Hapa sijakuellewa kwa kweli ulikuwa una maanisha kitu gani.Mkuu bwana soma hii" ni wangapi wanabaka! ni wote wanafikishwa mahakamani?" hapo ujapembua vizuri sababu wengine hawashikwi wengine hawana uthubutu wa kusema popote pale na watuhumiwa wanazidi kufanya uhalifu wao
Mkuu wewe ndio Chupaku I mean una ID mbili... just curiosity...! Anyway mimi sioni cha kujadili hapa. Kama wameshindwa kufuata taratibu tangia mwanzo, unategemea kupata suruhisho sasa?
Nambie basi maana uzi unafikia ukurasa wa tano sasa... Suruhisho ni nini?
Kuna mambo hapo juu nimayaeleza, lakini hakuna mtu ambaye ameyazingatia, ila naona watu wanatetea kile wanacho kipenda.
Unaniuliza mimi kuwa watu wajadili mambo yepi.... Siwezi kuwapangia kwa kweli... ila tunatakiwa kuwa na kiyasi katika kuelezea matukio yetu na haswa yanayo husu familia, si kila jambo ni kwenye Tovuti baraza... Mi bado nasisitiza kuwa ni ukosefu wa nidhamu na kukosa heshima na adamu.
Yaani mkeo/mume kakunyima, mbio JF, Baba na Mama wamegombana mbio JF...! Fulani kakukonyeza mbio JF... Mchumba wa zamani kakuudhi basi unaanika aibu yake JF pamoja na picha zake za utupu... Ahhhhhhh!
Nasikitika bado ujanielewa mpaka sasa... Na sijui kwa nini unielewi. Icho kisa nakijuwa na kuna kisa kama icho kimetokea miaka hii ya karibuni, vile vile naelewa na nafahamu hathari zake kwa mtendwa.... Ninacho sisitiza mimi ni kuwa kwa herufi kubwa and bold:Mimi sio Chupaku!
Mwisho wa siku inabidi 'agree to disagree'...
Kuna kisa kimoja huko Ulaya, Baba 'alimfungia' binti yake ndani ya nyumba yake miaka ya 80, na akamzalisha watoto kama 8 SOMA HAPA BBC News - German incest father-of-eight Detlef S jailed
Unataka watu kama hawa waendelee kunyamaziwa tu, kisa kutunza heshima..Kumheshimu mzazi hakutakiwi kuwa na mjadala..lakini kuna visa vingine ni balaa..
Wadau wa JF.
Hiki ni kisa cha ukweli kilichotokea wiki iliyopita. Ninakiandika kwa huzuni sana na aibu kubwa. Nilikuwa safarini na niliporudi nimekuta kesi hii inafukuta ikiwa imetokea kama siku 2 kabla ya mimi kuwasili.
Baba yangu ana umri wa miaka 70 plus. Mama yangu yupo Mid 60s. Ilitokea kwamba wana housegirl wa umri wa miaka 18 hivi toka maeneo ambayo hutoa wasichana wengi wa jinsi hii.
Bila kupamba jambo hili, baba yangu amembaka huyu msichana wakati mama hayupo. Msichana alitaka kwenda kushitaki polisi ila aliombwa sana na ndugu zangu asifanye hivyo.
Jambo hili limeleta vurugu kubwa sana nyumbani. Hakuna anayetaka kungea na mzee na mama amesema anafunga mizigo yake arudi kwao (at that age?). Watoto tumebaki tunashangaa hatujui la kufanya maana wale ni wazazi wetu na tunaona aibu hata ku-share na spouses wetu (tunaogopa kumbe nyiye ndivyo mlivyo). Pia watu wa dini unaanzaje kuwaelezea? Tunajiuliza kama huyo binti amepata ujauzito je? Kama akiamua kushitaki polisi je?
Yani sijawahi kupata fedheha kama hii. Hata sisi kwa sisi hatutaki kulizungumzia jambo hili.
Tumsaidieje mama?
Tuokoeje ndoa yao? Mzee hataki kukaa nyumbani safari za hapa na pale haziishi!
Tumsaidieje yule binti wa watu na trauma hiyo?
Naombeni msaada, bila matusi tafadhali. Mbakaji akiwa mbali rahisi kusema - afungwe, ila baba yako unasemaje?
Housegirl kaondoka ila tunazo contacts zake bado. Hivi babu wa hivyo unaweza hata kumuacha na mjukuu kweli? AArrrgggghhh
Kwanza kabisa naweza kusema wewe mtoa mada hii ebu niangalie jina lako kwanza... Ooh Chupaku, HUNA ADABU hata kidogo tena naweza kusema umemkosea adabu Mzee wako (I mean Baba yako Mzazi), napata wasi wasi kama huyo uliye muelezea hapa ni baba yako kweli au ni baba wa kambo au wa Kufikia.
Haiwezekani jambo kama ili la kifamilia mshindwe kulizungumzia uko uko nyinyi kwa nyinyi, mpaka ulilete hapa hadharani, kwani unafikiria watu hawakujui wewe Chupaku ni nani? Nikiangalia IP tu hapa najuwa unaandika kutokea wapi na unatumia mtandao gani.
Hivi uko kwenu ukufunzwa adabu na heshima? Ukuambiwa kuwa mambo yanayo husu familia huwa yanatatuliwa kifamimilia!? Hakuna wazee kwenye ukoo wenu, au mzee aliye baki hai ni Baba na Mama Chupaku tu!?
Siku mkeo akikunyima unyumba pia utaleta humu JF ili kupata ushauri? Grow up my friend, this is not funny.
Alafu unadai eti nanukuu "...aibu hata ku-share na spouses wetu (tunaogopa kumbe nyiye ndivyo mlivyo)...."
Sasa unataka kosa la mtu mmoja kuhumiwa ukoo mzima, unacho kiogopa kuongea na wake zenu nini na unacho kifanya hapa ni nini.
Yaani hapa unataka kudhihirisha kuwa wewe unamini watu walioko JF kuliko spouses wenu, familia yako wewe na ndugu zako na hata wazee wa Ukoo wanu.
Maybe you better think twice next time my friend before you just post mambo ya kifamilia.
Lol watu wanamfeva mzee tu, ambae umri wake umesha na sasa hivi anamkopa Mungu, wamesahau kabisa kuhusu huyu binti ambae bado anadai miaka kama hamsini hivi! huyu mzee ni wa kufunga tu hakuna cha kumfichia siriMambo ya familia yanamalizwa kifamilia. Kaeni kifamilia myazungumze. Cha msingi kama mmoja alivyoshuri, kampimeni huyo binti kama ni mjamzito au kama ameathirika. Kama hana tatizo, basi mumsihi mambo yaishe kwani suala hili likipelekwa kisheria, baba atafia jela
Nasikitika bado ujanielewa mpaka sasa... Na sijui kwa nini unielewi. Icho kisa nakijuwa na kuna kisa kama icho kimetokea miaka hii ya karibuni, vile vile naelewa na nafahamu hathari zake kwa mtendwa.... Ninacho sisitiza mimi ni kuwa kwa herufi kubwa and bold:
WATU WAFUATE TARATIBU ZA KISHERIA NA SIO KULETA MAMBO KWENYE TOVUTI... KILICHO WAFANYA WASHINDWE KWENDA POLISI NI KITU GANI?