Pole sana Mkuu, maswali yako nitajitahidi kukujibu kwa mfumo wa maswali pia:
1. Baba yenu alikuwa anafuata mfumo gani wa maisha?, Nakuuliza hivi kwa sababu kwenye murathi kuna aina tatu za mfumo wa maisha ambayo ni:-
A. Mfumo wa kimila
B. Kikristu
C. Kiislamu
Sasa kama alifuata mfumo wa kimila mali zake zitagawanywa kwa mfumo au taratibu za kabila lenu, ila hapa kuna swala la ndia, sasa je alioa kimila?, na je ndoa zilisajiliwa?, na je alimtalaki mama yako?
Haya maswali muhimu kuyajibu ili tuelewe uelekeo wa kimfumo utaegemea bado hapa
Kama alifuata mfumo wa maisha ya kikristu, hapa ni kama alibatizwa/aliokoka na kuishi kwenye misingi ya dini za kikristu, huu mfumo utaleta utata kwenye hizi ndoa mbili endapo ta awali haikuwa na talaka. Ikumbukwe pia mfumo wa kikristu ndio mfumo unaoangaliana zaidi na sheria za kiserikali, sasa hapa ndoa ni ya mke mmoja, na hazifuatani mbili labda pawepo talaka, je talaka ipo?
Kama alifuata mfumo wa kiislamu, hapa utafuatwa ule utaratibu wa mgawanyo ulioelekezwa kwenye quorani, hapa ndoa zinaruhusiwa hadi nne hivyo kama hamna talaka na alioa kidini haitasumbua sana.
SASA, tuendelee hapo kwenye swala la mali kama wanaweza kuuza na kuja kuishi hapo kijijini.
Ipo hivi jambo muhimu kwanza ni kufanya vikao vya ukoo/familia ili mteue msimamizi wa mirathi hapo mtayajadili yote kwa maslahi ya watoto, hakikisheni mnajua nani atakuwa na jukumu la kuwalea hao watoto hii itategemea taratibu zenu inawezekana nyie wakubwa mkawaangalia wadogo zenu.
Msimamizi wa mirathi atafanya maombi mahakama ya mwanzo, kusipokuwa na mgogoro ni ahueni, ila hakikisheni mnajali maslahi ya watoto kwenye kikao maoema kabisa.
Swala la kuuza mali haliwezi kuamuliwa juu juu bila kuwepo msimamizi wa mirathi aliyeizinishwa na mahakama, mkiuza kiholela baadae mtapata migogoro ndugu.
Pia kila mtoto anayo haki ya kurithi mali za baba yake, swala ni kuzitambua mali za marehemu baba yenu ni zipi na hivyo kuzigawanya kwa taratibu sahihi.
Kila la kheri Mkuu. Ukiwa na swali usisite kuniuliza.
Karibu.