Baba yetu amefariki lakini hakuacha wosia wowote

Baba yetu amefariki lakini hakuacha wosia wowote

Hata kisheria nikifahamu itapendeza zaidi , mimi na wadogo zangu sina makuu nao , kama sheria itaruhusu wauze kule mjini kwa sababu wamezaliwa kule na wakaishi kule mpaka kifo cha wazazi ,wala haina shida na sisi wa kwa upande wa mke wa kwanza tubakie na kiwanja cha kijijini na nyumba zakijijini siyo vibaya kikubwa tu wasijaribu kuja kuishi huku wala kuomba kiwanja maana watakuwa wameweka utengano.
Kwa haya maelezo yako ni wazi kabisa huna nia njema na hao watoto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa haya maelezo yako ni wazi kabisa huna nia njema na hao watoto.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu nina nia njema maana kama wataamua kuuza kule walikoishi na wazazi wao ina maana kabisa wameweka utengano na kama wataweka utengano sisi hatutahangaika nao .

Pia sitakuwa tayari kushirikiana nao .
 
Historia kwa ufupi.

Mzee wangu alioa mke wa kwanza na alikuwa amejenga nyumba kubwa na ndogo na akabahatika kuzaa nae watoto wanne wote wakiume (04).

Baada ya hapo waliaachana na mama yangu mzazi kwa sababu mama yangu aliugua sana akamtibisha bila kupata auhueni.

Ilipofika mwaka 2002 alioa mke wapili wakaishi nae hapa kijijini kwetu kwa muda mfupi na baada ya hapo walihamia mjini na huko mjini waliondoka tayari mtoto wakwanza akiwa ashazaliwa tayari , walipoenda mjini walinunua kiwanja na kubahatika kuzaa nae watoto sita (6)wote kwa ujumla upande wa mama mdogo, wakike wanne (04) na wakiume wawili (02).

Huko mjini walinunua kiwanja na wakajenga nyumba ya kuishi , pia wkt wa uhai wao walijenga msingi wa nyumba kubwana ipo mjini katikati .

Ilipofika tarehe 13.07.2021 nilipata taarifa baba yangu katangulia mbele za haki kwa ajali ya moto na mama mdogo pia yuko khali mbaya sana naye ilipofika tarehe 17.07.2021 akafariki pia.

Kibaya zaidi mzee wangu hakuacha usia wa aina yoyote.

Pia wakati tumeweka majadiliano ya kuwalea watoto wadogo waliobakia tulisema shina la watoto wote wa marehemu ni hapa kijijini.

Je wale watoto wa Ma. Mdogo wana uwezo wakusema kiwanja cha kule mjini kiuzwe kwa ajili ya kuwasaidia? Na Je wakiuza wanaruhusiwa kuja kwenye nyumba aliyojenga baba yetu kijijini enzi yupo na mke wa kwanza ?

Pia naombeni ushauri wenu wakisheria zaidi.
Lazima ujue warithi hawana wosia. Pili wote nyinyi ni warithi na laana itawajia nyinyi wakubwa mtakapo wanyanyasa wadogo zenu, Msisahau hilo..

Hekima iwe juu yenu..
 
mi naona wote mnahaki ya kurithi ,Kwa upande wa Baba .

Wote mnahaki sawa na ni warithi halali wote.

Huyo mama yenu ambaye ni mgonjwa naye ataingia kama mrithi halali kwenye ile nyumba aliyojenga akiwa na mumewe.

Yeye hatahusika kwenye mgao wa nyumba aliyojenga mumewe akiwa na mke mdogo.

Ila nyie watoto wote kwa pamoja mnahaki ya kuzirithi mali zote za baba yenu kwa upande wote

Mimi siyo mwanasheria ila kwa uelewa wangu nafikiri ni hivyo.
Lakini ndugu yangu naona inakuwa ngumu umefafanua vzr na nimekuelewa .

Shida ni moja kwanza mpaka sasa watoto wa kwa mke mdogo wamekaa kwa upande wa mama yao alikozaliwa.

Kaka yangu mkubwa ameomba watoto wasisambaratishwe wakae sehemu moja lakini imeshindikana .

Maana baba zetu wakubwa wanadai kwamba mtoto anawajibu wakuchagua wapi aende kulelewa ila mimi kuna kauli nainukuu ¶YATIMA HACHAGUI MLEZI¶

Sasa mbona watoto wanaanza kuchagua wakae kwa upande wa mama yao wakati upande wa baba yao wanajiweza na wapo tayari kuwalea watoto ?

Mimi kuna kitu nimehisi kuwa wale watoto wamepandikizwa sumu yakuuchukia upande wa baba yao.

Je wale watoto wote tukiwahitaji wakae kwa kuwalazimisha kwetu kwa sababu ni wadogo zetu hivi inakataa kweli ?

Naombeni ushauri.
 
Tatizo la mitoto ya sikuhizi imekalia kusubiria urithi tu na hapo ndio chanzo cha migogoro, ushauri mdogo tu achaneni na masuala sijui ya kuuza sijui kugawana sijui nini kama eneo ni prime kaeni wote hakuna cha mke sijui mdogo wala mkubwa wote watoto, fanyeni kitu cha maana kwa maendeleo yenu wote kinachofanya hii migogoro iendelee ni ubinafsi, mtu akishaanza kusema sijui mke mdogo sijui mkubwa hapo ndio shida inaanzia , nyie kama watoto wote baba yenu alikua mmoja , pambaneni muelewane muishi kwa amani hizo mali kwanza hazikuwa zenu hilo mosi, pili ulishawahi kusikia msiba wa masikini watu wanagombania mali? tafakari, wosia sio ishu sikuhizi
Shida ni moja ndugu yangu sisi tulipenda tukae na wadogo zetu lkn chakushangaza ilishindikana wamechagua wenyewe etii wakae kwa mama zao wadogo , je tutawalazimisha tuwe wamoja ?
 
Back
Top Bottom