"Baba Yenu anaumwa kichwa, nendeni mkacheze nje"

"Baba Yenu anaumwa kichwa, nendeni mkacheze nje"

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
15,835
Reaction score
23,776
Kipindi tukiwa watoto, baba unakuta amesafiri, kaenda zake shamba wiki mbili au tatu, akirudi unaona mama kapika ugali-kuku na maziwa ya mgando ,mchicha pembeni na pilipili kichaa vijana wa mjini wanaita mwendokasi.

Asubuhi tunatumwa sokoni kuandaa karanga mbichi na mbata, alafu mama anasema baba yenu anakuja leo.

Basi wote tunafuraaahi kweli kweli ,baba anarudi, khee, akija anatusalimia, anaenda zake kuoga, tunamrukia rukia anatupa zawadi ya maembe sindano/kunyonya, dodo ,lawa-lawa na mapera alafu unasikia mama anasema "msimsumbue baba yenu anaumwa kichwa, anaenda kulala , msimsumbue, leo nawapa rukhsa mkacheze kwa mama Mwakitobo ila msiumizane"

SWALI : Hii mbinu wazazi wa kisasa mnaitumia?

WATOTO.jpeg
 
Zamani kulikuwa na ujenzi wa polisi post choo nje ,kwasasa nyumba ni self contained ,watoto wana sebule yao ,chumba cha baba kipo mbali na sebule ,watoto wakiwa wanacheck cartoon au movie hawajui chochote kinachoendelea.
 
Back
Top Bottom