Yaani ungeelewa point yangu ni kwamba mahitaji ya watoto tupo tayari kuhangaika nao , kwa sababu sisi wakubwa tuna uwezo wakuwalea , ila nilichotamani kusikia asiwepo wakusema kiwanja kiuzwe haswa watoto aliowaacha mama mdogo .Ila hatua ya kwanza, ni kujua mahitaji ya watoto hao, ni hela kiasi gani inahitajika, na mambo ya kuuza ni baadaye tena Muuze Kwa Bei ya FAIDA na sio ya hasara.
Nami hapo ndo nataka nisimamie kabisa ,Una umri mzuri tu kuwasaidia vizuri. Kumbuka penye hela mikono mingi itawekwa.. Pia Nenda Mahakama na ww upewe Haki za kusimamia Mali. Na USIOGOPE KUWA MKALI UKIONA MTU ANALETA UROHO KWENYE MALI NA HELA ZISIZOMHUSU.
KUZIKWA ni jambo lingine na mali ni kitu kingine...maiti aiwezi kutupangia sehemu ya kumzika...ila mtu awezi kupangiwa pia jinsi ya kutumia mali zake...kama mlikuwa familia 2....kila familia imejengewa na imewekewa aset zake...nyie bakini na zakwenu na madogo nao waachieni mali zao wakikuwa wataziendeleza...kisiuzwe kitu chochote....naongea kwa niaba ya marehemu mzazi wenuHilo linawezekana lkn wao bado wadogo sana na siku zote kikao chetu kiliazimia shina la watoto wote wa marehemu ni hapa kijijini . Je mtoto akifa azikwe tofauti na kwenye shina la baba yake ?
Hili ndiyo jibu sahihi.Kwenye hili suala ninavyoona mimi
Kama kutakua hakuna kugombea mali kila mtu akae kwenye mji wake
Hao watoto wadogo mali ya baba yao iwe chini ya uangalizi wa mtu wakifikisha umri wakujitambua wakambiziwe
Ukisema hivo tukiwaachia kiwanja wakauza
Mama yenu yuko wapi?naishi nae?baba alijenga kwenye eneo la ukoo au alinunua?Walianzia kuishi hapa kijijini kwenye nyumba aliyojenga baba yangu na mama yangu mzazi baada ya hapo walihama wakiwa na mtoto mmoja tayari , hawakugawana mali .
Sasa mkuu unataka aende kulimaliza kujadili kifamilia bila kujua chochote atachangia nini? Hata akienda kwa mwanasheria ataenda bila A,B,C na ushauri wa kwenda kwa mwanasheria anaweza upata hapahapa. Umeitwa kwenye interview, umeenda kama mbumbumbu hujui lolote kuhusu hiyo organization na hints zake utajibu nini sasaHilo kwanza siyo suala la kisheria ni suala la kumaliza kwenye familia tu.
Suala dogo kama hilo unahitaji ushauri wa kisheria ?
Kwanini hakuenda kwenye ofisi ya wakili akapata ushauri mdogo tu ambao hauhitaji kuanika family affairs kwenye mitandao japokuwa anatumia fake identity ?
Baada ya hapo waliaachana na mama yangu mzazi kwa sababu mama yangu aliugua sana akamtibisha bila kupata auhueni.
Pole kwa kufiwa. Lakini nashindwa kujizuia kusema hili. Something wrong here! Yaani mwenza wako akiugua sana, unamwacha? Wakati ambao mweza wako anakuhutaji sana, unamwacha! Halafu unaoa mwingine? Mambo mengine ni magumu kuelewa.
Mkuu nahisi wamjini wabaki mjini na mali zao na nyie wakijijini bakini na mali zenu.Mimi ni mtoto kwa upande wa mke wa kwanza , mama yangu yupo hai lakini ni mgonjwa mpaka sasa. Ila kama nilivyoeleza hapo juu kwenye Uzi upande wa wadogo zetu na mama yao nae katangulia mbele za haki.
Mkuu naomba nikusahihishe hapa kidogo, kisheria watoto wote wa marehemu wana haki ya kurithi mali za baba yao. Hili swala kuna kesi zinazoliongelea na sababu ni ule msemo maarufu wa 'kitanda hakizai haramu' plus sheria ya mtoto ya 2009 plus mambo ya haki za binadamu.Bila kupepesa macho nyie hapo hamna chenu maana mama yenu hakufunga ndoa na Baba yenu,hivyo kisheria hatambuliki anayetambulika na huyo Mama yenu mwingine kama mkiamua kufuata mkondo wa kisheria,
Lakini cha kufanya haya mambo muyamalize kifamilia tu bila kuoneana wivu maana miyapeleka kisheria yatawagawa sana na kuwa acha na ugomvi mkubwa sana.!
Hatujaelewana nadhani , maana yangu ni kwamba wale watoto wa mke wapili wakishawishiwa kuuzwa kiwanja chao je , sisi kama watoto wa wakubwa wa marehemu tuna pingamizi? Binafsi nilitamani tupaendeleze mjini ikiwezekana tuwe wamoja mwenye pesa apaendeleze kwa kujenga nyumba lkn iwe asset yakuwasaidia ambao bado ni watoto wadnaona
Ahsante , lakini hakuna namna mkuu maamuzi ya mzee aliona kwake ni sahihi .Pole kwa kufiwa. Lakini nashindwa kujizuia kusema hili. Something wrong here! Yaani mwenza wako akiugua sana, unamwacha? Wakati ambao mweza wako anakuhutaji sana, unamwacha! Halafu unaoa mwingine? Mambo mengine ni magumu kuelewa.
Wanaongelewa ni watoto. Suala la ndoa halina athari kwenye urithi wa watotoPole sana Mkuu, maswali yako nitajitahidi kukujibu kwa mfumo wa maswali pia:
1. Baba yenu alikuwa anafuata mfumo gani wa maisha?, Nakuuliza hivi kwa sababu kwenye murathi kuna aina tatu za mfumo wa maisha ambayo ni:-
A. Mfumo wa kimila
B. Kikristu
C. Kiislamu
Sasa kama alifuata mfumo wa kimila mali zake zitagawanywa kwa mfumo au taratibu za kabila lenu, ila hapa kuna swala la ndia, sasa je alioa kimila?, na je ndoa zilisajiliwa?, na je alimtalaki mama yako?
Haya maswali muhimu kuyajibu ili tuelewe uelekeo wa kimfumo utaegemea bado hapa
Kama alifuata mfumo wa maisha ya kikristu, hapa ni kama alibatizwa/aliokoka na kuishi kwenye misingi ya dini za kikristu, huu mfumo utaleta utata kwenye hizi ndoa mbili endapo ta awali haikuwa na talaka. Ikumbukwe pia mfumo wa kikristu ndio mfumo unaoangaliana zaidi na sheria za kiserikali, sasa hapa ndoa ni ya mke mmoja, na hazifuatani mbili labda pawepo talaka, je talaka ipo?
Kama alifuata mfumo wa kiislamu, hapa utafuatwa ule utaratibu wa mgawanyo ulioelekezwa kwenye quorani, hapa ndoa zinaruhusiwa hadi nne hivyo kama hamna talaka na alioa kidini haitasumbua sana.
SASA, tuendelee hapo kwenye swala la mali kama wanaweza kuuza na kuja kuishi hapo kijijini.
Ipo hivi jambo muhimu kwanza ni kufanya vikao vya ukoo/familia ili mteue msimamizi wa mirathi hapo mtayajadili yote kwa maslahi ya watoto, hakikisheni mnajua nani atakuwa na jukumu la kuwalea hao watoto hii itategemea taratibu zenu inawezekana nyie wakubwa mkawaangalia wadogo zenu.
Msimamizi wa mirathi atafanya maombi mahakama ya mwanzo, kusipokuwa na mgogoro ni ahueni, ila hakikisheni mnajali maslahi ya watoto kwenye kikao maoema kabisa.
Swala la kuuza mali haliwezi kuamuliwa juu juu bila kuwepo msimamizi wa mirathi aliyeizinishwa na mahakama, mkiuza kiholela baadae mtapata migogoro ndugu.
Pia kila mtoto anayo haki ya kurithi mali za baba yake, swala ni kuzitambua mali za marehemu baba yenu ni zipi na hivyo kuzigawanya kwa taratibu sahihi.
Kila la kheri Mkuu. Ukiwa na swali usisite kuniuliza.
Karibu.