Baba yetu amefariki lakini hakuacha wosia wowote

Acha wauze nyie inawahusu nini maana mnataka kudhulumiana hapa
 
Upande wetu hatuna shida hatuwezi kuingia kwenye vita .

Mimi nachosema wakitaka kuuza mali ya kule mjini wauze lakini kwa masharti haya..

Asiwepo wakuja kukaa kwenye nyumba aliyojenga baba yangu pindi yupo na mama yangu mzazi na wakiuza kule wasijihesabu huku tena maana watakuwa wameweka utengano , lakini wakiweka ushirikiano kwamba mali zote zibakie salama asiwepo wakuuza itapendeza .
 
Mirathi watu hugeukana na kuzulumiana so na hao watoto wajiandae kwa lolote tu,
 
Mkuu poleni sana, ila mahakama inasimamia tu mgawanyo kisheria, huwa haishughuliki na migogoro/chuki zitakazotokea.

Keenye mirathi hauwezi kuikwepa mahakama sababu ndio wahusika wa kuwaizinisha wasimamizi wa mirathi na watekelezaji wa wosia.

Kwenye kesi yenu ukiiangalia vizuri utakuja kugundua waliosababisha imeenda mbali zaidi ni nyie nyie wahusika.

Huwa mwanzo kabisa akitokea mtu akapinga jambo ni bira mkamsikikiza sana na kufikia azimio la pamoja msilazimishe jambo sababu mnapokwenda mahakamani kuomba kupitishwa kwa msimamizi wa mirathi akienda kuwapinga tayari mchezo unabadilika na kuanza kuwa mgumu.

Haya mambo ya mirathi hayaitaji kabisa ubabe wala ule ukubwa wa umri kwamba wazee wamesema ndio mwisho inahitaji zaidi majadiliano
 
Mzizi ni baba, yeye anahusika na watoto wote. Kugawa mali kwa mujibu wa ndoa sijui imekaaje ila nadhani inapaswa kubadilika.

Kijijini ndio chimbuko lilipo, kama wa kwa mke mdogo wanaendelea kujitambua kwa ubini wai, basi kijijini ni kwao pia na nyumba ya baba yao ndio kwao haswa.

Mila nyingi, nyumba/eneo litakalotumika kutambulisha ubini wenu, huwa linarithishwa kwa mtoto wa kwanza wa kiume au wa mwisho wa kiume, na kila mtu anakuwa na access ya kufikia hapo!

Kwa minajiri hiyo, wekeni mali zote mezani, nyumba ya wote itakayokuwa kijijini iachwe kuwa ya wote, zilizobaki bila kujalj zilichumwa wakati gani, zigawanywe kwa kuzingatia utegemezi wa watoto, mdogo zaidi na kama yuko shule anapata kwa asilimia kubwa zaidi ya wengine ili imsaidie na yeye kusogea.

Kisha kama kuna kwere, basi taratibu za kikwere kwere ziendelee.
 
Hayo yote mtayamaliza kwa consensus na siyo legal battle mahakamani itawapotezea muda tu.

Go talk to your kinsmen mtaelewana tu hakuna kinachoshindikana kwenye mazungumzo.
 
Mirathi watu hugeukana na kuzulumiana so na hao watoto wajiandae kwa lolote tu,
Mkuu hatuko hivo , sisi vijana wakubwa wa marehemu kila mtu ana maisha yake wala hakuna mwenye tamaa na mali alizoacha mzee maana hata huku kijijini alijenga vzr sana kuliko hata mjini .

Ila tizama kwanini mzee wangu alifia mjini na akaletwa kijijini huoni kuwa shina ni kijijini , kwahiyo ni vema sisi kama watoto wa marehemu tukaendeleza kila alichokiacha marehemu ?

Maana hata wakati anaishi alisema tusiwaache wadogo zetu maana ni damu yetu.

Je kwanini tusiishi kwa upendo na ikawepo amri asiwepo wakuuza mali za marehemu ?

Ombi langu lilikuwa kama hivo na nilishawasilisha upande wa wazee waliobakia
 
Ww una umri gani?
 
Mkuu swala la watoto kusom tushasema tutampana nao na watasoma kama sisi tulivyosoma hata kama ni kwa shida na raha watasoma kikubwa Mungu azidi kubariki kazi ya mikono yetu .

Nimesoma kufikia level fulani na natamani wadogo wangu nao wapate elimu ili iwasaidie maishani mwao.
 
Sababu kuna wanasheria wabinafsi sana, watakupotezea hela na muda.
 
Hayo yote mtayamaliza kwa consensus na siyo legal battle mahakamani itawapotezea muda tu.

Go talk to your kinsmen mtaelewana tu hakuna kinachoshindikana kwenye mazungumzo.
Kweli mkuu ila nilitamani kuona mali zote alizoacha mzee wangu zikiendelea kusalia mikononi mwa wanao. Maana km ni pesa huwa inaisha ila mali kama kiwanja haiishi
 
Ushauri Msiuze Kitu Chochote Kwanza. Muwe na mpango mzuri kabisa wa kuwasaidia. Kama ww ni kaka mkubwa, tafuta ndg wa karibu mwenye hekima, haki, na mwaminifu sana akusaidie.
 
Ila hatua ya kwanza, ni kujua mahitaji ya watoto hao, ni hela kiasi gani inahitajika, na mambo ya kuuza ni baadaye tena Muuze Kwa Bei ya FAIDA na sio ya hasara.
 
Umri wangu ni miaka 27 .
Una umri mzuri tu kuwasaidia vizuri. Kumbuka penye hela mikono mingi itawekwa.. Pia Nenda Mahakama na ww upewe Haki za kusimamia Mali. Na USIOGOPE KUWA MKALI UKIONA MTU ANALETA UROHO KWENYE MALI NA HELA ZISIZOMHUSU.
 
Kweli mkuu ila nilitamani kuona mali zote alizoacha mzee wangu zikiendelea kusalia mikononi mwa wanao. Maana km ni pesa huwa inaisha ila mali kama kiwanja haiishi
Hayo yote mtakubaliana nyumbani na hili linahitaji ushauri wa kisheria?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…