi ya mwanzo kabla ya mwezi April uchaguzi wa TAA ulipofanyika.


Mohamed Said,
Hakika nimepata somo,nyumba aliyokuwa anaishi mzee mwapachu ilikuwa ni nyumba ya Babu yangu,nilikuwa naona picha tu kwenye kabati lake zimeandikwa majina,akiwa yeye,mwapachu na Sykes na zingine akiwa na chief wa wakerewe.
 
Saint...
Hili si suala la dini kama ''doctronaire,'' hapa tunaangalia iweje fursa za serikali zikahodhiwa na watu wa dini moja kw akiwango hiki cha 20:80?

Wanaostahili kuwajibu Waislam wako kimya.

Wewe ndiye unaetoa majibu.

Nakuhakikishia kuwa serikali haiwezi kutoka jibu jepesi kama lako.

Hii ndiyo sababu ya ukimya wake.

Wapo kimya kwa sababu wanawaona hamna hoja za msingi ni wapuuzi,mfano nikuulize wewe kama muislam waajiriwa 100% wakawa ndo wapo kwenye hizo nafasi unazozungumza wewe unaona kuna fursa gani kwa muislam maskini aliye Namtumbo?au kwa wakristo wote 100% wakawa ni watu wao wapo kwenye system ni favour gani wataipata?obviously hakuna na ugumu wa maisha utakuwa pale pale as long as hao waajiriwa wataziangalia familia zao na wale wanaowazunguka hata kama wakawa ni dini tofauti hilo hawataliona.

Ukiingia ofiisi ya serikali (mf mimi mfanyabiashara) hawaangalii dini wale kama ni fine wanakuandikia kama stuff akawa ni muislam au mkristo mwenzako haendi tofauti na sheria inavyotaka sasa kwa machapisho yako haya utasababisha waliopo kwenye ajira serikalini kuanza kuwabagua wa Imani tofauti na yao.
 
Sasa hivi tunatawaliwa na Waislamu tu Tanganyika na Zanzibar.
Je na sisi wa Jamii nyingine tuchukue hatua gani?

Ili kuondokana na hii Islamic Rule
Ambayo inaonekana imechukua nafasi hizi kwa hila za kututawala sisi wengine ?

Waislamu kwani uislamu ni jina la mtu?
Anayetawala ni CCM chama kilichoundwa Na kanisa.
 
Humkuti akijibu maswali kama haya,ingekuwa imechomwa misikiti angekushushia gazette la maelezo.

Udini tu miaka na miaka ndo anachopst humu na jamii forums moderator wanamwacha azidi kutuvuruga.
Unafikiri Zanzibar ilivamiwa Na nani? Okello alikuwa Na dini gani ?
 
Sasa hivi tunatawaliwa na Waislamu tu Tanganyika na Zanzibar.
Je na sisi wa Jamii nyingine tuchukue hatua gani?

Ili kuondokana na hii Islamic Rule
Ambayo inaonekana imechukua nafasi hizi kwa hila za kututawala sisi wengine ?
😂😂😂
Maswali kama haya Mohamed Said anapotezea tuu. Hana majibu!
Seems hana fikra huru, ni mdini wa kutupwa!
 
Mag,


View attachment 2102181
Kulia waliosimama: Mohamed Said (Mmnanyema kitukuu cha mlowezi), wa tatu Kleist Sykes (Mzulu kitukuu cha mlowezi. Waliochutama wa kwanza kulia Abdul Mtemvu (Mluguru mtoto wa Mmanga Mtemvu) na anaefuatia ni Wendo Mwapachu (Mdigo mtoto wa Hamza Mwapachu) sisi wazee wetu walikuwa katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika. Huu ulikuwa mwaka wa 1968.


Samahani unaweza kutuambia kwanini umeweka hii picha hapa?una ujanja fulani uliopitwa na wakati wa kuhamisha mantiki ya mjibu hoja yako kwa wewe kushindwa kuijibu hoja yake na kuweka picture ili mtu huyo aachane na wewe.

Sidhani kama uliyem-quote alitaka kuwafahamu hao kwenye picha ila wewe unamlazimisha akili yako inavyotaka!!!
 
Mkuu,
Ili kuweka mizania sawa kwenye huu uzi wako, Una maoni gani juu ya uchomaji Moto uliopelekea uteketezaji wa maelfu ya makanisa Bara na Znz wakati wa awamu ya 2 na ya 4 ?
Una ushahidi wa muislamu yoyote kuchoma kanisa katika muda Huo ulioutaja ?
 
😂😂😂
Maswali kama haya Mohamed Said anapotezea tuu. Hana majibu!
Seems hana fikra huru, ni mdini wa kutupwa!

MJADALA unaendelea nchini kote juu ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika na muundo wa Muungano wa Zanzibar na Tanganyika. Inavyoelekea yapo matatizo, dosari na sababu za msingi zilizopelekea wananchi kuhoji muundo wa sasa wa Muungano na kuleta hoja ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika ni yenye kuundwa kama si leo kesho.

Lakini wapo pia wanaopinga kabisa kuundwa kwa serikali ya Tanganyika.

Aliyejitokeza kwa nguvu na kwa ukali hadharani kupinga hoja hiyo ni Mwalimu Julius Nyerere, katika kupinga hoja hiyo Mwalimu anatoa hoja zifuatazo:

Hoja ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika imeletwa kwa kuwachoka Wazanzibari na Waislamu. Ufupi wa maneno Mwalimu Nyerere anadai hoja ya kuundwa Serikali ya Tanganyika imetokana na chuki za kidini - Wakristo kuwachukia Waislamu.

Hoja haipo katika sera za CCM na taratibu zimekosewa.

Kuundwa kwa serikali ya Tanganyika kutavunja Muungano na kutavunja Tanganyika pia.

Ukizingatia sifa nyingi ambazo Nyerere alijilimbikizia wakati wa utawala wake na sasa si vigumu kuelewa kwa nini anapinga kuundwa kwa serikali ya Tanganyika. Mambo yake yote aliyoyaanzisha kwa vishindo huku akisifiwa kuwa zidumu fikra zake, yamekuwa yakiporomoka moja baada ya jingine huku mwenyewe akiona. Lililosalia ni Muungano; nao ukiporomoka haitaleta picha nzuri katika historia yake katika siasa.

Lakini lililo gumu kueleweka ni hatua ya Mwalimu Nyerere kutumia Turufu ya udini kuwagawa Wabunge; wana-CCM na Wa-Tanzania kwa ujumla katika suala hili. Kauli hiyo ingesemwa na Muislamu ingepewa mtizamo tofauti na labda isingeeleweka hasa miongoni mwa Waislamu. Lakini kusemwa na Mwalimu Nyerere kunaleta mkanganyiko zaidi. Kwanini; (udini ulikuwa umejengeka). Hali hiyo ilipelekea Masheikh kumlalamikia lakini akawanyamazisha kwa kuwashutumu kuwa wanachanganya dini na siasa. Miongoni mwa Masheikh hao wapo waliofukuzwa nchini; waliowekwa kizuizini, waliofukuzwa katika chama na kadhalika.

Sheikh Hassan bin Amir katika waraka wake kwa Waislamu mwaka 1963 aliutaja udini uliokuwa unajengwa Tanzania kwa kutoa mifano ifuatayo:

Kuingizwa nchini Tanganyika mara tu baada ya uhuru vimedali vidogo vidogo vyenye picha ya bendera ya Tanganyika usoni na katikati ya bendera hiyo amesimama Mama Maria na mtoto mchanga na nyuma yake maandiko 'MARIA MTAKATIFU ULINDE UHURU WA TANGANYIKA'.

Gazeti la KIONGOZI la tarehe 1/8/1963 lilimuonyesha Bwana George Kahama akipewa cheo cha dini na Pope kwa kuwakilisha serikali ya Tanganyika katika mkutano wa Makanisa ya Roma.

Mwaka huo huo wa 1963, mnamo tarehe 24 mwezi wa nane, Baraza Kuu la Makanisa ya Kilutheri Tanganyika lilitoa matangazo kuwa Uhuru wa Tanganyika ulikuwa 'Chini ya Msalaba'.

Tarehe 17/5/1963 Makanisa yalifanyia mkutano wao ndani ya Bunge.

Alipokufa Pope Yohana wa 23 bendera ya taifa ilipepea nusu mlingoti nchi nzima!

Kabla ya kifo chake Pope Yohana wa 23 alimletea Mheshimiwa Nyerere barua ya pongezi kwa kuupanua Ukristo- barua ambayo ilitiwa saini na Pope mwenyewe. Barua hiyo imetangazwa kwenye gazeti la Tanganyika Standard.

Gazeti la Reporter la Kenya la tarehe 20/6/1963 lilitangaza katika ukurasa wake wa mbele: "KUIBADILI AFRIKA YA MASHARIKI KUWA KATIKA DINI YA ROMANI CATHOLIC". Ndani ya gazeti hilo ukurasa wa 18 liliwataja waliopewa dhamana ya kufanikisha jambo hilo kuwa ni: Uganda - Kiwanuka, Kenya - Mboya na Tanganyika Mheshimiwa Nyerere.
 
Mbaya zaidi anayekuambia hivyo Ni mtoto mdogo na anatambua fika wewe ni sawa na baba yake

Hapa JF tunaangalia hoja zako hatuangalii umri ,unaweza kuwa babu yangu lakini hoja unazotoa hazifanani na kuwa babu yangu

MS tangu kajiunga JF mada zake ndio hizi hizi na akiulizwa maswali ya msingi anakwepa baada ya wiki moja anafungua mada nyingine hoja ni hizo hizo atatuma picha hizo hizo


Nyerere anayemlalamikia alishaondoka madarakani karibia miaka 40 iliyopita
 
Ngorunde,
Kugombea haki si kuleta chuki.
Tanganyika haikudai uhuru wake kwa kuwa wanawachukia Waingereza.
Mzee inaoneasha wazi una msongo wa mawazo ambao aidha umesababishwa na malezi au makuzi enzi ya utoto/ujana wako.
Pole sana...M/Mungu akufanyie wepesi!
 
Mzee inaoneasha wazi una msongo wa mawazo ambao aidha umesababishwa na malezi au makuzi enzi ya utoto/ujana wako.
Pole sana...M/Mungu akufanyie wepesi!

Wewe utakuwa umezidi otherwise ungalimjibu kwa hoja
 
Hapa JF tunaangalia hoja zako hatuangalii umri ,unaweza kuwa babu yangu lakini hoja unazotoa hazifanani na kuwa babu yangu

MS tangu kajiunga JF mada zake ndio hizi hizi na akiulizwa maswali ya msingi anakwepa baada ya wiki moja anafungua mada nyingine hoja ni hizo hizo atatuma picha hizo hizo


Nyerere anayemlalamikia alishaondoka madarakani karibia miaka 40 iliyopita
Nyerere alishaondoka mbona kila siku Baba wa taifa kajamba hivi kafusa vile ?
 
Samahani unaweza kutuambia kwanini umeweka hii picha hapa?una ujanja fulani uliopitwa na wakati wa kuhamisha mantiki ya mjibu hoja yako kwa wewe kushindwa kuijibu hoja yake na kuweka picture ili mtu huyo aachane na wewe.

Sidhani kama uliyem-quote alitaka kuwafahamu hao kwenye picha ila wewe unamlazimisha akili yako inavyotaka!!!

Ukweli asiotaka kuueleza ni Mohamed Said ni jinsi uhusiano kati ya walowezi Wazulu (Wakristo) na Manyema ulivyopandwa, ukakua na ukakomaa hadi wakawa ndugu wa damu.

Ukweli mwingine asiousimulia ni kilicho nyuma ya hizi jitihada zake za kutaka kuwakuza hawa walowezi wawe msitari wa mbele kama Watanganyika zaidi ya wazawa wenyewe wa asili.

Dini anaitumia tu kuficha lengo lake kwani Waislamu wazawa ni kama vile anawaweka daraja la pili. Anajua fika kuwa katika kitabu cha Watanganyika kilichotaja makabila yote ya Tanganyika wakati wa mkoloni, wazulu na Manyema hawapo.

Akafikiria namna ya kuwaingiza wazee wake kwenye historia ya Tanganyika ni kwa kutumia udini. Wazulu walikuwa ni askari vijana waliotoka vitani wakalowea Tanganyika na hawakuwa na familia.

Vijana wa Kizulu (Wakristo) wakatengewa na wakoloni eneo la Gerezani wakiishi na Manyema. Wakawaona mabinti wa kimanyema (Waislaam) kuwa ni wazuri na kutaka kuwaoa. Sharti walilopewa ili kuwaoa ni kubadilisha dini.

Undugu wa damu ukaanzia hapo na Mohamed Said alizaliwa kwenye mazingira yanayofanana na hayo. Wajomba zake walikuwa Wazulu. Leo anawakuza wazee wake kama ndio hasa wapigania uhuru wa Tanganyika!

Vipi Watanganyika? Je bila walowezi hatungepata uhuru? Je bila wazulu na Manyema hakuna Mtanganyika angedai uhuru? Hizi nguvu zote za kuwaingiza na kuwatanguliza walowezi katika historia ya Tanganyika lengo lake hasa nini?

Eti ndio hao walowezi walioongoza mapambano ya kudai uhuru ni tusi kubwa kwa Watanganyika. Unamkuta mjukuu wa walowezi anamdhihaki hadi baba wa Taifa akidai si lolote, si chochote! Kwamba uongozi alipewa tu na wazee wa Gerezani!

Really? Naishia hapo.
 
Back
Top Bottom